Harusi ni ya Mwanamke, Ndoa ni ya Mwanaume

Harusi ni ya Mwanamke, Ndoa ni ya Mwanaume

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Katika dunia ya sasa, harusi imegeuka kuwa tamasha la kuonyesha mali, hadhi na umaarufu. Watu wengi – hasa wanaume – wanajikuta wakilazimika kutumia mamilioni ili kufanikisha harusi ya kifahari, ilhali maisha ya ndoa yanayofuata yanakuwa magumu, yenye mivutano na yasiyo na furaha.
images - 2025-06-28T210811.210.jpeg

Ni wakati sasa kwa mwanaume kuelewa kuwa harusi ni ya mwanamke, lakini ndoa ni ya mwanaume.

Mwanaume wa kweli hatakiwi kujishughulisha kupita kiasi na maandalizi ya harusi ya kifahari, bali ajitahidi kuhakikisha maisha ya ndoa yanakuwa yenye msingi thabiti. Harusi ni tukio la siku moja tu, lakini ndoa ni safari ya maisha.
images - 2025-06-28T210801.874.jpeg

Wanandoa wengi wameingia kwenye mikopo mikubwa, kuuza mali zao au hata kuingia kwenye matatizo ya kifamilia kwa sababu ya kutaka kuonyesha harusi ya kifalme, lakini baadaye wakajikuta kwenye ndoa yenye majuto.
images - 2025-06-28T210752.495.jpeg

Kama unampenda mwanamke, jambo la msingi zaidi ni kwenda kumtambulisha kwa wazazi wake kwa heshima na unyenyekevu. Hiyo ni hatua ya uanaume. Ukisha tambulika rasmi, mnaweza kupanga harusi ya kawaida, yenye gharama nafuu lakini yenye heshima.
images - 2025-06-28T210743.204.jpeg

Cha muhimu ni kuanza maisha ya ndoa yakiwa na msingi wa mapenzi, heshima, mawasiliano na uwazi – siyo msingi wa deni na maumivu. Kuna wanawake wana mipango mingi sana kuhusu harusi kuliko ndoa, anafahamu vitu ambavyo anatakiwa kuvifanya kwenye harusi ila sio kwenye ndoa.
images - 2025-06-28T210722.776.jpeg

Wanaume tunapaswa kuelewa kuwa furaha ya ndoa haipo kwenye ukumbi mkubwa au gari la kifahari siku ya harusi, suti kali ya laki tano, bali ipo kwenye tabasamu la mkeo anapokuandalia chakula cha jioni baada ya siku ndefu ya kazi, ipo kwenye watoto wenu mnapowatazama wakikua kwa maadili mema, na ipo kwenye utulivu wa akili na amani ya moyo inaopatikana nyumbani kwako.
images - 2025-06-28T210650.534.jpeg

Uanaume si kuandaa harusi kubwa – uanaume ni kuongoza familia yenye misingi bora. Si vibaya kufanya harusi nzuri kama una uwezo, lakini si busara kuifanya kuwa lengo kuu ili upate kuonesha dunia kuwa una pesa ama uwezi.
images - 2025-06-28T210752.495.jpeg

Kuna msemo kuwa ni bora harusi ya kawaida inayopelekea ndoa bora, kuliko harusi ya kifahari inayopelekea ndoa ya mateso.
images - 2025-06-28T210811.210.jpeg

Kama mwanaume, jenga ndoa bora, si harusi kubwa. Fikiria mbele, chagua hekima badala ya maigizo. Ndoa ni safari ya maisha, na wewe ndiye dereva wake. Hakikisha unaanza kwa msingi sahihi.
 
Kama mwanaume, jenga ndoa bora, si harusi kubwa. Fikiria mbele, chagua hekima badala ya maigizo. Ndoa ni safari ya maisha, na wewe ndiye dereva wake. Hakikisha unaanza kwa msingi sahihi.
Nakazia ✍️
Umenena vyema
 
Back
Top Bottom