Harambee.

samanya

Member
Feb 1, 2011
48
6
Askofu aliendesha harambee kuchangia ujenzi wa kanisa. Wakristo wakatoa Tshs 750,500 tu. Ghafla majambazi wakateka kanisa na kuamrisha kila mtu atoe alichonacho! Wakakusanya Tshs8,945,800 na kumkabidhi askofu ili aendeleze ujenzi. Je majambazi wana dhambi au wakristo wanathawabu? Toa maoni yako.
 
Majambazi wana dhambi tu kwani watu wanamajukumu hata mengine sio hela yote ni ya kujitolea kwani hautaeleweka ukibakiza watoto nyumbani kisa ada yote umetoa kanisani kwa ajili ya ujenzi, utasomeka kuwa na dhambi wewe, dawa ni kumshauri mchungaji awarudishie watu hela baada ya majambazi kuondoka.
 
majambazi hawana dhambi ila wakristo wana dhmabi ya uchoyo.

Nikama Mungu alivyomtumia Nebukadreza, Mfalme Koresh au Senekarebu kuiadhibu Israel pale Israel walipomkosea Mungu. Na aliwaita hawa akina koreshi watumishi wake.
 
Jamani wana JF mbona hamsumbui kichwa, jambazi ni fani na ina taratibu zake na kanuni zake hapa ukifuatilia hakuna sifa za jambazi zilizofuatwa, huu ulikuwa mchezo wa kuigiza tu na zoezi zima limekiuka kanuni za kijambazi hivyo ni batili
 
Majambazi wana dhambi tu kwani watu wanamajukumu hata mengine sio hela yote ni ya kujitolea kwani hautaeleweka ukibakiza watoto nyumbani kisa ada yote umetoa kanisani kwa ajili ya ujenzi, utasomeka kuwa na dhambi wewe, dawa ni kumshauri mchungaji awarudishie watu hela baada ya majambazi kuondoka.

kama hela ni ya ada kaenda nayo kanisani ya nioi? Siwaungi mkono majambazi ila ni fundisho kwa waumini. Anachotakiwa kufanya mchungaji awaulize awarudishie au la.
 
kutoa ni moyo na sio kulazimishana. ukitoa milioni kwa kulazimishwa na mwingine akatoa buku kwa hiari na moyo, aliyetoa buku anakubalika zaidi machoni kwa mungu kuliko wa milioni moja. so majambazi wana dhambi.......
 
Jamani wana JF mbona hamsumbui kichwa, jambazi ni fani na ina taratibu zake na kanuni zake hapa ukifuatilia hakuna sifa za jambazi zilizofuatwa, huu ulikuwa mchezo wa kuigiza tu na zoezi zima limekiuka kanuni za kijambazi hivyo ni batili
Ahahahaaah kumbe kuna kanuni za kijambazi!
 
hao sio majambazi ni watu wenye nia na maendeleo ya haraka, nawapongeza kufanikisha fedha kupatikana haraka
 
Back
Top Bottom