Nasema Uongo Ndugu Zangu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 279
- 773
Watu nane wamefariki Dunia na wengine ambao idadi yao haijafahamika wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea leo Jumanne, Agosti 16 katika eneo ya Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani Mbeya.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, akieleza kuwa gari la kKampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.
“Waliopoteza maisha ni nane japokuwa bado idadi rasmi haijajulikana ila baadaye taarifa ya daktari itaeleza kwa ujumla, ila majeruhi wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwamo Igawilo na Mkoa,” amesema Kamanda Matei.
-------
UPDATES
MBEYA: AJALI YA INYALA, WALIOFARIKI WAFIKIA 19
ldadi ya vifo katika ajali iliyotokea Leo Agosti 16, 2022 imefikia Watu 19 ambapo majeruhi wawili kati ya 10 hali zao inaelezwa kuwa ni mbaya.
Awali taarifa ya ajali hiyo iliyohusisha Lori lililobeba mchanga kisha kufeli breki na kugonga magari matatu katika maeneo ya Shamwengo, Kata ya Inyala Mkoani Mbeya ilidaiwa waliofariki Dunia ni wanne.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Urlich Matei amethibitisha idadi hiyo ya vifo 19.