Hasara ya mabilioni ya dola baada ya mfereji wa Suez kuzibwa na meli kubwa ya mizigo

Meli kubwa sana hiyo,viwanja vinne vya mpira!ukitafakari utagundua hawa wenzetu wako mbali sana...
Huku kwetu sifa ya Mbunge/mtunga sheria na mpitishaji wa badget ya serjali sifa kubwa ni kujua kusoma na kuandika maendeleo yatatoka wapi?
 
Mzee unaujua upepo mkali? Kumbuka meli inakuwa kwenye maji sio nchi kavu
Nenda platforms nyingine uone kinachosemwa; sasa wanapambana na siltation, wanapakua mizigo iliyo kwenye ncha ili uzito uongezeke katikati. Upepo wa nchikavu si sawa na baharini kwahiyo hoja ya upepo ni dhaifu
 
Kama unataka kuwasingizia mabeberu, nakuhakikishia Mabeberu hawawezi kuwa stupid kiasi hicho kwa sababu Suez Canal ni muhimu hata kwao! Hebu angalia hiyo alternative route
Kwa dunia ya leo yote yanawezekana: kutaka kuliondoa hilo dude maana linaushindani mkubwa dhidi ya vyombo vyao ama kumtia hasara egypt ya kuingiza fedha nyingi zaidi za kuboresha suez
 
Kwa dunia ya leo yote yanawezekana: kutaka kuliondoa hilo dude maana linaushindani mkubwa dhidi ya vyombo vyao ama kumtia hasara egypt ya kuingiza fedha nyingi zaidi za kuboresha suez
Egypt ni "mpwa" wa Mabeberu!!! Mfereji ungekuwa unamilikiwa na Iran basi hiyo dhana yako ingewezekana; sawa na ile dhana ya kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku, lakini sio kwa Egypt. Mabeberu wanaihitaji sana stable Egypt kwa ajili ya Israel kama wanavyoihitaji Turkey kwa manufaa ya NATO, na ndo maana, kama sitakosea, after Israel, Egypt ndiyo inafuata kwa kupata misaada mikubwa zaidi ya kijeshi kutoka USA.
 
Nenda platforms nyingine uone kinachosemwa; sasa wanapambana na siltation, wanapakua mizigo iliyo kwenye ncha ili uzito uongezeke katikati. Upepo wa nchikavu si sawa na baharini kwahiyo hoja ya upepo ni dhaifu
Duuu! Basi sawa kila mtu aamini anachoamini,
_117720946_evergiven_salvage_1_640-2x-nc.png
 
Egypt ni "mpwa" wa Mabeberu!!! Mfereji ungekuwa unamilikiwa na Iran basi hiyo dhana yako ingewezekana; sawa na ile dhana ya kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku, lakini sio kwa Egypt. Mabeberu wanaihitaji sana stable Egypt kwa ajili ya Israel kama wanavyoihitaji Turkey kwa manufaa ya NATO, na ndo maana, kama sitakosea, after Israel, Egypt ndiyo inafuata kwa kupata misaada mikubwa zaidi ya kijeshi kutoka USA.
Bado hujaondoa dhana kuwa ajali hii inaweza kuwa organized, vipi compliance ya viongozi wa sasa wa egypt kwa matakwa ya wazungu, vipi kuhusu ku block njia ili waratibu vizuri global petroleum supply? Vipi kuhusu ku block njia ili wakague kijasusi vyombo vingine⁉️, vipi kuhusu kutaka dude hili likose biashara huko mbeleni ⁉️
 
Bado hujaondoa dhana kuwa ajali hii inaweza kuwa organized, vipi compliance ya viongozi wa sasa wa egypt kwa matakwa ya wazungu, vipi kuhusu ku block njia ili waratibu vizuri global petroleum supply? Vipi kuhusu ku block njia ili wakague kijasusi vyombo vingine⁉️, vipi kuhusu kutaka dude hili likose biashara huko mbeleni ⁉️
Man, hata tukiacha mambo ya siasa, Suez Canal ni MUHIMU sana kwa Mabeberu!! Wakati Egypt anapoteza kupitia ushuru lakini Ulaya na America wanapoteza biashara kubwa sana, tena sana kuliko ushuru wanaopoteza Egypt! Kutokana na ile ajali, cargo flow kati ya Asia na nchi za Mabeberu kupitia bahari imesimama, labda wa-opt hiyo long route ambayo na wenyewe wana mashaka nayo kutokana na Somali Pirates! Ajali imetokea juzi tu hapa lakini taarifa ya Leth Agencies iliyotolewa 7 hours ago inaonesha kuna meli 326 zimekwama!!! Sasa turudi upande wa pili, je zikikwama zitabaki zinaelea baharini? Hapana, na ndo maana kwa mujibu wa hiyo taarifa, inaonesha meli 1017 zimetia nanga bandari ya Port Said, na 127 zimetia nanga bandari ya Suez. Sasa anayeumia hapo nani kati ya Egypt na Mabeberu?! Labda Egypt wasiwatoze kwa kuwa hizo bandari na mfereji zote zipo kwenye mamlaka yake lakini hasara ya kuendelea kubaki tu hapo bandarini and around the canal, ni hasara kubwa sana sio tu in terms of money bali kwa mfumo mzima wa usambazaji wa bidhaa!!

Kwamba kutaka dude likose biashara huko mbeleni bado ha-make sense kwa sababu Egypt sio threat kwa Mabeberu kiasi cha wao kufikiria ku-risk biashara na Asia + Far East kilofa namna hiyo! Mabeberu wanaweza kuwa na njia 10 kidogo za kumfanya Egypt asipumue bila ya wao mabeberu kuathirika lakini njia hiyo katu haiwezi kuwa kui-block Suez Canal. Kilichotokea Suez kinatokea hata kwenye hizi bandari za kawaida ambazo sio natural habors. Na ndo maana bandari kama Dar es salaam katu mmeli kama ule hauwezi kuja kwa sababu lazima itatanasa tu!! Sasa sijui mara ya mwisho ni lini kwa Egypt kuhakikisha bado kina kipo vizuri au inawezekana nahodha alibugi step akapita sehemu ambayo hakutakiwa kupita!
 
Hiyo ajali hakuna mkono wa mtu, meli hiyo ilinasa hapo(Grounding) baada ya mfumo wa steering kufeli na hapo ilikuwa under command ya pilot mzoefu wa hiyo Suez Canal.

Grounding kama hiyo ni ajali za kawaida Sana, ukiachana na ajali za kugongana uso kwa uso.
 
Mkuu wazo la kuzamisha sio rafiki hata kidogo, ukizamisha hapo huo mfereji hautotumika tena.

Ulaya Wana kampuni za kuokoa Zinaitwa Salvage, Wana vifaa vya kisasa tatizo linakuja Wana Bei kubwa Sana. Ndio maana Misri hawajawaita wanakomaa kama mamlaka na jeshi.
Afrika hatutaki kuwekeza ila tunataka maisha ya kufikirika
 
Nimeona kwenye platforms conspiracy kuwa huenda ajali imetengenezwa: nakaribia kushawishika hivyo maana si rahisi tani "LAKI2* kusukumwa na upepo
Kitu kikiwa kwenye maji kinakuwa chepesi.
 
🤓🤓🤓🤓 Nimeona kwenye platforms conspiracy kuwa huenda ajali imetengenezwa: nakaribia kushawishika hivyo maana si rahisi tani "LAKI2* kusukumwa na upepo
Zikiwa zinaelea kwenye maji ni rahisi sana mkuu
 
Kitu kikiwa kwenye maji kinakuwa chepesi.
Sababu kubwa ya meli hiyo kukwama pale ni baada ya steering system (mfumo wa usukani) kufeli, maelezo kutoka kwa watu wa Marine Casualty Investigation.

Kweli kitu kikiwa majini kinakuwa chepesi, aina ya ajali hiyo ya Ship Grounding ni kukwama kwa meli kwenye mchanga au tope. Na hiyo mgongo wa meli umenasa kwenye tope.
 
Kwamba kutaka dude likose biashara huko mbeleni bado ha-make sense kwa sababu Egypt sio threat kwa Mabeberu kiasi cha wao kufikiria ku-risk biashara na Asia + Far East
Kwani meli ni ya misri?!
 
Inaonekana meli kubwa kama hii zinapitaga labda kuna tatizo limetokea au baharia kakosea hesabu namna ya kulenga kwenye njia ndogo
meli ikifika hapo captain anazima na injin kabisa, hapo meli haiendeshwi inavushwa kwa kuvutwa na tug boats na mitambo mengine inayokuwa pemben kweny kingo za mfereji
 
Hasara ya mabilioni ya dola baada ya Mfereji wa Suez nchini Misri kuzibwa na meli kubwa ya mizigo
Mar 26, 2021 08:01 UTC

Inakadiriwa kuwa kuna hasara ya dola milioni nne kwa saa baada ya meli kubwa ya kontena kuziba Mfereji wa Maji wa Suez nchini Misri. Mfereji huo ni kati ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za meli za kibiashara duniani.


Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Lloyd List, baada ya meli hiyo kuziba Mfereji wa Suez, meli zilizokwama kuelekea upande wa maghairbi zinapata hasara ya dola bilioni 5.1 kwa siku na zile zilizokwama upande uneoelekea mashariki zinapata hasara ya takribani dola bilioni 4.5 kwa siku.

Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na Shirika la Habari la Bloomberg, hivi sasa kuna jumla ya meli 185 ambazo zinasubiri kupita Mfereji wa Suez. Miongoni mwa meli hizo kuna meli 27 kubwa za mafuta ambazo zina takribani mapipa milioni 1.9 ya mafuta ghafi ya petroli.

Meli iliyoziba Mfereji wa Suez ina urefu wa mita 400 sawa na viwanja vinne vya mpira wa miguu na imekwama kwenye mfereji wa Suez unaounganisha Bahari ya Mediterania na Bahari ya Sham na hivyo kuzuia meli kupita huku shughuli mbalimbali muhimu zikivurugwa. Kukwama kwa meli hiyo kumesababisha bei ya mafuta kupanda kwenye masoko ya kimataifa.

Karibu asilimia 12 ya biashara ulimwenguni hupita katika mfereji wa Suez na ni njia ya mkato kati ya Bara la Asia na Ulaya. Meli hiyo iliyosajiliwa nchini Panama na kuendeshwa na kampuni ya usafirishaji ya Evergreen, ilikuwa ikielekea bandari ya Rotterdam nchini Uholanzi ikitokea China na ilikuwa ikipita Kaskazini kupitia mfereji huo kuelekea Mediterranean. Meli hiyo ya tani 200,000 ilitengenezwa mwaka 2018.

Juhudi za kuikwamua meli hiyo zingali zinaendelea huku wakuu wa Misri wakisema huenda zoezi hilo likachukua siku kadhaa.

Meli ambazo haziwezi kusubiri zitalazimika kuzunguka bara Afrika ili kufika Ulaya na hivyo kurefusha safari kwa takribani wiki mbili zaidi.

Dah!
Kumbe kuna meli kubwa namna hii yenye ukubwa wa viwanja vinne vya mpira? Big up wazungu
Ndugu bado ujaona meng io ni chq mtoto tu kuna manowar za marekan kubwa km wilaya ua temeke uko unaweza hata kisahau km upo kwenye meli kuna mpaka daladala humo
 
Back
Top Bottom