PreGE2025 Harmonize asema atagombea Ubunge Jimbo la Tandahimba 2025

PreGE2025 Harmonize asema atagombea Ubunge Jimbo la Tandahimba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Akiongea na Ayo TV kwa njia ya simu, Harmonize ambaye alizaliwa Kijiji cha Chitoholi Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara, amesema alichokiandika saa kadhaa zilizopita kuhusu dhamira ya kugombea Ubungo sio kitu cha utani bali anamaanisha ambapo muda ukifika atakwenda kuchukua fomu kupitia CCM ili aombe ridhaa ya Chama hicho kimpitishe kugombea.
Sugu na yule wa Mikumi waliwaambiaje?
Check and balance
 
Kwa hiyo zile bomboclaaaaaaaat zinaenda kupigwa kwa wingi mjengoni bila kusahau bangi za kutosha kama kawaida yake
 
Mwimbaji Staa wa Bongofleva Rajabu Adbul Kahali maarufu Harmonize ametangaza rasmi dhamira yake ya kwenda kugombea Ubunge wa Jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara ambako ndio alikozaliwa. Kabla ya kuongea na na kuthibitisha dhamira yake hiyo, Harmonize aliandika maneno yafuatayo kwenye ukurasa wake wa Instagram “Tandahimba Member of Parliament 2025 Inshallah October ✅ CCM oyee ”

Itakumbukwa October 15,2019, Harmonize ambaye kwa sasa ana-hit na wimbo mpya wa ‘best couple’, alitajwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambaye aliweka wazi kuwa anatamani Mwimbaji huyu akagombee Ubunge wa Tandahimba ingawa kwa wakati huo Harmonize alionekana kutokuwa tayari kugombea kiti hicho.

Hayati JPM alinukiwa akisema ““Lakini nampongeza sana Harmonize sijui anatoka Jimbo gani?, Tandahimba?, Mbunge wa kule ni nani?, (Katani), aah ningetamani sana Harmonize aende akagombee kule awe Mbunge wa Tandahimba”

Akiongea na kwa njia ya simu, Harmonize ambaye alizaliwa Kijiji cha Chitoholi Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara, amesema alichokiandika saa kadhaa zilizopita kuhusu dhamira ya kugombea Ubungo sio kitu cha utani bali anamaanisha ambapo muda ukifika atakwenda kuchukua fomu kupitia CCM ili aombe ridhaa ya Chama hicho kimpitishe kugombea.
View attachment 3378524
KKK tuui
 
Ukimuona Harmonize na kipaji alichonacho na lebel aliyonayo lakini bado kaona Siasa ina hela, tujiulize sana kuna nini huko kama taifa tunaelekea wapi ? Mshahara wa mbunge haukupaswa kuzidi hela ya mwalimu ila tatizo tumepata viongozi wachumia tumbo na sasa hata hawajui huko bungeni wafanye nini zaidi ya kumshukuru mama Samia na kupiga makofi jioni wakasign posho na pensheni ambayo ni jasho la umma maana hawalipi kodi na hawachangii hata 10. Nakulilia Tanzania 😭😭😭
 
Vilaza wanazidi kujipenyeza nafasi nyeti, Nchi ya ******* hii, utashangaa anakua kweli mbunge
Yaan halaf tunashangaa wakitunga sheria za hovyo?
Unapo peleka un qualified individuals usitegemee matokeo mazuri

Is why sheria ya kujua kosoma na kuandika ifutwe kabisa.
Educational background iwe walau degree , plus kupigwe interview kabisa majimboni ila wananchi waone

Wakienda kwenye uchaguzi wajue wanaenda na nani.
 
Kwa unyeti wa hii taasisi "bunge" ilitakiwa angalau kigezo mtu awe na degree

Hivi tuseme ukweli kama ile bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 yale maneno ya kiuchumi na financial terms alizokuwa anatamka Mwigulu, hivi kweli Musukuma alikuwa anaelewa au alikuwa anapiga tu meza ipite?

Hyo dogo kama kweli atapita basi bunge litakuwa limeongeza kilaza mwingine mgonga meza
​
 
Best wishes Harmorapa. Waziri ajaye wa uchumi
Atatekeleza sera ya kukopa ili kuleta maendeleo🤣
1000041275.jpg
 
Ndugu na karibu na harmonize wajiandae ubunge bila kafara kwa bongo ni ngumu.

Kuna waziri mmoja kapoteza baba yake juzi karibu na uchaguzi
Kuna waziri mmoja anacheza namba ya lomalisa kapoteza mdogo wake juzi wakiwa dodoma
Babu tale tayari kashafanya yake mapema kama kawaida yake
Karibia mawaziri wote ninaowajua mpaka jiwe kama hawajapoteza watoto basi ni ndugu wa karibu mnaotaka ubunge mjipange.
Yule jamaa anayejifanya anawaza nje ya box anayegombana na MO dewji kila siku yule ndio hana hata aibu kabisa kwenye kufanya mambo hayo wakimkosa ndugu au watoto au mke inapita na wenyewe moja kwa moja.
 
Ndugu na karibu na harmonize wajiandae ubunge bila kafara kwa bongo ni ngumu.

Kuna waziri mmoja kapoteza baba yake juzi karibu na uchaguzi
Kuna waziri mmoja anacheza namba ya lomalisa kapoteza mdogo wake juzi wakiwa dodoma
Babu tale tayari kashafanya yake mapema kama kawaida yake
Karibia mawaziri wote ninaowajua mpaka jiwe kama hawajapoteza watoto basi ni ndugu wa karibu mnaotaka ubunge mjipange.
Yule jamaa anayejifanya anawaza nje ya box anayegombana na MO dewji kila siku yule ndio hana hata aibu kabisa kwenye kufanya mambo hayo wakimkosa ndugu au watoto au mke inapita na wenyewe moja kwa moja.
 
Oooh vile vitanda maalum atavipiga miti mpk waanze kusutana pale langoni
 
Kua mbunge Tanzania ni UJUE KUSOMA NA KUANDIKA TU.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Huyu kijana wake alisema ana michezo ya kufukua tope, serikali na chama vime mkumbatia
Bungeni Kuna michezo hio patamfaa sana kama ataona vina umuhim, ila akitumia umaaarufu wake vizuri na kuchukua ushauri wa uongozi kutoka kwa viongozi wenye HOFU ya Mungu na wenye uzalendo ataisaidia sana Tandahimba alikozaliwa Huko
 
Back
Top Bottom