Has Kikwete lost his "Legitimacy" to Lead?

Has Kikwete lost his "Legitimacy" to Lead?

Wakuu JF salaam,

- Wote tumeyasikia yote yaliyosemwa kwenye kongamano la Mwalimu's Foundation, infact hata Mangula naye amejitokeza na kusema yake kuhusiana na ubovu wa serikali ya sasa chini ya uongozi wa Rais wetu Mheshimiwa Kikwete, na cha kutisha sana ni pale Rais aliporudi nchini na kudai kwamba anajitayarisha kuwajibu wale wote tunaohisi kwamba uongozi wake una matatizo, na akadokeza kwamba wengi tunaomkosoa tunasumbuliwa na chuki za binafsi.

- Ninasema hivi, wakati Rais anajitayarisha kujibu mapigo ni vyema na sisi wananchi tukaweka wazi our case against Rais na serikali yake, tena with facts! Sasa tafadhalini sana ndugu zangu tujitahidini kuweka facts za mapungufu ya Rais wetu wa sasa, yaani Mheshimiwa Kikwete na serikali yake toka ashike madaraka, miaka minne iliyopita!

- One thing ninataka kuamini ni kwamba wote hapa tunakubaliana kwamba toka ashike madaraka hakuna hata moja zuri alilolifanya, lakini kama lipo lisemwe hapa! Labda tukimuwahi kabla hajajitokeza tunaweza kupunguza some nonsense kwenye majibu yake na pia tutawasaidia ma-Prosecutors wetu, hasa DPP na Hosea kuanza kutayarisha kesi againts mafisadi!

Respect.

Field Marshall Es!
Hivi kuna mwenye nakala ya hayo mapungufu yaliyotajwa?

Na pia ndo humo Balozi Mwakawago aliwepo?(RIP) Nakumbuka hii issue ilileta sintofahamu nyingi sana!
 
- kwa kuanza ninasema kwamba Rais, ameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote wa ubaradhuli wa Richimond, ambao umeliletea hasara kubwa sana taifa letu, na haya yamethibitishwa na bunge letu kupitia kamati yake maalum ya Mwakyembe.

- Kamati hii ilifanya uchunguzi wa kisheria kwa mujibu wa katiba ya bunge laetu la jamhuri na kutoa mapendekezo kadhaa kuhusu watuhumiwa na adhabu wanazostahili, lakini mpaka leo serikali na hasa Rais, wameshindwa kuwachukulia hatua za kisheria, hasa zilizopendekezwa na bunge.

- Kwa kutowachukulia hatua wahusika, Rais amelidharau bunge la wananchi wa Tanzania na hata sisi wananchi tuliowachagua, na pia aamedharau sheria za jamhuri, hili ni tatizo lake Rais either anawaogopa watuhumiwa wa Richimond, au ni marafiki zake, au hajui wajibu wake kama Rais kwamba ndiye The Law Chief Enforcer wetu.

- Sasa hii ni moja ya sababu muhimu ya baadhi yetu wananchi kuamini kwamba serikali yake yaani Rais Kikwete, imeshindwa uongozi na ikibidi yeye na wenzake waachie ngazi, maana tunao wananchi wengi sana wenye uwezo wa kuongoza ipasavyo, ambao wataziheshimu sheria zetu badala ya kuzichezea kwa kutumia mahela yetu mengi sana kuigharamia kamati ya uchunguzi kama ya Mwakyembe na kuishia kuificha uvunguni ripoti yake.

Respect.

FMEs!

Kamanda kweli uliona mbali,asingeweza kujichukulia hatua mkuu wangu.
 
