Hasara kubwa mbegu za alizeti (ASA)

Alizeti halitaki mvua nyingi,Songea Kuna mvua nyingi,mvua nyingi inasababisha mafuta yawe kidogo.Inawezekana tatizo siyo mbegu ila ni wewe mkulima.
Kweli kabisa kama alina wakati wa mvua nyingi hiyo ni sababu Moja wapo.

Jambo la pili ni ujazi wa gunia. Gunia la kawaida la wastani ni kg 55 kwa alizeti iliyokomaa vizuri ni 65-70kg ambayo inakupa hadi lita 22 kwa mbegu za kienyeji
 
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Vipi mavuno kwa heka umepata gunia ngapi?
 
Bado unaiaminigi serikali tu nunua mbegu zako kutoka kwa wazalishaji binafsi

Kingine Alizeti sio kama mpunga yenyewe inataka unyevu tu kwenye udongo inatosha

Inaonyesha ulikurupuka kulima bila kulifuatilia vizuri hilo zao la alizeti linataka nn

NB:Mkulima hutakiwi kuwa na hasira
 
Hakika umenena..mkulima hasa wa kilimo cha mvua hitakiwi kuwa na hasira ama kinyongo na kilimo.

Kubali hasara..jipange upya anza msimu mwingine kwa matumaini mapya.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kawaida 65kg hutoa 21 litres ko hyo 45kg walau ulpaswa upate 16+ litres kwa ushuhuda wa Manyara
 
Alizeti halitaki mvua nyingi,Songea Kuna mvua nyingi,mvua nyingi inasababisha mafuta yawe kidogo.Inawezekana tatizo siyo mbegu ila ni wewe mkulima.
Acha uongo wewe! Unakijua kilimo cha Alizeti wewe? Au ndio ninyi wahitimu wa SUA, theory nyingii!
 
Bongo nyoso...full kutukana hasara...usikute Kuna kigogo mmoja alikuwa winga katika ununuzi na uuzaji wa mbegu
Ndivyo ilivyo kwani hata Pembejeo za Ruzuku na mbegu za mahindi si ilikuwa hivyo hivyo. Wakulima tuna rungu la kuiwajibisha Serikali hii ili ituheshimu. Kupitia kura 2023. Sijui tunakwama wapi?
 
Kweli kabisa kama alina wakati wa mvua nyingi hiyo ni sababu Moja wapo.

Jambo la pili ni ujazi wa gunia. Gunia la kawaida la wastani ni kg 55 kwa alizeti iliyokomaa vizuri ni 65-70kg ambayo inakupa hadi lita 22 kwa mbegu za kienyeji
Uko sahihi. Isipokuwa mbegu hii Record iliyoletwa na Serikali 2021/2022 ni counterfeit hybrid seeds. Ni Fake. Na iko zaidi ya varieties Nne. Sina shaka ASA na baadhi ya Watendaji wachache wasio waaminifu wa Serikali wali-collude, wali-conspire, wali-accomplice ktk hili.

Serikali na Watendaji wako, waoneeni huruma Wakulima.
 
Hii ni hatari sana; ngoja tuendelee kusubiri mrejesho kwa wengine; kuna jamaa yangu kalima heka 50 bado haijaanza kutoa maua; nasubiri mrejesho wake.

Hizo aina tutaweza je kuzitambua?
 
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Gunia Zima lita 7, daah Kilimo kigumu sana...... wakulima tuwaheshimu
 
Wapi naweza pata aina hii ya mbegu.
FB_IMG_1654351912072.jpg
 
Habari wana jamvi,

Naomba kujua waliolima alizeti kwa kutumia mbegu za serikali za ASA mafuta zimetoa kiasi gani maana, hasara tuliyopata sye huku tuliolima Songea sio mchezo. Gunia la kilo 45 mafuta yametoka lita 7 tu, hivi hawa watafiti wa hizi mbegu mlisomea chini ya zizi la nguruwe au?
Katika hali ya kawaida Hilo gunia la kilo 45 hitoa mafuta lita ngapi?
 
Back
Top Bottom