Mwigulu Nchemba usilalamike, Wewe ni mmoja wa waanzilishi wa siasa za "kuchafuana" na "kutesana"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Mwigulu Nchemba wewe nakuheshimu sana,umeeleza kwa kirefu jambo la siasa za "kumbambikiana mambo".Pole sana kwa "shutuma" zinazokukuta.Jipe moyo...Hii ndio tunaita "Post-Truth Politics",yaani kile kisicho cha kweli kinaaminika zaidi ya kile kilicho cha kweli.Yaani "ukweli halisi" unakujaa baadae sana baada ya "uwongo halisi" kutamalaki.Wewe ni muasisi wa aina hii ya siasa.

Aina hii ya siasa mlianzisha nyie,tena wewe ukiwa mmoja wapo.Ulitembea kwenye siasa hizi kwa muda mrefu,ukiwa kama mbunge na baadae kiongozi ndani ya chama,ulianza kwa kutupa na kuichanachana bajeti mbadala ya upinzani bungeni iliyoandaliwa na Zitto .Lile halikuwa ni tendo la "uungwana wa kisiasa".Kama mbunge kijana na msomi,uliwaangusha wengi na kuwakatisha tamaa wale wanapenda mtindo wa uvumilivu wa kisiasa.

Baadae ukaja kusema Lwakatare ni "Gaidi" na una ushahidi wa kutoa iwe mbinguni au duniani.Mbele ya kamera za Star Tv uliuthibitishia umma kuwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho anajihusisha na vitendo vya "ugaidi".Akaswekwa rumande,akawa jirani wa Sheikh Ponda huko mahabusu.Ikawa asubuhi,ikawa mchana na ikawa jioni,siku zikapita bila ushahidi wa mbinguni na duniani kupatikana.

Uliiumiza familia ya Lwakatare na yeye mwenyewe,katika ya ugonjwa wake wa kisukari alidhoofu na kunyong'onyea,na hakika mpaka anakufa sidhani kama atakusahau.Hii ni aina ya siasa ambazo "muasisi" wake ni Mwigulu Nchemba.

Ukazunguka na kijana aliyemwagiwa tindikali huko Igunga na ukampandisha kwenye majukwaa,ukisema kamwagiwa na Chadema.Na hata siku moja vyombo vya dola na umahiri wake,havikuwahi kuwatia nguvuni hao walioshiriki uharamia ule.Hii kwako ilikuwa ni karata nzuri kukihusisha chama cha upinzani na "ugaidi".

Ukaenda mbele zaidi kwa kuandika humu [HASHTAG]#JamiiForums[/HASHTAG] kuwa [HASHTAG]#DrSlaa[/HASHTAG] anahusika na kuanzishwa kwa RedBrigade inayouwa watu.Hizi zilikuwa ni aina ya siasa mbaya sana mlizozianzisha.

Mkiwa na Katibu Mkuu wako wakati ule Wilson Mkama,mlisambaza habari kuwa Chadema wameingiza "silaha" toka Pakistan ili kuja kufanya ugaidi ndani ya nchi.Bomu la Olasiti na upotevu wa roho za watu katika mkutano wa Chadema Arusha,ni kumbukumbu ya damu iliyomwagika ktk uso wa ardhi bila hatia.

Kuanzia hapo,kila uliposimama na kuongea,watu walitikisika,wakaogopa na safari yako ya Uchina iliyokubadili hata na aina ya mavazi ikachukua nafasi.Sasa ukaanza kuvaa mavazi ya "mgambo" na kofia yenye nyota nyekundu.Ukijiita "Field Marshall" na wengine wakakuita "Savimbi".Pengine jina hili la pili,lilisadifu aina ya siasa ambazo watu wanahisi unajihusisha nazo.

Sasa mambo haya yanaanza kukurudia.Katika kipindi ambacho unatakiwa ujitengeneze kwa ajili ya nafasi za uongozi wa kitaifa wa miaka ijayo,unajikuta nyuma uliacha nyayo zenye hisia ya "damu" isiyo na hatia.Pengine ilikuwa ni ugeni ktk siasa,au kutumika bila kujijua.

Mkuu badilika,achaneni na aina hii ya siasa,nyie bado vijana wadogo na viongozi wa kesho.Mnayoyafanya leo yanabaki ktk kumbukumbu zinazowafanya kesho mkose kuaminiwa.Madhira na chuki mnazopandikiza ktk mioyo ya watu,havipotei kama moto wa kifuu,bali hudumu chini kwa chini kama moto wa pumba.

