Hasara ya mabilioni ya dola baada ya mfereji wa Suez kuzibwa na meli kubwa ya mizigo

Hahahaaa ndio mkuu ulidhani ni rubani??

Kwanza pia kunakua na Nahodha mwenyeji anayeletwa na hizo Tug boat anasaidiana na Nahodha wa hiyo meli kuivusha hapo, naye pia anaitwa Pilot.

Hata baadhi ya bandari(Pamoja na DSM nadhani) meli huwa zinaenda kupokelewa na Pilot mwenyeji wa hiyo bandari kuepusha matatizo kama hayo.

Ni kama wale madereva wa Dar wanaopokeaga madereva wa serikali kutoka kasulu huko Pale kibamba wa nazunguka na bos wakimaliza wanawarudisha mpaka kibamba warudi kwao bara
Correct! 👏🏽
 
Hii system vipi?
 
Attachments

  • Screenshot_20210328_121216.jpg
    Screenshot_20210328_121216.jpg
    89.1 KB · Views: 2
Sababu kubwa ya meli hiyo kukwama pale ni baada ya steering system (mfumo wa usukani) kufeli, maelezo kutoka kwa watu wa Marine Casualty Investigation.

Kweli kitu kikiwa majini kinakuwa chepesi, aina ya ajali hiyo ya Ship Grounding ni kukwama kwa meli kwenye mchanga au tope. Na hiyo mgongo wa meli umenasa kwenye tope.
Mkuu hivi ni kwanini bandari nyingi hapa Bongo zimejificha, yaani huwezi kuifikia gati bila kupita kwenye strait!?
 
Ndugu bado ujaona meng io ni chq mtoto tu kuna manowar za marekan kubwa km wilaya ua temeke uko unaweza hata kisahau km upo kwenye meli kuna mpaka daladala humo
Meli kubwa zaidi ni za mizigo. Kama sijakosea manowari kubwa ina urefu wa meters 300 sawa na viwanja vitatu vya mpira
 
Mkuu hivi ni kwanini bandari nyingi hapa Bongo zimejificha, yaani huwezi kuifikia gati bila kupita kwenye strait!?
Bandari kuwa eneo lililojificha ni salama zaidi kama ilivyo kwa hizi zetu. Hii inasaidia meli kama ikiwa imefungwa kwenye gati isipigwe na upepo mkali kutoka baharini au mawimbi na kukata kamba na kusababisha maafa au wakati wa kuingia meli kupata tabu baada ya upepo kupiga Sana inakuwa vigumu kufunga kwenye gati.

Bandari kama haijajificha italazimu kujenga kingo kubwa kuzuia upepo na mawimbi.

Mfano bandari ya Bukoba ipo eneo la wazi hivyo meli pale hupata tabu wakati wa kuingia, hata kuna tukio liliwahi kuripotiwa miaka ya nyuma meli ya MV Victoria ilishindwa kuingia na kuleta taharuki ila halo ilipo kaa shwari ikaingia gatini.

Hii hapa chini ni bandari ambayo haina eneo la kujificha au Kati ya milima/miamba.Imebidi ijengwe kingo(breakwater) za kuzuia mawimbi na upepo ili meli zisipate shurba na kuwa salama.
images.jpeg

Bandari kama ya Dar es Salaam iliyojificha baada ya kupita kwenye strait/mlango ipo salama dhidi ya upepo na mawimbi.
images (1).jpeg
 
View attachment 1736828
Bandari kama ya Dar es Salaam iliyojificha baada ya kupita kwenye strait/mlango ipo salama dhidi ya upepo na mawimbi.
View attachment 1736833
Umemaliza mkuu, nikijiuliza sana juu ya hili, now nimeelewa. Asante sana.
 
Nimeona kwenye platforms conspiracy kuwa huenda ajali imetengenezwa: nakaribia kushawishika hivyo maana si rahisi tani "LAKI2* kusukumwa na upepo
Meli ya urefu na upana huo ina surface area kubwa sana mkuu, ni kma ukuta unaoelea kweny maji mbele ya upepo wa hata 50kph inasukumwa vzuri tu.
 
View attachment 1734844
Juhudi zinaendelea

Wakuu hili dude ni kubwa wazee unaona Excavator inavyoonekana kama kagari kadogo hapo

Ila Suez Canal Authority wanatia aibu mpaka leo hii wameshindwa kumobilise vifaa vya maana kama Crwalers au monster excavators wanatumia hako ka barabara

Au nilitegemea nione/nisome kuwa Underwater Sand pumps zinatumika hapo kutoa tope inasuke meli
Pesa wanazoingiza sijui wanazipeleka wapi
 
Back
Top Bottom