Happy National Bus laanguka Mbeya, Inyala

sexon2000

JF-Expert Member
Apr 18, 2010
299
65
Taarifa kwa simu kutoka Inyala, Mbeya zinasema basi la Happy National limeanguka baada ya kushindwa kuumudu mteremko wa pale TAZAMA, maarufu kama Pipeline.

Habari toka kwa abiria alipanda basi la Nganga, anasema watu wamejeruhiwa vibaya ila hakuna vifo.

Basi hilo likiwa kwenye mwendo kasi lilitaka kulipita basi la Nganga, lakini kukawa na gari jingine linapandisha mlima huo, ndipo dereva akalazimika kulirudisha nyuma ya basi la Nganga na kuligonga kwa nyuma na kupinduka. Abiria wa basi la Nganga wamesalimika wote.

Mlio Mbeya tupeni taarifa zaidi hapo rufaa.

Mungu ashukuliwe mgomo wa madaktari umeisha, vinginevyo!!!!!!.
 
Hao Happy nation wanaoenda Mby wanatembea mwendo mkali sana, hawana ustaarabu hata kidogo. Poleni majeruhi!
 
Poleni majeruhi, abiria tuwe wakali na madereva wasiofuata sheria za usalama bara barani.
 
Too bad!
Tunashukuru Mungu hakuna vifo, majeruhi Mungu awape nafuu!
Huu ni uzembe live...mtu yuko kwenye mteremko mkali kama wa hapo Pipeline, anajaribu kuovertake...shiit!
 
ni kweli Taifa lenye furaha limepata ajali na kama alivyosema mtoa mada kuwa hakuna vifo ila majeruhi ndio wapo na tayari polisi wa usalama barabarani wapo ktk eneo la tukio,kuna kijana mmoja yeye amepoteza vitambulisho vyake vyote vya bank na kazini hata hivyo bado yupo ktk eneo la tukio akijaribu kutafuta vitu vyake ingawaje ana maumivu ya kiuno na mgongo
 
Mabasi mengine sio ya kusafiria nayo kabisa, na hilo ni moja ya mabasi hayo!
 
Mabasi mengine sio ya kusafiria nayo kabisa, na hilo ni moja ya mabasi hayo!

Kwa kujazia, mabasi yaendayo Mbeya kama Al Saedy, Budget na Nganga si ya kupanda, wako rafu sana.
Mungu awape nafuu majeruhi
 
Mshukuruni Mungu kwa heri na uzima aliowapa siku ya leo maana tofauti na hapo tungekuwa tunaombeleza muda huu.
Madereva muwe makini haraka zenu zinatugharimu kila wakati.
 
hilo bus sio la kupanda linatembea mwendo wa hatari sana,nahisi wamechakachua engine!!haiwezekani bus linakimbia kuliko mengine
 
aiseeeeh haya mabasi haya,

haya ndo yaaale yaliyokua yakiitwa KILIMANJARO,

watu wakawa hawapandi yakabadilishwa rangi na jina.
 
hawa madereva wawe wanapimwa IQ kabla ya kupata reseni.
Tuanze kupima IQ ya MADAKTARI WETU kwa kutususia wagonjwa,IGP kwa kuridhia mwandishi habari za uchunguzi JERRY MURO, kufunguliwa kesi bandia kwa kuwaumbua matraffic police,TRAFFIC police kwa kugeuza magwanda meupe kuwa maduka,,Abiria wenyewe wa mabasi husika kwa kukubali dereva mmoja kuwaendesha kizembe watu wapatao zaidi ya sabini ndani ya basi,hadi kupelekea ajali huku wakiwa kimya. Bila kumkemea au kuwaambia maaskari waliojaa kibao mabarabarani.
.
 
Cha ajabu, abiria nao hupenda kupanda hayo magari kwa sababu yanawahi kufika.ndiyo maana dereva akiendesha gari kwa mwendo kasi,abiria wanakaa kimya.
 
Too bad!
Tunashukuru Mungu hakuna vifo, majeruhi Mungu awape nafuu!
Huu ni uzembe live...mtu yuko kwenye mteremko mkali kama wa hapo Pipeline, anajaribu kuovertake...shiit!

Source : Paka Jimmy
 
hilo bus sio la kupanda linatembea mwendo wa hatari sana,nahisi wamechakachua engine!!haiwezekani bus linakimbia kuliko mengine

Mkuu lile sio bus ni loli aina ya scania 114,engine yake ni kubwa sana na inanguvu sana,mara nyingi ndio linakuwa la kwanza kufika,wakati kuondoka linachelewa.
 
Back
Top Bottom