Kumbukeni kuwa,kuna maisha ya vizazi vyenu hata ninyi baada ya kufa.Na ndio maana Julius Caiser alipoulizwa unatenda wema wa nini wakati utakufa?Alijibu "Non Omnis Moriar" ie "Not all of me,Will die".Tenda yaliyo bora kwa ajili yako na vizazi vyako.

Aina hiyo ya mambo yanayokutokea sasa;Watu wakihoji masuala ya uhusiano wa wewe na kupotea kwa Ben Saanane na namna ulivyosikitika kwa "uzushi" huo na kunung'unika,ndivyo hali hiyo ilivyowakumba wale waliopata kuathirika na aina hiyo ya "Post-Truth Politics" mliyoiasisi wewe na makomredi wenzako.

Fungueni ukurasa mpya,endesheni siasa za hoja na masuala.Sio siasa za mtu na utu wake.Hii ni aina moja wapo ya "Fallacy"(an error of thinking),ambayo wajuzi wa logic kama sehemu ya wigo mdogo wa falsafa;wanaiita "Argumentum ad hominem"

Nb:Wakumbushe polisi kuwa [HASHTAG]#JamiiForums[/HASHTAG] ina umuhimu wake;kama huu unaotolea ufafanuzi hapa kuhusu shutuma zilizokuandama.
2013,Shahidi:Mwigulu alikodi watu kufanya fujo Singida
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,002
2,000
Jana nilikataa kujibishana naye kwa sababu hakujibu swali hata moja nililouliza........

Mtu unaulizwa kuhusu Soweto wewe unajibu hata Lema anajua.........

Mtu unaulizwa uko na ushahidi wa Lwakatare kuwa ni gaidi unajibu kuwa ushaidi uliuficha how come waziri mwenye dhamana ya ulinzi anaficha ushaidi wa Gaidi eti kesi imalizike tu hivyo hivyo waziri wa usalama analinda magaidi na Magufuli anakubali hili?.......

Unaulizwa kwanini Maiti 7 zilizikwa bila kutambuliwa unajibu zilikuwa zimearibuka na ni waamiaji haramu!! How come? waamiaji haramu wazikwe bila kutambuliwa? Hiyo mifupa inafanyiwa DNA wapi na lini majibu yake yatatoka je waliopotelewa na ndugu zao kama Fucus Saanane wataruhusiwa kushiriki?...

Unaulizwa Ben Saanane yuko wapi unajibu Ben Saanane ni Rafiki yangu na tuliwasiliana mpaka siku ya wiki ya mwisho!!!

Rafiki yako anapotea na wewe unakaa kimya unakuja kutoa tamko baada ya tuhuma za kuusika kupotea kwa rafiki yako?.......

Nilikuwa nakuheshimu sana Mwigulu lakini kwa kauli yako ya Jana kuwa Ben ni rafiki yako wewe lazima anajua kinachoendelea juu ya Ben..............

Jiulize tu why always you?

Laana hii haitaacha mtu anayechezea maisha ya wengine....................
 

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
2,968
2,000
Tatizo huwa wanasahau waliko toka.

MN ni mmoja ya wanasiasa waliowahi kuchukiwa na kutajwa sana humu ndani.

Kuna siku alikula ban kwa kututukana ki-lugha. Uzuri Jamiiforums huwa inaweka kumbukumbu na ndio maana napingana na wote wanaosema kuwe na kitufe na kufuta thread. Huyu angekuwa alishafuta thread zake zote.

Huyu jamaa ni mwanasiasa anayefuata falsafa za kimachiavelli.

"Matendo ya kinyama yatekelezwe haraka na vikali kwa sababu yatasahauliwa, lakini mema yatolewe pole pole na kidogo kidogo ili yakumbukwe kwa muda mrefu" - Machiavelli-
 

mtafiti05

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
963
1,000
Viongoz vijana wamekuwa wa hovyoo kweli mmesahau kuwa bado maisha yhanaendelea? Mnashka wadhifa mnajfanya ninyi ni miungu watu, mnafanya lijalo kichwan mwenu bila kuona kama kuna wengne wanaumia?

Hukumu hutoka kwa mungu tu hivyo msijihesabie haki, SIASA za za kunadi ccm tu nakugandamiza vyama vingne nahs elimu ya siasa mnavamia!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom