Avanti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2010
- 1,209
- 240
Nimevumilia sana ila inabidi tu kumweleza ukweli Bwana Mwigulu khs anavyozidi kuharibu jina na sifa zake kwa ajili tu ya uroho wa madaraka. Haipingiki kuwa Mwigulu ana uroho wa madaraka na hii inaweza kuthibitishwa na hata waliokuwa naye shule ya sekondari Mazengo. Mdogo wangu alikuwa naye kwa maana hiyo anamfahamu sana na anaweza kuzisimulia harakati za Mwigulu za utafutaji wa madaraka. Kuna mambo mengine km ya kurudia shule na yule rafiki/ndugu yake ambaye anajiita Inosenti - Diwani wa kata yao Mwigulu ambaye naye alirudia shule zaidi ya mara 3 na bahati mbaya form 4 yake pale Tumaini Sekondari alibumba. Huyu pia aliwahi kubadili badili sana majina, enzi fulani alirudia shule kwa jina la Mandi Kapendo - kama Mwigulu unabisha sema ushahidi uletwe. Kwa leo siongelei hayo ila kuna mambo machache tu yaliyotokea hivi karibuni yamenifanya unikere sana.
1. Wewe uliitisha kikao kwa Wanairamba Magharibi kule Dar na ukajifanya km vile umealikwa tu. Kikao hicho ulikiandaa km vile kuna sherehe kubwa ya harusi ukaandaa na futari lakini mafanikio yake nasikia yalikuwa madogo sana, kwani mpaka leo kikao hicho hakijakueletea mrejesho mzuri. Hapa inasemekana kuwa tayari wewe ulishauasi Mfuko wa Maendeleo ya Iramba ambao mlikuwa mnauanzisha na wenzako mnaoishi nao Dar kwa kuona kuwa huo Mfuko huo amejumuishwa Dr Kitila Mkumbo ambaye ni adui wako kiasiasa. Inasemekana uliomba mkutano then ulipoambiwa kufuata taratibu mlizojiwekea na wanakamati wenzako za kuitisha vikao ukakasirika na kuamua kumtumia yule kijana Daniel Manupa ambaye ameanzisha blogu ya Singida Connections ili ufanikiwe katika mambo yako lakini haukufanikiwa sana kutokana na kususwa kwa kikao hicho na wanakamati wenzako ambao hakufika hata mmoja. Inasemekana hasira hizo zililetekeza hadi ukaanza kuropoka mwisho wa kikao hicho kuwa wazee wa Iramba wanajidai na wanataka kufuatwa fuatwa majumbani kwao ndiyo wahudhurie kwenye kikao chako.Kuna ubaya km kuna wazee walikuambia uende ukaenda? Dharau hiyo umeipata wapi? Mbona inasemekana wakati unataka kugombea mwaka 2010 ulikuwa ukiambiwa uende kwa hao hao wazee ulikuwa unaenda? Leo umeshasahau Mwigulu?
2. Nimeelezwa na rafiki yangu ambaye anatoka kata moja na wewe anasema ulitoa takwimu mbalimbali siku ya kikao chako, ambazo zilikuwa ni za uwongo kwani hata shule ya Sekondari katani mwako ambapo ulisema umepeleka walimu 12 ilikuwa ni uwongo mtakatifu. Inasemekana shule hiyo ina walimu 6 tu wawili kati yao ni vijana waliomaliza sekondari na wanajitolea tu kufundisha. Nimeambiwa mbaya zaidi watoto wa mwalimu wako wa shule ya msingi Makunda na wa diwani rafiki yako Mandi Kapendo inasemakana umewahamisha toka shule hiyo kwa sababu unajua matatizo ya shule, mojawapo ikiwa ni ukosefu wa walimu. Kama umepeleka walimu kwa nini umewahamisha watoto hao?
3. Wewe uliamua kuipelaka timu ya Simba Iramba ili kuvuruga mkutano wa wapinzani wako ambao walikuwa wanaongelea mambo muhimu tu na jamii yako inapaswa kuyasikiliza, kuyajua au hata kuyapuuza kwa kadri ya uelewa wao. Kwako wewe, hata kama wewe uliingiliwa katika ratiba zako, ina maana mpira ulikuwa una maana sana kuliko mambo yaliyoongewa na CDM. Kwa ushabiki sana, ulitoa thread ya majigambo na ikiwataka CDM wakuheshimu. Mi nashangaa kwa nini ufanye mkutano huo wa CDM km visa? kwa nini usingekuwa mtu wa kwanza kusisitiza wananchi waende kusikiliza? Kwani kuna ubaya gani wewe kukaa karibu na Kitila Mkumbo kwa manufaa ya Iramba? Naamimi ungeweza hata kuwaomba CDM wafanye mkutano siku ingine wangekubali tu, ama hata wewe ungeweza kubadili siku ya uzinduzi wa ligi ya kombe lako, sidhani km siasa unazoendekeza zinakujenga - sana sana zinakubomoa sana. Badala ya kuzuia watu wasiende mikutano ya wapinzani wako kisiasa nadhani ungewasisitiza waende then ungekuwa unajijengea sifa kubwa sana pale unapojaribu hata wewe kukubali pale wanapoongea mambo ya maana na kuyacriticise kwa hoja nzuri yale yasiyo ya maana.
Mambo haya na mengine ni kweli yanadhihirisha ambavyo umeshakuwa na hofu sana kuwa njia zako za kukufikisha katika madaraka uyatakayo (uwaziri) zinaweza zisifanikiwe. Ni kweli kuwa wewe una uroho sana wa madaraka na nakumbuka kuna siku mwaka 2011 nikiwa na wewe wawili Arusha uliwahi kuongelea njonzi zako kuwa unataka baada ya muda mfupi jina lako lisikike na ulijitapa kuwa unaweza kuongea na mkuu wa nchi direct, then...
Mwigulu, katika kuchangia hoja kwenye thread hii, naona umemtetea sana diwani wako ambaye inasemekana ndiye alikuwa anakupeleka kwa wazee (sijui waganga wa kienyeji?) wakati unaanza harakati za kugombea ubunge. Huyu ambaye umetetea majina yake, nimejulishwa pia na ndugu yenu wa karibu kuwa huyu diwani naye aliwahi kujipachika majina ya Kusukuma kama wewe ili arudie shule. Inasemekana alipewa jina la Masaganya Zengo ambalo ndilo alisomea sekondari. Hii inaonesha ni jinsi gani wewe na huyo diwani wako mlivyo waongo waongo tu na mnadanganya danganya ili kuweza kufikia malengo yenu ya kutawala mkidhani hamjashtukiwa.