Harakati za Mwigulu zinavyozidi kumharibia

Tanzania kwanza siasa baadae, hata kile kikao cha wanairamba kilikua ni cha Iramba kwanza siasa baadae, siasa hazikupewa nafasi, tatizo tu watu wengi wanachuki za kisiasa kuliko kukubaliana na uhalisia, waliohudhuria kile kikao wanajua kilichojadiliwa siku ile ya kikao cha wanairamba waishio dar, mambo mengi yaliyozungumzwa pale yalikua yanaihusu jamii ya Iramba na sio CCM wala Chadema, wanasiasa wanaeneza chuki pasipo na mantinki, kushirikiana na Mwigullu haimaanishi wewe ni mfuasi wake, kumbuka Mwigullu ni mbunge mwenye dhamana ya jimbo la Iramba Magharibi kwa sasa, ni lazima awajibike kwa wananchi wote haijalishi ni kutoka chama gani, tunastahili kumshauri, kumkanya na kumhoji pale inapodibi, kwa hiyo kikao kilichofanyika dar kilikua na malengo hayo ya kushauriana, kuhoji na kujenga umoja kati yetu wanairamba,afu suala la watu kualikwa kwenye kikao na kutokutokea ni chuki binafsi tu za kisiasa, ngoja ukikaribia uchaguzi tuitishe kikao tena uone kama watu hawatakuja wengi, sasa hao ndio wanakua na uroho wa madaraka, wanakuja ili waonekane wanajua sana kujadili mambo, ili hali ukiwaambia leo hii jamani kuna harambee ya kujenga hospitali ama shule kila mtu atadai yuko busy na majukumu yake binafsi, mambo hayaendi hivyo wandugu, ushirikiano ni muhimu sana, inamaana mwanao akikunyea mkono utaukata au utanawa tu na kuendelea na maisha, vivyo hivyo kwa ndg. Mwigullu nae ni mwanairamba lazima tukae nae tuzungumze nae na tushauriane, hatuwezi tukamsusa na kusubiria uchaguzi 2015, je kwa kipindi hiki kilichobaki nani atusemee bungeni, nani asimamie kazi za mbunge? Lazima ahusike tu, kikubwa ni kukemea mabaya yake na kuwekana sawa mambo yaende mbele, hii ni QUID PRO QUA- NOTHING GOES FOR NOTHING, tulimpatia kura zetu nae lazima atutumikie wanairamba, siasa zisitawale uhalisia, kuna wakati wa kupiga siasa hasa kipindi cha kampeni, sasa hivi ni muda wa vitendo dhidi ya maneno.
 
Huyo wa kushoto ndio alikuwa kiongozi wa UVCCM mbona anaonekana mzee hivyo? kama sikosei ana miaka zaidi ya 43

Umesahau kisa kilichomtoa Masauni Yusuf? UVCCM majanga
 

ungekuwa unaelekeza majungu yako kwa CHADEMA tungesema umepewa BUKU 7 za lumumba, sasa hapa sijui umepewa za UFIPA?
 

mkuu, kutoa lecture kama hii kwa mtu kimeo kabisa kama huyu ni matumizi mabaya ya muda na akili yako.

mwambie atujuze kama na yeye amelamba buku 3 za ufipa
 

Bwana Mwigulu Nchemba,


Nina maswali machache hapa napenda uyajibu ili wasomaji wa JF waweze kupata picha.
  1. Kuna wakti ulipotea ukasema ulikwenda nje ya nchi kwa majukumu ya kikazi. Uliporudi ukaanza kuvalia hiyo kofia ya KIJANI NA NYOTA NYEKUNDU. Swali ni: Je ulikwenda kuchukua mafunzo gani na hiyo kofia inamaanisha nini kwako na kwa wana CCM wenzako?
  2. Kwanini tangu uanze kuvaa hiyo kofia umekuwa na ukatili usiomithilika kwa Watanzania wenzako ambao wana mtazamo tofauti na CCM na hasa chama cha CDM na viongozi wake?
  3. Juzi umesimama Bungeni kuuliza swali kuhusu Viongozi waandamizi wa CDM kwa maana ya Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Slaa ukitaka kwanini wasifungwe jela kwa kusababisha mauaji Morogoro,Iringa,Arusha na Ndago.Je,wewe siku hizi umekuwa ndiye Mahakama Kuu,Jaji Mkuu na Polisi wa Nchi hii?
  4. Kitila Mkumbo ni Mhadhiri Chuo Kikuu ambako wewe ndiyo ulisoma Digrii yako ya Kwanza ya Uchumi. Kwanini unamdharau Kitila Mkumbo wakti ni ndugu yako na mnatoka sehemu moja ka vile tu yuko CDM? Wewe unaposema yeye siyo saizi yake na hata Viongozi wa CDM wanakuogopa una maana gani?
  5. Hivi wewe unafikiri siasa za Majitaka kwa Viongozi wa CDM kwa kuwabambikia kesi za kigaidi na zisizokuwa na kichwa wala miguu ndiyo watakuogopa?


Mwisho napenda kukupa ushauri wa bure. Kwamba kwa sasa wewe ni kiongozi ambaye Watanzania wanakuona kama mchochezi,mgomvi na mwenye chuki kwa wapinzani. Matukio ya Bomu la Arusha kule Soweto pamoja na matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani katika Kata 4 za Arusha limekuaibisha sana kama hujijui.

Kauli zako wakti wa Kampeni za Udiwani pamoja na kutembea na Tesha ambaye ni mwathirika wa Tindikali lakini wewe ulimtumia kama Kinyago kwa ajili ya kuichafua CDM ili kuisaidia CCM bado haikukisaidia chama chako cha CCM. Hili ni fundisho tosha kwa mtu mwenye akili timamu. Sina hakika kama una akili timamu ya kuweza kusoma na kuelewa alama za nyakati na kubadili mwelekeo!
 
Endelea kujidanganya eti wanakuhofia,mbona hawakutajitaji kama wewe ufanyavyo?
Nani anamhofia mwenzie hapo?
 

watanzania tutumie kura yetu vizur tukiwatoa ccm viongozi kama mwigu hatutawaona tena
 
mkuu mpigie simu umueleze, unatuchosha
 
Kwa Mh mwigulu mchemba(mbunge iramba magharibi,naibu katibu mkuu CCM)
Juzi umesimama Bungeni kuuliza swali kuhusu Viongozi waandamizi wa CDM kwa maana ya Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Slaa ukitaka kwanini wasifungwe jela kwa kusababisha mauaji Morogoro,Iringa,Arusha na Ndago.Je,wewe siku hizi umekuwa ndiye polisi,Mahakama Kuu,Jaji Mkuu ?

zingatia blue
1.Ulisema una ushahidi kuwa CDM walihusika na bomu la Arusha ulishaupeleka polisi?
2.Ulisema una ushahidi wa mauaji Morogoro,Iringa,Ndago na Arusha wamefanya viongozi waandamizi wa CDM pls tuwekee humuhumu JF polisi wataufanyia kazi tu kama ule mkanda wa Lekwatare
3.Mauaji ya Iringa unamaanisha yale ya MWANGOSI(R.I.P)?
4.Mauaji ya Morogoro ni ya yule kijana aliyepigwa risasi ktk kibanda cha muuza magazeti?
5.Mauaji ya Arusha ni yale ya vijana watatu waliopigwa risasi wakati wa maandamano ya CDM? au ni yale ya mlipuko wa BOMU katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani au yale ya mlipuko wa BOMU katika ibada ya kanisa katoliki au yale ya kiongozi wa CDM wilaya ya Arumeru aliyechinjwa kama kuku?
6.Mkuu yale ya Ndago kesi ipo mahakamani si ingekuwa vyema tukasubiri uhamuzi wa mahakama?
Inawezeka ukajikweza kuwa wewe ni mkuu kuliko Dr kitila Nkumbo sawa tuthibitishie,mimi namuona huyu Dr Kitila Nkumbo ni kati ya wasomi wa ukweli katika taifa letu na ametoa mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Tanzania kuliko wewe labda wewe unidhibitishie vinginevyo
 

Mawazo ya kim'a's'a'b'u'r'i
 
Kuongoza jimbo na ccm ndo ujiite kiongozi wa kitaifa wewe ni kiongozi wa iramba na ccm sio taifa
 
Namchukia mwigulu kuliko shetani coz hajali maslahi ya taifa anajali maslahi ya kwake, chama mufilisi na mafisadi anaowatetea ktk makundi ya ccm(lowasa).
 

Maombi/dozi yamekubali umeanza kuwa mstaarabu kdogo ingawaje tolerance yakpo bado hatujaijua.Duh Dr kitila siyo size yako una maana gani au kwa vile kakuzidi kielimu/kihoja na ushawishi?Viongozi wa CDM kama kweli wanakuogopa ni kutokana na matendo yako uharakati unaosababisha vifo vya waTz wakati hujali.ulimsababishia mauti Msisiemu mwenzio kule NNdago wala hilo hujali.
 

Lakini mengine hujayajibu! Khs kuwapendelea watoto wa diwani na mwlimu wako. Halafu huyo Mandi Kapendo una uhakika hakurudia shule?
 
Chadema mnaweweseka nn? Ni mtu mmoja tuu mmepewa kupambana nae kijasho kinawatoka jee mkipambana na akina Mwigulu kumi hv c mtachanganyikiwa na kupoteza muelekeo? Mlianza wenyewe siasa za mtindo huo sasa pambaneni Muone kilichomtoa khanga Manyoa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…