Jakaya ana hulka moja ambayo wengi mnaompinga hamtakubaliana nayo; toka tukiwa nae chuoni ni mtu ambaye sio mnafiki!! Najua hamuwezi kuamini hili lakini ni kweli ; Jakaya has always been loyal to his friends, wakati wa raha na wakati wa shida. Hilo mimi nitamtetea to the hilt!! Sasa kwa wale wasiomfahamu wanadhani hata kama hiyo kamati ya Mwinyi itarecommend wakina RA na EL wafukuzwe CHAMANI nawaapieni Jakaya will NEVER NEVER support such a move; he is going to marshall his forces within Nec [ spearheaded by the likes of Ngeleja from Shinyanga, Guninita from Dar and Kusila from Dodoma]to vehemently oppose the recommendations!! Hapo hatakuwa yeye aliyekataa mapendekezo bali NEC ya CCM! Huyo ndio Jakaya Mrisho Kikwete!!!
You were right mkuu!
 
Wewe huelewi strategies za vita,

Hapa kuna short term goals na long term goals. Let's say Butiku ni fisadi tu aliyefanya mengi ya ajabu enzi za Nyerere, na sasa anapiga kelele (za kweli) kuhusu uchafu wa JK.

As long as anasema ukweli, hatuwezi kukataa mchango wake katika kumtoa JK.

JK akishatolewa hapo ndipo tutaweza kusema hata Butiku naye ni msanii tu, kwa hiyo hatuwezi kumpa position ya power.

Kama nilivyosema hapo juu, tushaingiliwa na nyoka nyumbani (JK) kitu cha kwanza kufanya ni kumtoa nyoka huyu.Tunajua kina Butiku na CCM ndio walioacha mlango wazi na kumruhusu nyoka huyu kuingia nyumbani, lakini hatuwezi kuanza kutafuta nani kaacha mlango wazi kabla ya kumtoa nyoka.

Tumtoe huyu nyoka JK kwanza, tusafishe na magamba yake yote yenye sumu kutoka ndani ya nyumba (mtandao) tukishamtoa, sasa tutafunga mlango na kuana kujadiliana nani aliacha mlango wazi, na awajibishwe vipi.

Lakini tukianza kujadiliana nani aliacha mlango wazi (kina Butiku na wenzake wa CCM) huyu nyoka atatuuma na ma EPA / Buzwagi/eremeta mengine tutabaki tunashangaa shangaa na bila shaka kujifia kutokana na sumu hii.
Kumbe hii style ya magamba hawa CCM waliiotoa humu JF?Manake hii posti ni ya 2009 kabla hata haya mambo ya magamba hayajaanza!?

Ama Mukama ndo Pundit?Lol!
Viva la JF!
 
Hakuna anaeweza kusema kuwa alichosema Lowassa ni 100 percent kweli
wote ni wanasiasa na wanazungumza kwa timing na mazingira fulani...
JK kutomjibu haina maana 'alikubali' kuwa Richmond ni yake
Ninavyomuelewa JK 'tactic zake za kisiasa' anaweza kukubali au kunyamaza
ili kupisha jambo fulani...

bado mapema mno kusema alichosema Lowassa ndio ukweli asilimia mia moja...
 
Mkuu kama hapo awali alisema hamjui RICHMOND,halafu then ameambiwa na aliyekuwa waziri mkuu wake kuwa yeye ndiye RICHMOND unaionaje hiyo mkuu?

Kweli hastahili kujibu?

Halafu uelewe pia kuwa hii kashfa ni serious ndo maana alijiuzulu mtu...Checki hii mkuu...

http://leaks.hohesc.us/?view=07DARESSALAAM1555
 
Mkuu kama hapo awali alisema hamjui RICHMOND,halafu then ameambiwa aliyekuwa waziri mkuu wake kuwa yeye ndiye RICHMOND unainaje hiyo mkuu?

Kweli hastahili kujibu?

Mkuu una haraka sana naona...
JK haendi hivyo kabisa....
maamuzi ya kujibu mapigo au kuchukua hatua gani kwake ni taratibu mno..
we subiri utaona....

chukua mifano miwili
wa kwanza ni aliyekuwa mkurugenzi wa Air Tanzania .Mattaka....
leo yupo mahakamani....wakati watu walishakata tamaa kama kuna hatua zingechukuliwa

na hata kesi za akina Mramba na wenzie hasa yule aliyekuwa katibu wa wizara ya fedha
zilichukuwa mda mrefu kwenda mahakamani....hiyo ndo JK style..

