Harufu ya mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harufu ya mabadiliko

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Nov 2, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,901
  Likes Received: 12,033
  Trophy Points: 280
  • Slaa ang'ara, wabunge CHADEMA wapeta


  MATOKEO ya awali ya kura za urais, ubunge na udiwani yaliyoanza kutolewa jana kwenye vituo mbalimbali nchini, yameonyesha kuwa nyota ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, imeendelea kung’ara huku wagombea ubunge wa chama hicho nao wakionekana kufanya vizuri.
  Habari kutoka Jimbo la Iringa Mjini, zinasema matokeo ya urais katika kata saba, mgombea wa urais wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alikuwa akiongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete.

  Vituo hivyo ni stendi, Dk. Slaa (146), Kikwete (114), Ndiuka Dk. Slaa (133), Kikwete (272), Soko Kuu 2, Dk. Slaa (114), Kikwete (84), Zimamoto 1, Dk. Slaa (93), Kikwete (84), Zimamoto 2, Dk. Slaa (84), Kikwete (108), Hazina Dk. Slaa (138), Kikwete (97), IDYC Dk. Slaa (75) na Kikwete (72).

  Katika Jimbo la Mbeya Mjini, matokeo ya ubunge vituo vya Block T- A, CHADEMA (140), CCM (33), kituo B, CHADEMA (115) na CCM (15).
  Mbeya Mjini, katika Kata ya Mwakibete, Dk. Slaa (3,564), Kikwete (950), Kalobe Sekondari 1 Dk. Slaa (109), Kikwete (97), Kalobe Sekondari 2 Dk. Slaa (107), Kikwete (76), Kalobe Sekondari 5 Dk. Slaa (93) na Kikwete (85).

  Geita kura za urais Kikwete (376), Dk. Slaa (341), kwa upande wa ubunge CCM (396), CHADEMA (322) na CUF (10) na kwa udiwani CCM (315), CHADEMA (474) na CUF (0).

  Jimbo la Kyela matokeo ya urais katika kituo cha Nsesi, Kikwete 150, Slaa 119, kituo cha Katumba shuleni Kikwete 150, Slaa 120, Kilasilo, Slaa 36, Kikwete 205, Community Centre Slaa 125, Kikwete 56, Itungi Slaa 76, Kikwete 54. Katika kituo cha Bunge, jijini Dar es Salaam, Slaa 225, Kikwete 189.Arusha Mjini, katika Kata ya Kaloleni A1, Dk. Slaa amepata kura (112), Kikwete (59), Kaloleni A2, Dk. Slaa (119), Kikwete (76), Profesa Lipumba (2), Kaloleni A3, Dk. Slaa (104), Kikwete (61), Lipumba (1), Kaloleni A4, Dk. Slaa (109) na Kikwete (165).

  Kituo B1, Dk. Slaa (118), Kikwete (67), Profesa Lipumba (0), kituo B2, Dk. Slaa (102), Kikwete 64, B3, Slaa 92, Kikwete 50, B4, Slaa 87, Kikwete (67) na Lipumba (3).
  Jimbo la Segerea, Kata ya Kipawa, kituo Minazi mirefu A1 urais, Kikwete (79), Dk. Slaa (75), Profesa Lipumba (7), kituo A6, Dk. Slaa (69), Kikwete (62), kituo A2, Dk. Slaa (102), Kikwete (52), Profesa Lipumba (1), kituo B3, Kikwete (64), Dk. Slaa (78) na Profesa Lipumba (3).

  Katika matokeo ya ubunge wa kata hiyo, mgombea wa CHADEMA, Godbels Lema alionekana akiongoza ambapo katika Kata ya Kaloleni A1, (113), dhidi ya mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian (54), Kaloleni A2, Lema (120), Burian (71), Kaloleni A3, Lema (109), Batilda (62), Kaloleni A4, Lema (111) na Batilda (63).

  Jimbo la Ukerewe katika vituo vitatu, Mtoni, Nansio, Bwisya, mgombea wa CHADEMA, Salvatory Namuyaga wa CHADEMA alikuwa akiongoza akifuatiwa na mgombea wa CCM, Gertrude Mongela.

