mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,966
Hiki kisa ni cha kweli na cha kusikitisha.
Ni asubuhi njema ,mipango ya harusi imekamilika na siku imewadia.Hawa(Mke na Mume) wanajiandaa kuelekea kanisani,kwa lengo la kufunga ndoa(au kubariki kama ilivyozoeleka kwani walikwishakaa kwa muda wa miaka miwili pamoja).
Ndoa imefungwa,tarumbeta na shamrashamra za kila mahali zinaoonekana,msafara wa magari na watu wa kila aina unaipamba harusi ile.Hatimaye muda wa kuingia ukumbini kwa maharusi unawadia,na kazi ya msema chochote (MC) inaanza rasmi.
Kama kawaida wageni kutoka ukeni na kuumeni wanakaribishwa,tukIo la kwanza ni kufungua champaigne kutakiana kheri na baraka.Kipindi chote hiki kuanzia asubuhi mpaka muda huo nyuso za maharusi zinaonesha tabasamu ya khali ya juu.
Ukawadia wakati wa kukata keki,hapa ndipo,sinema ya kusikitisha ilipoanza,kama mnavyojua staili ya ukataji wa keki inategemea na maandalizi,inasemekana bwana harusi aliomba kila mtu akate keki yake ila kwa wakati mmoja.MC katika kukoleza na kuchangamsha shughuli,akawaambia maharusi kunyanyua juu visu vyao na kuanza kuwahesabia: moja..........mbili..........tatu,ghafla!! sura ya bwana harusi inabadilika,MC anapohesabu kwa mara ya tatu,badala ya kukata keki,kisu cha bwana harusi kinatua kwenye tumbo la bibi harusi,utumbo wote nje.Historia ya maisha ya watu hawa inaishia hapa,historia imeandikwa hivyo.
Bwana harusi anaanza kulia na kulalama:"huyu mwanamke kazidi kwa usaliti,nimemkomesha..............!
RIP Bi harusi!!
My take: Visasi au ukimya ni bomu baya sana kwa wapendao>Vunja Ukimya, Zungumza na mwenzio.