Pole binti, una umri gani? haya mambo yapo, nilikuwa na binti fulani mwaka mmoja uliopita huyu binti alinieleza tatizo lake, yeye akimuona tu mwanaume tayali analegea na kulowa kabisa, japo si kila mwanaume lakini ilimtokea mara kwa mara, nadhani ilikuwa kwa wanaume wenye mvuto wa kimapenzi. Hii huwa ni kutokana na maumbile ya mtu mwenyewe, hata hivyo tambua huo ni udhaifu na unapaswa kupambana nao ili usije kuwa rahisi sana.
Zaidi ni kuamua kuipotezea hiyo harufu pindi unapoihisi na kujilazimisha kuondoa mawazo, taratibu utaweza kuondokana na hiyo hali, lakini pia kupata ushauri kwa wataalamu ni muhimu zaidi pamoja na kumuomba Mungu.