Lowassa anaweza kuwa 'ameshinda' leo hii kwa public opinion
lakini ngoma bado mbichi mno...
sasa JK probably anapanga the final blow on him...

wao wawili hatuwezi jua yupi anasema ukweli..
usisahau now its personal between them...
 
JK style yake ya uongozi ni ya "kichoganishi". Hataki kuonekana mbaya kwa wananchi na hataki kuonekana adui kwa marafii hata kama ni mafisadi.

Ila nachoamini ni udhaifu wa leadership na management ya JK ndio unampa kiburi EL. Inawezekana hata nusu ya maofisa UWT bado wanaripoti kwa lowasa.

Kuhusu Richmond sina shaka kuwa JK alijua lakini msuka mipango, muwezeshaji na mratibu mkuuani EL. Ni udhaifu wa JK ndio unafanya EL azidi kupaa.
 
Wakuu Jmushi na The Boss

Issue ya Lowasa na Richmond iko wazi kabisa. JK alikuwa final sayer wa hili swala japo mtendaji alikuwa Lowasa. na Kamati ya Bunge ililaumu watu wa chini ya Lowasa! na sio Lowasa directly!

siasa za CCM zisituweke kwenye position ambayo hatutaweza kulifikiria hili kiundani inapotamkwa Richmond lazima watamkwe watu wawili JK na Lowasa, imekuwa kinyume anasemwa EL tu, vyombo vya habari vinajua ila vinaogopa! na ndiyo maana kila vikikutana na EL vina mdodosa kuhusu Richmond hili aseme jambo!

JK knew and directed everything about Richmond...Lowasa did everything about Richmond!
 
JK style yake ya uongozi ni ya "kichoganishi". Hataki kuonekana mbaya kwa wananchi na hataki kuonekana adui kwa marafii hata kama ni mafisadi.

Ila nachoamini ni udhaifu wa leadership na management ya JK ndio unampa kiburi EL. Inawezekana hata nusu ya maofisa UWT bado wanaripoti kwa lowasa.

Kuhusu Richmond sina shaka kuwa JK alijua lakini msuka mipango, muwezeshaji na mratibu mkuuani EL. Ni udhaifu wa JK ndio unafanya EL azidi kupaa.

wewe umeongea ukweli
JK hawezi kuonesha 'sura yake' halisi
watu hatujui anapinga nini na anaunga mkono nini
hana a spine....
kwa hiyo Lowassa sasa 'anambambikia' kesi ya Richmond mchana kweupe
na yeye 'bado anagwaya gwaya'...
 
wewe!! supported!
 
Mtazamaji,soma hii linki hapo chini utajuwa ninachomaanisha,kwasababu si amemsikiliza Mkapa kwenye uamuzi wa kuuwa issue ya magamba?

Sasa cheki ndo utajuwa unafiki wa watu,ina maana rushwa inapigwa vita nje ya chama na ndani ya chama rushwa is a none issue,yani viongozi wakuu wa chama na serikali ndo vinara wa rushwa wanayodai wanaipiga vita!Only in Tz!

Africa Review*- WikiLeaks spotlights Tanzania on corruption
 
wewe umeongea ukweli
JK hawezi kuonesha 'sura yake' halisi
watu hatujui anapinga nini na anaunga mkono nini
hana a spine....
kwa hiyo Lowassa sasa 'anambambikia' kesi ya Richmond mchana kweupe
na yeye 'bado anagwaya gwaya'...
Mkuu,hadi wasauzi wanamchora tu...
President Jakaya Kikwete's proves indecisiveness in tackling graft. He was ridiculed in The East African recently relating his behavior to that of someone ‘hobbled with a reputation of a lazy, foreign-trip-loving President, who is soft on corruption.'

Donors are unhappy the way the government is handling corruption;
thus they have either slashed or withheld their development aid- which is injected in the form of General Budget Support .

