gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,674
- Thread starter
- #21
Last edited by a moderator:
Opps, hapo blue, ndo mnafanya socialization kwa jinsi hii?
Mie kuna siku nilikuuliza, je ukiolewa na Baresa unaacha kazi uwe pika pakua?
yeye kasema her brain works good if she makes things happen. so hata kwa baressa anaweza akawa ndiye mkanda unga wa chapati ama mwoka mikate unamtania halafu uzuri wa jembe hili halichagui shamba bana yani popote pale linapiga tu.
Ngoja nitafakari, hard working au mazoea?
'Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo'
Hii naiangalia zaidi kama ni athari ya makuzi mtu aliyopitia
Mfano, unakuta mdada tangu utotoni kazoezwa kuwa 'responsible' kwa vitu vilivyo ndani ya uwezo wake
Hata akiolewa tabia ile inaendelea, mfano hata kama mmewe ni mkurugenzi na mke ni Mwalimu wa shule ya msingi, utakuta mama akipata mshahara tu, basi ka shopping ka jikoni hasahau.
Wakati anajua fika kuwa hata gari anayotumia kwendea kazini ni mmewe anai-service kkila kitu hadi mafuta, ila mwanamke wa aina hii ile moyo wa kuwajibika uko ndani yake. Hujawahi ona hii?
Mwanamke huyu huyu akiolewa na mwanamme mwenye kipato sawa, akibahatisha mwanammme aliyekuzwa kwa kuwajibika pia, basi utakuta aina ya familia yenye ushiriakiano kama siafu. Kipato kinawekwa mezani, kila mtu na majukumu yake, maisha yanasonga.
Balaa linakuja pale mwanamke wa aina hii anayekutana na mwanamme mwenye aidha kipato sawa ila hakulelewa kwenye mazingira ya uwajibikaji. Mwanamme wa aina hii akiona mkewe ananaunua sukari tu na vitumbua yeye anaona wameshamaliza maisha na anaona kama mkwewe ni 'Newton' nikimaanisha anaweza kufanya yasiyowezekana.
NA kama mwanamke huyu akiolewa na mwanamme anayemzidi kipato, hawezi subiri mmewe alete vitu ambavyo mke anajua kabisa anaweza fanya mwenyewe.
Hii ni athari ya malezi zaidi, ku-take responsibility, na kama uko dizaini hii hata ufanyeje ngumiu sana kubadilika hapa unapojikuta unaishi na 'mzembe'
3. Wamama Wanyamwezi na wamanyema! Kutwaaa pesa yote kusaidia nduguzo. Hata hamuendelei wewe ndo umejitwisha familia yenu mazimaaaa! Haihusu kabisaaaa. Pesa zote watuma nymbani!!!
Mwalimu
Pamoja na kuwa nimeajiriwa lakini ni mjasiriamali pia,
Ujasiriamali siyo lelemama inatakiwa kujituma haswa,
kama mama ambaye niko na watoto wangu 4 nina hakika
ya kutengeneza hela nzuri tu nje ya salary.
I wish wamama wote wangejituma maisha yasingesumbua
but wamama we should work hard.
Owkay, kuna wamama huwa wanasema, 'mie sichangii chochote nyumbani kwangu, mme wangu ana hela zaidi yangu'
Unakuta anayesema hivyo ni mtu na kazi yake tu ya maana na anamiliki labda kadegree kamoja, sasa naaki najiuliza, unaweza ishi bila majukumu kabisa?
lara 1 again,
yaani haya uliyoongea lara ukisema ukayafanye humo ndani wanao very soon watavimba utapiamlo. uzuri jamani mtasema hivyo hujakuwa ndani ukiwa ndai kwanza hutaelewa kumwona mwanao haendi shule kisa kakosa ada, ama hali kisa hakuna chakula na hii ndio hali halisi ya maisha ya ndoa.
muulize mama lara atakuambia kwamba muda miwngine alishindwa kuvaa vzr ili nyie msome na kula na mtibiwe na hapo so kwamba baba lara hayupo ama wamegombana hapana lkn hatoi tu.
tena ujue kwa wanwake wengi wanaojitambua kuomba hela kwa waume zao ni kitu kigumu sana sana sasa unamkuta mtu anaona kabasaa hapa pana tatizo lkn hadi uombe hela ya kutatulia why?? basi mtu kama mm siombi nafanya niwezavyo ishu ipite basiiiii. ndani ni tofauti sana na haya ambaayo huwa tunatamanai yawe hivyo
simwelewi mtu anyeish pasi majukumu kabisa halafu ni mzazi.He he he, usikute napiga misele tu mjini
Ila kutimiza wajibu inakupa aina fulani ya 'maana ya maisha'
Kuishi bila majukumu nacho ni kipaji, si kila mtu anaweza.
Mama Lara hatoi hata senti tano. Alitoaga tu kipindi cha mpito wakati mwenzie hayupo kakwama nchi za watu! Ila kama yupo ndani hatoi!
Kuna majukmu keshajipangia ndo anatoa, na mengine ni ya mdingi. Akishafanya vyake baaaaaaaaass.
Tumerudishwa ada si mara moja au mbili. Kama tano hivi. Akikuona nyumbani anakwambia ongea na baba yako uzuri, masomo yanakupita kule! Namwambia baba hana! Atapata tu, usiwe na wasiwasi, atapata tu mwanangu mzuri!
Ananiambia hata mimi, usiwe na roho nyepesi, wanaume hawa bila kuwakazia hutowaweza kabisaaaaa! We mtu anafanya kazi na business inakuwaje hana hela za kulisha familia? Ujanja ujanja tu huo!
umesema vyema Kongosho ila unajua kwamba kuna watu ambao wameumbwa tu hivyo?? yaani ten aunamkuta sio mtu mwenye gubu wala nn na hata utafute kosa gani kwake hulipati kabisa.
ukija kwenye ku care na kupenda ndo wa kwanza manake hata akiwah kurudi job atatangulia home kukusubiri urudi ili mtoke lakin inapokuja kwenye kujituma kimaendeleo hayupo kabisaaa.
mfano unakuta labda kuna kazi ya kufanya mama unasema basi ngoja mie nikope tufanye haya, kweli unakopa mnafanya yeye mwenzio ingawa anajua na mshahara wako umekopea bado kuona ana wiwa kutoa kwaajili ya mambo mengine haipo akilini mwake. na kutwa kucha atakusifia na kuppreciate kwa uliyoyafanya.
kuna shoga yangu mmoja kweli hadi anauguza ndugu wa mume mwenye ndugu hastuki kabisaa ila kila siku wanamigia simu kumshukuru kwa jinsi ambavyo shemeji anajitoa kuwasaidia kwenye ugonjwa sasa hivi huyu baba hajiulizi mke wangu anapata wapi hizi hela?? ama aseme ngoja basi na mm nimsaidie wife kwa hii kidogo??
anyways mie huwaga nasema kam shida ni hela ai will solicit mine kwani upendo na amani uliopo unatosha
tena siku watu tuna graduate baba anapewa sifa zote kasomesha watoto ila ukweli mama ndo anajua na sisi. binafsi sionagi manitiki ya kumwambaia mtu naomba hela ya ada ya watoto kwan hawaoni?? kwann nimwambie?? kwanza naanzaje kumwambia?? kwann asisieme ada hi hapa??
atakuwa amebarikiwa kuliko wanaume wote duniani? kama unategemea ulale ,uuze sura,uje ugombanie mkorogo wangu asubuhi dressing table mimi nikulishe na wanao mjini hapa utasubiri sanaayaani atakaye waoa kingasti na smile ana kazi ,nampa pole