Harakati ya Fat'h ya Iraq: Vita dhidi ya Wazayuni ndio kwanza vimeanza

Malaria 2

JF-Expert Member
Oct 17, 2023
2,646
3,936
Mjumbe wa Muungano wa al Fat'h wa Iraq ameashiria jinsi makundi ya muqawama ya nchi hiyo yanavyoyaunga mkono makundi ya muqawama ya Palestina katika vita vya Ghaza na kusema kuwa, makundi hayo yataendelea kushambulia vituo vya wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Iraq.

Kanali ya Televisheni ya al Maaluma imemnukuu Eid al Hilali akisema hayo na kusisitiza kuwa, vita dhidi ya madola vamizi ya Kizayuni na Marekani ndio kwanza yako katika hatua zake za awali.

Ameongeza kuwa, vita dhidi ya Wazayuni na Wamarekani ndio kwanza vimeanza na vinapiganwa katika medani tofauti kuanzia huko Palestina hadi Lebanon, Yemen na Iraq.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Muungano wa Fat'h katika Bunge la Iraq ameongeza kuwa, wanajeshi wa Marekani hawana haki ya kufanya shambulizi lolote dhidi ya maeneo ya Iraq.

Mwaka 2003 Marekani iliivamia tena Iraq na tangu mwaka huo hadi hivi sasa inafanya njama za kuidhibiti nchi hiyo na inatumia visingizio tofauti kutia nguvu uwepo wake wa kivamizi nchini humo.

Dola hilo la kibeberu linafanya njama pia za kuingilia masuala yote ya Iraq, lakini wananchi na makundi ya muqawama ya Iraq, muda wote yamekuwa yakivuruga njama hizo za Marekani.
 
Back
Top Bottom