Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,003
- 33,631
Mkutano wa ndani wa TANU nyumbani kwa Ali Msham Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa miaka ya mwanzoni 1950
Fatilia ukurusa huu In Shaa Allah nitaweka picha zaidi kila nipatapo nafasi.
Tumia picha upendavyo hazina hati miliki.
Picha hii ilipigwa 1942 wakati Abdul Sykes alipokuja Dar es Salaam kutoka mafunzo ya kijeshi Lower Kabete, Kenya kuaga kabla ya kwenda vitani Burma Vita Vya Pili Vya Dunia.
Kulia Lawi Nangwanda Sijaona, Abdulwahid Kleist Sykes, Julius Kambarage Nyerere, Waziri Dossa Aziz Ukumbi wa Arnautoglo dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956.
Kulia ni Ali Msham, baba yake Ali Msham Mzee Msham na aliyekaa kwenye kiti ni Julius Nyerere siku alipoalikwa kwenye tawi la TANU la Ali Msham kupokea fanicha alizotengenezewa na Ali Msham kwa ajili ya ofisi yake New Street.