Tetesi: Harusi ya Ruge na Zamaradi iko tayari, imepewa jina la Harusi ya Watu

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,661
21,635
Mkurugenzi na mtangazaji kutoka redio ya watu wako tayari kabisa kufunga harusi siku yoyote kuanzia wiki ijayo. Harusi hiyo iliyopewa jina la harusi ya watu inatarajiwa kuwa kubwa Tanzania kuliko harusi yoyote ile tokea tupate uhuru.

Mmoja wa wanakamati wa harusi hiyo amedai harusi hiyo itafanyika katika sehemu nne tofauti kwa wakati mmoja,alizitaja sehemu hizo kuwa ni Bukoba, Tanga, Mjengoni Mikocheni na Ukumbini.

Wageni kutoka sehemu tatu wataunganishwa moja kwa moja na wale wa ukumbini kupitia sophisticated technology inayoitwa virtual reality (VR). Mwanakamati huyo alidai wageni hao watavaa VR gears na hivyo kuungana moja kwa moja na wageni wengine kutoka Dar na hivyo kuweza kufanya vitu kadhaa kama vile wako ukumbini.Baadhi ya vitu hivyo ni kama kutoa zawadi ,kushikana mikono na maharusi, kucheza mziki na vitu vingine kadhaa.

Ukubwa wa harusi hiyo unafananishwa na harusi mbili zilizoahirishwa dakika za mwisho, moja ikiwa ya mnyange Sepetu na Simba au ile ya Baharia aliyowachangisha waarabu wanaomiliki sheli na super moguls kadhaa kabla ya kuamua kuendelea kuwa single maana umri ulikuwa bado unaruhusu.

Tunawatakia kila la heri katika maisha yao ya ndoa.
 
Ruge mutahaba.. ni bingwa wa biashara ya burudani tanzania..
digrii yake ya masoko aliyoipata san diego state university usa.. mwanzoni mwa miaka ya 90 ameitendea haki sana.. maana toka alivyotua bongo baada ya kumaliza chuo ni mafanikio tu

hajawai kuomba ajira kwa mtu toka ametoka chuo zaidi ya kuungana na mwenzake kusaga na kujiajiri kwa mafanikio makubwa sana...
Ruge mutahaba tatizo lake ni moja tu mapenzi na kazi..
ukiacha hilo pungufu lake jamaa ni kichwa sana kwenye kuongoza kampuni ya burudani...

angalia clouds ya miaka ya 90 clouds disco..
angalia mfumo wake wa uongozi utamkubali huyu mhaya noma
 
Hongera zao bhana, at the end of the day ni wao waili tu kitandani. I wish hizo VR zingetuonyesha hadi kitandani aaaghh ingekuwa harusi kubwa ya karne at least watuonyeshe the first official night hahahahaa
 
Dah! Kuna mtu ameniudhi hapa tulikuwa tumekaa kimya kama mabubu hapa huku kila mtu akitumia simu yake, sasa nilipopitia huu uzi nimejikuta nacheka kwa sauti hasa hapo kwenye harusi zilizoahirishwa dakika za majeruhi, na hatimaye tumejikuta tumepatana na tunaongea. Ahsante sana MSAGA SUMU.
 
Dah! Kuna mtu ameniudhi hapa tulikuwa tumekaa kimya kama mabubu hapa huku kila mtu akitumia simu yake, sasa nilipopitia huu uzi nimejikuta nacheka kwa sauti hasa hapo kwenye harusi zilizoahirishwa dakika za majeruhi, na hatimaye tumejikuta tumepatana na tunaongea. Ahsante sana MSAGA SUMU.
Hahahah...Jamaa nahisi atakuwa na shahada ya juu ya habari na mawasiliano
 
Back
Top Bottom