Justine Marack
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 564
- 1,548
Katika Maisha lazima tujiandae na Mabadiliko tusiyo yatarajia. Hivyo hata katika Muziki wa Kibongo wasnii wanapaswa kuishi kwa maandalizi. Hata Diamond amabaye ni nguli wa hizi kazi naye lazima aishi kwa kujiandaa. Nitaandika kuhusu anguko la Diamondo siku nyingine.
Leo napenda kuzungumzia kiti ambacho kwa sasa kiangombewa kwa vita kali. Kiti kinacho gombewa ni kile cha upinzania mbacho Alikiba amekikalia kwa takribani miaka kumi na sasa ameinuliwa toka kitini hapo na sasa anasubiriwa apige hatua kurudi nguma au pembeni ili aache mwingine akalie. Je, nani kukalia kiti hicho ? Ni Marioo?ni Harmonize? au Alikiba atafanikiwa kung'ang'ana kama mzee wetu Polofesa kule kwa Ngangari?
Baada ya Konde boy kujiondoa WCB ilitarajiwa aibuke kuwa mpinzania mkubwa wa Mzee Baba lao lakini hali inaoneka kuwa tofauti na matarajio hasa baada ya Alikiba naye kufanya mabadiliko makubwa katika menejimenti yake mbayo infanya tunaona vitu ambavyo hatukuvizowea kwa Kiba. Sasa Kiba naye Anafanya festival, sasa kiba anamdis mondi kila interview sasa Kiba anapost na kuandika Mambo mbalimbali ya kujimwambafai tofauti na zamani. Meneja wa Kiba naye sasa anamjibu Tale ngadukwangadu . Hii yote ni Kiba anajaribu kubakisha mashabiki wake ambao waliona Harmonize ndio kimbilio ili kumkomoa Mondi na wakati wakiwa njiani kuelekea kwa Mmakonde huku nyuma wanaona mfalme wao amezinduka, je watamuamini na kurudi au wanaendelea na safari.
Wakati hayo yakiendelea kuna Marioo naye kaibuka kwa kasi ya kisulisuli. Huyu naye anaimba syle ya Mondi. Ndio, kila mtu anaangalia upenyo na si mwingine ni kupita alipo pita Mondi kama alivyo fanya Harmonize na kufanikiwa kutoboa.
Sasa Marioo anapita muemule na sasa naye amejimegea Mashabiki hasa toka katika kundi tengefu la Kiba. Hkweli ni Kwamba Mashabiki wa Diamond ni Blood fans ndio maana unaona vimbunga vyote kuanzia kwa Belle9,Yamoto Band,Aslay,Mavoko,Darasaa mpaka sasa kwa Harmo na zilipendwa wetu Kiba bado Mondi yuko imara. Uimara wa Chibu ni hii miaka kumi ambayo kila kijana amebarehe akicheza Sangoro sangoro mpaka sasa wana Kanyaga na Yope kisha wanajiona Baba lao.
Hizi ndio mbegu anazo panda mondi kwenye Mioyo ya hawa shabiki zake bila kusahau namna anavyo wapinduapindua katika dancefloor ukitoa Mbagala unabandika Kanyaga ukipiga Yope na kupoozea kwa Inama unakuja Kutuliza kwa Iyena na Nasema nawe hapo unakua umefika mpaka pwani na ukichoka untuliza kwa Baila.
Sasa hapo tunaona Mondi hana wa kumtikisa tena baada ya Darassa kushindwa. Nitaeleza makala ijayo kwanini namtaja Darassa. Labda kwa kudokeza tu kama ulikua hujui Wimbo ya Diomond na Mavoko KOKORO ni moja kati ya Nyimbo kubwa sana WCB na ingetikisa sana lakini Kimbunga cha MUZIKI ya Darassa kilifanya mpaka leo wimbo huu umekuwa wa kawaida yaani ile kisulisuli cha Darassa kinapoa na Kokoro imesahaulika ingawa mpaka sasa Mavoko huu ndio wimbo wake wa kujivunia jukwaani.
Turudi kwenye Mada yetu, je Nani atakalia kiti. Ni wazi Harmonize hakutarajia kama Kiba atabadilika na kuzinduka huku Marioo akiangalia step za wababe hawa ili awapige push kwa pamoja akae na kupambana na Mondi.
Tupe maoni yako.