Happy birthday Hon. Mwigulu L. Nchemba: Hizi ni salamu zangu kwako!

Status
Not open for further replies.
Hongera mjomba, kwa leo 7th july kutimiza umri wa miaka 33.ni umri wa kijana wa makamu na inabidi sasa uanze kuenenda kama umri wako, what do i mean by this?

Namaanisha sasa uache ile tabia ya kuropoka hovyo bungeni na kutumiwa kama afisa mipasho wa chama.

Kadhalika ,tumeshuhudia ukikiongoza chama chako kupoteza kiti cha ubunge jimbo la arumeru mashariki, kana kwamba ukistaajabu ya musa, majuzi tena bungeni umekurupuka na kukishutumu chadema kuhusika na mgomo wa madaktari na ukashindwa kuthibitisha:

Ni matarajio yangu kuwa kwa umri uliofikia leo, utajirekebisha uropokaji na kuanza kuishi kisomi na ki-kijana wa makamo!! nakutakia afya njema na mungu akujaalie busara kadri unavoongezeka umri!!

Happy birthday Mwigulu Nchemba

Ukichanganya na anavyobebwa na "mh. mwenyekiti" hiyo kazi anaiweza sana.
 
Umempa ushauri mzuri lakini sijui kama ata uzingatia maana ana huwezo mdogo wa kutafakari!

Mi nahisi ametimiza miaka 18 bwana, itakuwa mtoa mada umekosea kuangalia

mbona miaka uliyoitaja na yeye ni vitu vitatu tofauti? Au kuna mwigulu mwingine?

Jamani mna mkuza bwana si unasikia hata maneno yake yana onesha hawezi kuwa na hiyo miaka bhana.
Siamini macho yangu!
 
katika cv yake iliyopo bungeni , inaonyesha kazaliwa 7th july 1978, so ni miaka 33 mkuu

Kama kawaida ya watu wa magamba ,huyu lazima amegushi miaka ; haiwezekani kabisa kuwa ana umri wa miaka 33 kwani sura yake haiendani na miaka hiyo nadhani ana miaka karibia 50!!
 
Mwingulu kumbe una umri sawa na mimi? Mbona sasa unaongea pumba hivo! Linda hadhi ya umri huo. Uropokaji na kusema ujinga vitakuponza, jitambue. nakuombea kwa Mungu akupe walau busara kidogo tu upungoze nonsensi na stupidity.
 
CDM hawahitaji kuogopwa na m2,kazi yao kubwa waliyotumwa na Mungu na walalahoi wa nchi hii ni kutetea maslahi ya wananchi wao na kutoa hoja zenye mashiko,angalia kijana bungeni sio Darlive pakushuhudia taarabu zenye vijembe.
 
Hivi hujajua mpaka leo kuwa huyo jamaa yako ana "Behavioral Disoders"? Na wewe kama zuzu unamsifia badala ya kumsaidia apate huduma stahili.Kweli kwa wajinga kama nyie hakuna dawa

Huo ugonjwa ndio unamtafuna Lema mpaka kapoteza ubunge.
 
Mwigulu ni JEMBEEEEE pale mjengoni kila akisimama utasikia CDM wote wanamtizama na kusikitika utadhani kuna msiba, kumbe jamaa haogopi kuwaambia ukweli. Mwigulu ni sawa sawa na CDM wote bungeni


Duh kaka umefirisika mawazo kiasi hii??
Unamzungumzia huyu Nchemba??unamjua lkn au na ww ni wa kumuona tu kwenye TV unashabikia

Msaidie kujibu basi yale maswali magumu ya fedha za EPA aliyoulizwa bungweni basi na Mnyika!

Hv kumbe wapo watu wanafikra fupi kiasi hiki!
 
mwigulu nashindwa kuelewa ni nini kinampa confidence ya kuweza kuongea utumbo bungeni na kwenye mahojiano kwenye tv.au kule iramba hawana umeme hivyo wananchi awawezi kuona uchokozi anaoufanya dhidi ya wapinzani bungeni na media
 
Huo ugonjwa ndio unamtafuna Lema mpaka kapoteza ubunge.
Kama sio kulindwa na mafisadi anaowatumikia, Mwigulu alitakiwa awe amepoteza ubunge zamani sana. Hata wewe mwenyewe ni shahidi mkubwa kwa hilo. Kwa aliyoyafanya na kuonesha Igunga, Arumeru na bungeni hapa juzi, huhitaji shahidi kuthibitisha, lakini kwa kuwa mafisadi wananufaika na hii "behavioral disoder" ya huyu jamaa yako, wanaishia kumpamba na kumsifu kama unavyofanya wewe bila hata aibu au huruma kwake!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom