Hasara ya mabilioni ya dola baada ya mfereji wa Suez kuzibwa na meli kubwa ya mizigo

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,590
32,672
Hasara ya mabilioni ya dola baada ya Mfereji wa Suez nchini Misri kuzibwa na meli kubwa ya mizigo
Mar 26, 2021 08:01 UTC

Inakadiriwa kuwa kuna hasara ya dola milioni nne kwa saa baada ya meli kubwa ya kontena kuziba Mfereji wa Maji wa Suez nchini Misri. Mfereji huo ni kati ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za meli za kibiashara duniani.

4bxz0ff283dc5b1ud2a_800C450.jpg

Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Lloyd List, baada ya meli hiyo kuziba Mfereji wa Suez, meli zilizokwama kuelekea upande wa maghairbi zinapata hasara ya dola bilioni 5.1 kwa siku na zile zilizokwama upande uneoelekea mashariki zinapata hasara ya takribani dola bilioni 4.5 kwa siku.

Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na Shirika la Habari la Bloomberg, hivi sasa kuna jumla ya meli 185 ambazo zinasubiri kupita Mfereji wa Suez. Miongoni mwa meli hizo kuna meli 27 kubwa za mafuta ambazo zina takribani mapipa milioni 1.9 ya mafuta ghafi ya petroli.

4bxz9b1c8c90e91ud2c_800C450.jpg
Meli iliyoziba Mfereji wa Suez ina urefu wa mita 400 sawa na viwanja vinne vya mpira wa miguu na imekwama kwenye mfereji wa Suez unaounganisha Bahari ya Mediterania na Bahari ya Sham na hivyo kuzuia meli kupita huku shughuli mbalimbali muhimu zikivurugwa. Kukwama kwa meli hiyo kumesababisha bei ya mafuta kupanda kwenye masoko ya kimataifa.

Karibu asilimia 12 ya biashara ulimwenguni hupita katika mfereji wa Suez na ni njia ya mkato kati ya Bara la Asia na Ulaya. Meli hiyo iliyosajiliwa nchini Panama na kuendeshwa na kampuni ya usafirishaji ya Evergreen, ilikuwa ikielekea bandari ya Rotterdam nchini Uholanzi ikitokea China na ilikuwa ikipita Kaskazini kupitia mfereji huo kuelekea Mediterranean. Meli hiyo ya tani 200,000 ilitengenezwa mwaka 2018.

Juhudi za kuikwamua meli hiyo zingali zinaendelea huku wakuu wa Misri wakisema huenda zoezi hilo likachukua siku kadhaa.

Meli ambazo haziwezi kusubiri zitalazimika kuzunguka bara Afrika ili kufika Ulaya na hivyo kurefusha safari kwa takribani wiki mbili zaidi.

Dah!
Kumbe kuna meli kubwa namna hii yenye ukubwa wa viwanja vinne vya mpira? Big up wazungu.

PIA SOMA>> Meli kubwa ya mizigo yashindwa kukwamuliwa katika Mfereji wa Suez kwa siku ya tatu
 
Hasara ya mabilioni ya dola baada ya Mfereji wa Suez nchini Misri kuzibwa na meli kubwa ya mizigo
Mar 26, 2021 08:01 UTC

Inakadiriwa kuwa kuna hasara ya dola milioni nne kwa saa baada ya meli kubwa ya kontena kuziba Mfereji wa Maji wa Suez nchini Misri. Mfereji huo ni kati ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za meli za kibiashara duniani.
View attachment 1734745
Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Lloyd List, baada ya meli hiyo kuziba Mfereji wa Suez, meli zilizokwama kuelekea upande wa maghairbi zinapata hasara ya dola bilioni 5.1 kwa siku na zile zilizokwama upande uneoelekea mashariki zinapata hasara ya takribani dola bilioni 4.5 kwa siku.

Kwa mujibu wa data zilizokusanywa na Shirika la Habari la Bloomberg, hivi sasa kuna jumla ya meli 185 ambazo zinasubiri kupita Mfereji wa Suez. Miongoni mwa meli hizo kuna meli 27 kubwa za mafuta ambazo zina takribani mapipa milioni 1.9 ya mafuta ghafi ya petroli.
View attachment 1734753
Meli iliyoziba Mfereji wa Suez ina urefu wa mita 400 sawa na viwanja vinne vya mpira wa miguu na imekwama kwenye mfereji wa Suez unaounganisha Bahari ya Mediterania na Bahari ya Sham na hivyo kuzuia meli kupita huku shughuli mbalimbali muhimu zikivurugwa. Kukwama kwa meli hiyo kumesababisha bei ya mafuta kupanda kwenye masoko ya kimataifa.

Karibu asilimia 12 ya biashara ulimwenguni hupita katika mfereji wa Suez na ni njia ya mkato kati ya Bara la Asia na Ulaya. Meli hiyo iliyosajiliwa nchini Panama na kuendeshwa na kampuni ya usafirishaji ya Evergreen, ilikuwa ikielekea bandari ya Rotterdam nchini Uholanzi ikitokea China na ilikuwa ikipita Kaskazini kupitia mfereji huo kuelekea Mediterranean. Meli hiyo ya tani 200,000 ilitengenezwa mwaka 2018.

Juhudi za kuikwamua meli hiyo zingali zinaendelea huku wakuu wa Misri wakisema huenda zoezi hilo likachukua siku kadhaa.

Meli ambazo haziwezi kusubiri zitalazimika kuzunguka bara Afrika ili kufika Ulaya na hivyo kurefusha safari kwa takribani wiki mbili zaidi.

Dah!
Kumbe kuna meli kubwa namna hii yenye ukubwa wa viwanja vinne vya mpira? Big up wazungu
Hii sasa ndiyo vita vya kiuchumi, siyo mtu anaumwa karibu na kukata roho lakini ukijaribu kusema anaumwa unaambiwa hiyo ni vita vya kiuchumi.
 
Back
Top Bottom