While the opposition is up in arms calling the government to institute criminal charges against the culprits, corruption is costing Tanzania millions of dollars.

"Mr. Aziz's resignation showed political maturity. He has shown the way that should be followed by other party members of questionable integrity," says Zitto Kabwe, from Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Announcing his resignation in a remote township of Igunga -where he had been a legislator, Mr. Aziz blamed fellow leaders for entertaining what he termed as ‘gutter politics'Analysts say Mr. Aziz's move is likely to pile up pressure on Mr. Lowassa and Mr. Chenge who have yet to make up their mind about whether they are ready to give up as demanded by the party.

Mr. Aziz had been a backbencher in politics despite having big influence considering the strides he made during campaigns for CCM presidential candidate in 2005.

Mr. Aziz, has insisted that not all the allegations against him were true but admitted that his name had been associated with those undermining the performance of his party.

"My party's performance went down to 61 per cent last year from 80 per cent in 2005. This did not impress me and I wish my decision improves its popularity," he said.He warned that CCM's future would prove difficult if infighting does not stop.Kizito Makoye is journalist writing from Dar es Salaam

Kwa maana huyu hapo chini naye ameonewa?Ama ni uarabu wake?Lol!

Former-Tanzanias-legislator-Rostam-Aziz-in-one-of-his-campaign-meetings.-e1311714285593.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
...Mkuu, huyu jamaa (hapa namaanisha Baba Riz1), ana uwezo mdogo, sio tu wa kufikiri hata kuthubutu (hapa namaanisha kwenye mambo ya msingi tu, ya hovyo anaweza), alishapoteza "legitmacy" kutuongoza kitambo tu huko nyuma, ila hili la Richmond linamwanika, linamsasambua na hatimaye linamweka uchi, na ni kutokana na staili yake ya kuongoza kwa staili ya bendera, kwamba upepo umevuma vipi, pasipokuwa na upepo ana stuck, hebu cheki nukuu chache za EL kuhusu Richmond "...mwenyekiti, unakumbuka ukiwa nje ya nchi nilikupigia simu kukushauri kuwa tuvunje mkataba wa Richmond wewe ukasema ngoja tusikie ushauri wa kamati ya makatibu wakuu ambao ndo waliosababisha mkataba usivunjwe?" "....mwenyekiti, unafahamu hakuna jambo nililolifanya ambalo sijakushirikisha, kila kitu unajua"mwisho wa nukuu za mh. ...ni ngumu kwangu kuamini kwamba EL anamfanyia sanaa japo yote yanawezekana, kwa maoni yangu huyu ndio GAMBA namba moja.
 
Hakuna anaeweza kusema kuwa alichosema Lowassa ni 100 percent kweli
wote ni wanasiasa na wanazungumza kwa timing na mazingira fulani...
JK kutomjibu haina maana 'alikubali' kuwa Richmond ni yake
Ninavyomuelewa JK 'tactic zake za kisiasa' anaweza kukubali au kunyamaza
ili kupisha jambo fulani...

bado mapema mno kusema alichosema Lowassa ndio ukweli asilimia mia moja...

Kwa nnavyoifahamu kurugenzi ya habari ya ikulu siku hizi lazima watatoa press release kuhusu hili, just wait and see!!!!!
 
Sioni ni kwavipi JK bado ana legitmacy ya kuisimamia ofisi ya urais.

Sioni kwa kweli...

Amekimbiza issue nyeti zinazohusu taifa zima huko kwenye vikao vyao vya NEC,lakini huko nako pia hana madaraka ya kutoa maamuzi,hana nguvu.

Sasa huyu si aliapa kulinda taifa na ameshindwa kwanini asiachie ngazi? Kwa maana halisi ya neno Legitimacy to lead imepotea,hakuna tena!

Pia kama ameshindwa kaswababu yeye ndiye fisadi nambari wani,then hiyo ndiyo even a better reason to leave office,imeshamshinda hilo liko wazi!
 
Back
Top Bottom