Harmonize anakuja na mapinduzi ya Kijeshi kuinua muziki

mohamed ismail

Verified Member
Mar 16, 2014
196
250
Ilinichukua muda nikiwa kimya najiuliza maswali siyo chini ya 20 kwamba Harmonize ataingia jukwaani kwa style gani? Sikutegemea kuona akija na helikopta maana alishaitumia kwenye mazoezi. Nikiwa kwenye tafakuri nikaona watu wanapita na farasi mara wengine na vibaiskeli nikahisi huyu mtu hakawii kuja na tembo uwanjani.

Konde ni mtu wa kuthubutu nani alijua kwamba angetoka Wasafi na akasimama kama alivyo sasa? Ni mtu asiyekata tamaa na shupavu ambaye damu yake ina chembechembe za Kinjekitile pamoja na Mtwa Mkwawa.

Nikiwa kwenye runinga niliona mtu anatambaa kwenye kamba kutoka angani huku akipeperusha bendera ya Yanga kwa madoido.... Nikamuambia mtu niliyekuwa naye karibu huyo ndio Konde akaniambia hapana hawezi kuwa yeye itakuwa katumia Komando wa jeshi.

Uwanja ukiwa umekaa kimya na wale wenzangu na mimi wenye roho nyepesi walishindwa kuangalia tukio wakaangalia chini. Mara paap! tuliona yule mmakonde aliyetokea kijijini Chitoli akidondoka kama kitenesi na kudunda na baada ya hapo akaendelea kuwatumbuiza wananchi. Wananchi walinyanyuka kwa furaha wakaona kweli Yanga mpya imezaliwa na kitendo hiki kilifanya wananchi wajisikie vibaya maana waliona kiingilio kimekuwa kidogo kulingana na show babkubwa waliyoipata.

Harmonize ujasiri wake ni kama wa sisimizi wawezao kuvuka mto kwa kuwafanya sisimizi wenzao waliokufa na kuelea majini kama daraja lao. Baadae yule jirani akaniambia huyu mtoto siyo wa kawaida maana hayo ni mafunzo ya kijeshi. Na huwa si chini ya wiki tatu ili mtu aweze kuiva. Na ukienda kwenye mafunzo ya ukomando kwenye Airborne ndio utakutana na hizo Commando rope kwa kutumia Carabiner ambapo hili tukio kitaalamu kijeshi wanaita Rappel seat method.

Mlimwengu mimi nasema hivi kwamba wapenda muziki tumepata jibu maana huyu mmakonde anakuja na mapinduzi ya kijeshi. Na hii imedhihirisha umma kupitia siku ya mwananchi kwamba Harmonize ni mjeshi kamili na mwanamuziki aliyekamilika.

#mlimwengumimi

B4B16DE0-932E-4D51-B05F-5F728437221D.jpg
 
anthony_art

JF-Expert Member
Jul 9, 2020
213
250
Bado anayo safari ndefu Sana mpk alipo saivi bado hajafikia ukubwa wa diamond Ila ana mwanzo mzuri anatumia trending story vizuri hakauki kwenye midomo ya wa2 lakini alete kazi zaidi zenye ubora apunguze matumizi ya 'I no go' kwenye nyimbo zake pia apunguze 'sampling' hasa kwenye album zake azidi kujituma ubunifu zaidi kuwa midomoni mwa wa2 sio ukubwa kimuziki
 
Top leader

JF-Expert Member
Aug 20, 2020
203
500
Harmonize bado sana haswa kuwapita watu kama diamond platnum ni ndoto kwa nn kwa sababu still anaiga diamond nn anafanya ni sawa kucheza na barcelona ukiwa unapiga pasi sana kama arsenal ya wenger huwezi kumfunga labda upige counter attack uende tofauti nae ndo utamdhiti

Kingine ajue huu mziki wa sasa wa ovyo wa kucheza cheza tu ni staili ya wcb au mond ndo kaleta huu uzungu wao wanafanya kama yeye wote ni ngumu kumpita labda watu wa singeli na hiphop wanaweza kustruggle kumpita

Ujinga kafanya harmonize ni chuki kutaka kumfunika mtu mbaya zaidi kwa Tz hata africa kwa show hawamuwezi diamond except malegend kama kofi olomide,fally ipupa na p square ambao sio waafrika kwa sasa

Kaona jamaa kaingia ivi basi anafanya ivi then anaropoka sana kwanza 70% katembelea shortcuts ya diamond kila kona alikuwa anaenda nae mpaka kukutana na watu wakubwa nje kifupi harmonize aje na style mpya ya muziki wake mfano zamani walikuwa huwezi kumjua mkali wa game maana mr nice ana mfumo wake juma nature wake matonya wake mr blue wake ,ukija feroux wake njoo sasa kwa dully sykes ana ladha yake pia ila wa sasa video ikianza ujue utaona walllpaper kwa nyumawatu wanacheza tu hamna yale mazingira ya kipekee nyimbo zipo vinafanana thuw why kuja kumpita master wa hizo nyimbo ambaye ni diamond ngumu sana
 
Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,842
2,000

Mleta uzi hana hamu, anataman aufute uzi tu make raia hawamuelew kabsa huyo mmakonde.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom