Ndaro: Marioo umetusahau tunaoumizwa na mapenzi

Ndaro: Marioo umetusahau tunaoumizwa na mapenzi

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
443
Reaction score
1,101
Mchekeshaji, muigizaji, na content creator, Ndaro , kupitia Instagram yake ametoa ya moyoni na kueleza masikitiko yake kwa njia ya utani kuhusu mabadiliko ya kimtindo ya msanii wa Bongo Fleva, Marioo.

Ndaro amelalamika kuwa Marioo ameacha kuachia nyimbo za simanzi za mapenzi ambazo zilikuwa zikiwagusa na kuwaliza mashabiki wengi waliopo au waliowahi kuwa kwenye majeraha ya mahusiano.

Alieleza kuwa zamani nyimbo za Marioo zikianza tu na neno la utambulisho la "Kapipoooo...", ilikuwa ni uhakika tosha kwamba msanii huyo amewaimbia waliopo kwenye changamoto za kimapenzi na kuliza wengi waliopitia maumivu hayo.

Hata hivyo, Ndaro amesisitiza kuwa hali imebadilika tangu Marioo aanze kufungua kazi zake mpya na sauti au viitikio vya "Aloooooooo" na "Kanibaliiiiiiii".

Ndaro anaamini mtindo huu mpya umewasahau kabisa wale waliokuwa wakitegemea kazi za msanii huyo kupata faraja ya maumivu yao ya moyo, na amehitimisha ujumbe wake kwa kuandika kwa utani neno "Free Marioo" akitaka msanii huyo arejee kwenye mtindo wake wa zamani.
1789642720054.png

1789642691162.png
 
Back
Top Bottom