Kiula Mzalendo
New Member
- Jan 8, 2013
- 4
- 0
Tanzania kwanza siasa baadae, hata kile kikao cha wanairamba kilikua ni cha Iramba kwanza siasa baadae, siasa hazikupewa nafasi, tatizo tu watu wengi wanachuki za kisiasa kuliko kukubaliana na uhalisia, waliohudhuria kile kikao wanajua kilichojadiliwa siku ile ya kikao cha wanairamba waishio dar, mambo mengi yaliyozungumzwa pale yalikua yanaihusu jamii ya Iramba na sio CCM wala Chadema, wanasiasa wanaeneza chuki pasipo na mantinki, kushirikiana na Mwigullu haimaanishi wewe ni mfuasi wake, kumbuka Mwigullu ni mbunge mwenye dhamana ya jimbo la Iramba Magharibi kwa sasa, ni lazima awajibike kwa wananchi wote haijalishi ni kutoka chama gani, tunastahili kumshauri, kumkanya na kumhoji pale inapodibi, kwa hiyo kikao kilichofanyika dar kilikua na malengo hayo ya kushauriana, kuhoji na kujenga umoja kati yetu wanairamba,afu suala la watu kualikwa kwenye kikao na kutokutokea ni chuki binafsi tu za kisiasa, ngoja ukikaribia uchaguzi tuitishe kikao tena uone kama watu hawatakuja wengi, sasa hao ndio wanakua na uroho wa madaraka, wanakuja ili waonekane wanajua sana kujadili mambo, ili hali ukiwaambia leo hii jamani kuna harambee ya kujenga hospitali ama shule kila mtu atadai yuko busy na majukumu yake binafsi, mambo hayaendi hivyo wandugu, ushirikiano ni muhimu sana, inamaana mwanao akikunyea mkono utaukata au utanawa tu na kuendelea na maisha, vivyo hivyo kwa ndg. Mwigullu nae ni mwanairamba lazima tukae nae tuzungumze nae na tushauriane, hatuwezi tukamsusa na kusubiria uchaguzi 2015, je kwa kipindi hiki kilichobaki nani atusemee bungeni, nani asimamie kazi za mbunge? Lazima ahusike tu, kikubwa ni kukemea mabaya yake na kuwekana sawa mambo yaende mbele, hii ni QUID PRO QUA- NOTHING GOES FOR NOTHING, tulimpatia kura zetu nae lazima atutumikie wanairamba, siasa zisitawale uhalisia, kuna wakati wa kupiga siasa hasa kipindi cha kampeni, sasa hivi ni muda wa vitendo dhidi ya maneno.