  Katika Jimbo la Musoma Mjini, CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa madiwani katika kata nane, CCM ikipata kata tatu na CUF ikipata madiwani wawili.
  Taarifa za awali zimedokeza kuwa Vincent Nyerere, alikuwa akiongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya mgombea wa CCM, Vedasto Manyinyi.

  Jimbo la Moshi Mjini, CHADEMA ilikuwa ikiongoza kwa kiti cha urais na ubunge huku upande wa madiwani ilikuwa ikiongoza kwa kupata viti 15 kati ya 21.
  Hali hiyo, ilijitokeza katika majimbo ya Kigoma Mjini na Kigoma Kaskazini, ambako upinzani mkubwa ulikuwa kati ya vyama vya CCM na CHADEMA.

  Katika Jimbo la Kigoma Mjini, Peter Serukamba wa CCM anachuana na Ally Mleh wa CHADEMA, huku katika Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe wa CHADEMA anachuana na Robinson Lembo wa CCM.

  Jimbo la Mbeya Mjini, mpaka tunakwenda mitamboni mgombea wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi, ameonekana kuongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Benson Mpesya. Kituo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (DARUSO), urais Dk. Slaa (454), Kikwete (71), ubunge, John Mnyika wa CHADEMA (473) na Hawa Ng’umbi wa CCM (45).

  Maswa, Magharibi, ubunge

  Mgombea wa CHADEMA, John Shibuda, alikuwa akiongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Peter Kisena, ambapo katika kituo cha Bukigi, Kata ya Malampaka Shibuda 113, Kisena 65, Sokoni Shibuda 68, Kisena 46, Sokoni B Shibuda, 61, Kisena 56, Mahakama A, Shibuda 66, Kisena 47, Mahakamani B, Shibuda 65, Kisena 50.

  Shule ya Msingi Malampaka, Shibuda 54, Kisena 55, Chekechea A Shibuda 79 Kisena 5, Chekechea B, Shibuda 74, Kisena 53, Oil Mill, Shibuda 56, Kisena 36.

  Jimbo la Nyamagana, inadaiwa mgombea wa ubunge Ezekiel Wenje, ameonekana kuongoza dhidi ya mgombea wa CCM, Lawrence Masha, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Katika jimbo hilo CHADEMA inaongoza kwa kupata madiwani katika kata 12 kati ya 14.
  Katika Jimbo la Iringa Mjini, hadi tunakwenda mitamboni mgombea wa CHADEMA, Peter Msigwa, alikuwa akiongoza katika vituo vingi dhidi ya mgombea wa CCM, Monica Mbega.
   
 2. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,726
  Likes Received: 3,144
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaleta matumaini lakini mbona kila mmoja ameshakataa tamaa? Kila kona wanadai Kikwete kashinda sasa which is which? Kichwa kinauma macho hayaoni tena kwa kuikodolea macho laptop nikijipa matumaini labda mambo yatabadilika. CCM CCM mnatufanya tunalia halahala tusipokezane kulia hapo baadae.
   
 3. V

  Vitus mkumbee Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi cna tena matumaini ila tuskate tamaa maana wakijua watazidi
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwanini mnakata tamaa?...........msikubali kudanganywa na mbinu ya NEC kuanza kutangaza zile sehemu ambazo Jk ana nguvu............ngoma bado sana hii......tukikata tamaa ndio mnawapa NEC nguvu ya KUCHAKACHUA votes
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,210
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  You all right Ogah;

  inachofanya NEC ni kutangaza mikoa ambayo JK ana wafuasi wengi ili kukatisha tamaa upinzani lkn ukweli wenyewe inabidi sisi wapinzani no matter tujimwage barabarani kushangilia ushindi wetu!

  Kumbukeni kuwa kabla ya uchaguzi huu CHADEMA ilikuwa na wabunge 5 tu wa kuchaguliwa lkn hadi sasa imezoea wapya karibu 20,NCCR ilikuwa haina Mbunge lkn sasa imekwisha pata wabunge zaidi ya 3,CUF imeongeza toka wabunge 18 waliokuwa nao hadi kufikia 25 hadi sasa na UDP likely imetetea Shinyanga!

  Jamani tufurahie uchaguzi bila woga wala aibu,na hata CCM wanajua kuwa sasa watz sio wa kuchezewa tena na wanataka kusikilizwa matakwa yao;Je ilikuingia akilini kuwa ipo siku CCM itapoteza jimbo Lindi na Mtwara?Ilikuwa inaingia akilini kabla ya uchaguzi huu kuwa CCM itapoteza karibu majimbo yote Kigoma?Ikapoteza in land slide in Shinyanga,Mwanza na Mbeya?wapinzani tumeweza kuchukua jimbo atleast kila Mkoa safari hii tofauti na chaguzi zilizopita!

  Tusibabaike na NEC;Matokeo ya U-Rais ya mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Mwanza,Dar,Mara,Manyara,Arusha na kwingineko yakianza kumiminika Dr Slaa atakuwa na nafasi kubwa zaidi!

  NEC bado haijagusa sehemu ambazo Slaa ana wafuasi wengi
   
 6. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  :smile: Niliwaza hicho kitu jana wakati nasikiliza matokeooo.... Wanatangaza majimbo ambayo Kikwete amepata yale mengine wameweka kapuni wanaangalia namna ya kuchakachua. Ndio maanaaaaa... hata jana wakajidai kutangaza saa 10 majimbo 4 badala ya kutangaza saa 2 usikuuuu.....
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Msikate tamaa,vinginevyo mpango wa kuwachakachua saikolojia umefanya kazi.Walichokifanya Tume ni kutangaza kwa mfululizo maeneo ambayo Kikwete ameshinda kwa kishindo ili kuathiri saikolojia ya wapiga kura.Kama tukishaathirika kiasikolojia na kusema kikwete kashinda,hata wakichakachua maeneo yaliyobaki tutaamini tu.Ni jukumu la mawakala husika kuhakikisha kuwa matokeo ya majimbo yaliyobaki yanatangazwa kwa ufasaha.Yapo majimbo mengi ambayo matokeo yamekamilika muda mrefu lakini bado kutanganzwa,haya ni yale ambayo kikwete kashindwa vibaya.
   
 8. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu ina maana kura zote za uraisi zilihesabiwa na mawakala na record zipo vituoni?
   
 9. doup

  doup JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  ndio maana yake, mahesabu yote huwa kituoni
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mungu yuko upande wetu, siku zote haki ya mtu haipotei
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,158
  Likes Received: 417,585
  Trophy Points: 280
  tatizo ni kuwa wasimamizi wa majimbo hawapeleki matokeo ya kweli juu ya ushindi wa JK. Mfano leo asubuhi ITV imebaini Morogoro Mjini uchakachuaji wa fomu ya uraisi na sasa imegoma kupita kwenye mashine za fax na fomu yenyewe imethibithishwa kuwa ni ya kughushi na kuashiria ya kuwa hata matokeo yamebadilishwa ili kumbeba JK......

  Sasa lengo ni nini? Chadema wanatakiwa walinganishe kwa ukaribu sana matokeo waliyonayo na yale yanayotangazwa na NEC ili kujihakikishia ya kuwa hayajachakachuliwa.......
   
 12. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,918
  Likes Received: 1,024
  Trophy Points: 280
  kile chama cha michakachuaji (ccm) kiko hoi bin taaban. mabadiliko yanakuja hatua kwa hatua lakini kwa kasi ya ajabu.
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu uko sahihi NEC wanataka kutuchakachua kisaikolojia, CHADEMA iko makinis ana, wanawasubiri watangaze tu ili kulinganisha na yale waliyo nayo tayarai, msihofu ushindi ni wetu!!!

  Wanachokifanya hapa ni kuwafanya watu waanza kuamini CCM imeshinda, ngoma mbichi sana!!!
   
Loading...