Elections 2015 Kutoka Chuo cha Mipango, Dodoma: Mwigulu Nchemba atangaza nia kugombea Urais

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Sasa ni zamu ya Mwigulu Nchemba na anatarajia kutangaza nia kuanzia saa 9 mchana wa leo na atafanya hivyo live kupitia star tv akiwa Chuo cha Mipango, Dodoma.
mwigulu.jpg
Muda: saa 9 Alasiri hadi Saa 12 Jion.
Mahali: Chuo cha Mipango Dodoma.
Ukumbi: Mwl. Nyerere Hall

KAULI MBIU YA MWIGULU: MABADILIKO NI VITENDO, WAKATI NI SASA

Mwigulu anadai alibeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.

Pia naona Mwigulu anamponda EL kiani kwa kusema watu wanajisifu kuwa wamekuwepo serikalini muda mrefu wakati huo huo wamelisababishia Taifa hasara kubwa katika muda huo mrefu waliokaa serikalini.

Inasikitisha kumuona analalamikia mambo mengi yanayoendelea chini ya serikali hii ya CCM wakati kila siku wanawakejeli wapinzani wanapolalamikia na kuhoji mambo hayo Bungeni.

Kwa kifupi,Mwigulu leo anaivua nguo CCM hadharani na zaidi leo anamponda kiana mh.sana na pia anaonyesha kuwa Mkulu na chama chake wamekuwa ni dhaifu.

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ametangaza nia yake ya kugombea urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba akieleza jinsi atakavyoivusha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati utakaopatikana kwa kutoa haki kwa watu wote.

Akitangaza nia hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Mipango Dodoma, Nchemba alisema: "Ahadi yangu kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha. Nitawavusha wanaCCM wenzangu pamoja na Watanzania kwa ujumla… wakati ni sasa tunataka Taifa letu lifike kuwa nchi yenye uchumi wa kati," alisema Nchemba na kuongeza:

"Ninachoomba kutoka kwenu, mniamini na mniunge mkono katika hili… nitawavusha. Lakini tukumbuke kwamba kila mmoja lazima atimize wajibu wake katika utendaji kazi ili tufikie huko tunapotaka kufikia."

Nchemba aliyekuwa ameongozana na mkewe, Neema na watoto wake watatu, Isaack, Grecious na Joshua pamoja na ndugu jamaa na marafiki, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo hayo, lazima nchi iwe na mfumo wa uwajibikaji utakaowezesha kulinda rasilimali za Taifa na kuongeza Pato la Taifa.

Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko ni Matendo, Wakati ni Sasa', ambayo ataitumia katika safari yake ya kuelekea Ikulu, Nchemba aliyetumia dakika 115, kuanzia saa 10.10 jioni hadi saa 11.25 jioni, alisema atapambana na tabia za watu kufanya kazi kwa mazoea, rushwa, ufisadi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano atakayoiongoza endapo atachaguliwa, itakuwa ya uadilifu na uaminifu.

Alisema iwapo atachaguliwa, ataifanya nchi kuwa ya kipato cha kati sambamba na watu wake, kujenga Taifa linalojitegemea kibajeti na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.

Huku akieleza jinsi atakavyomaliza kilio cha ukosefu wa ajira, wanafunzi, wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara na watu wa kada mbalimbali nchini, Nchemba alianza hotuba yake kwa kuwashukia baadhi ya watu wenye dhana potofu juu ya mtu anayestahili kuwa rais wa nchi.

"Nimeamua kutangazia nia hapa Dodoma kwa sababu ndipo makao makuu ya nchi na kama nikiwa rais nitaapishiwa hapa. Pia sikutaka kutangazia nia nyumbani Iramba ili kuondokana na umimi," alisema na kushangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo.

Awajibu wanaomponda
"Uzoefu ni mazoea ya starehe. Mtu aliyekaa katika uongozi ni mtu aliyesahau shida za Watanzania.

Jambo la kwanza na la msingi ni kuitambua ajenda ya Watanzania, Watanzania watamuunga mkono kiongozi kwa kuitambua ajenda yake," alisema.

Alisema wakati akijitathimini kutangaza nia ya kugombea alikuwa akifahamu ajenda ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa umaskini hakuusoma katika vitabu, bali amekulia katika maisha ya kimaskini.

"Ukizungumzia ukosefu wa ajira na dawa hospitali hilo sijalisoma vitabuni, ukizungumzia ajira kwa vijana na watu wote hilo jambo sijalisoma vitabuni."

Alisema katika pitapita zake, amesikia habari za mtu anayefaa kuwa rais zikihusishwa na umri na uzoefu, "Ujana na uzee haviwezi kuwa sifa ya kuiongoza nchi. Kukaa serikalini muda mrefu haiwezi kuwa sifa ya kutosha kuliongoza Taifa hili, unaweza ukakaa sana serikalini lakini ukasababisha hasara kubwa.

Hata kuishi ni hivyohivyo, kinachoangaliwa si kuishi miaka mingi, bali ni kipi ulichokifanya. Leo hii marehemu (Edward) Sokoine hakumbukwi kwa sababu alikaa sana serikalini, anakumbukwa kwa matendo yake kwa kipindi kifupi alichokaa serikalini."

Huku akishangiliwa alisema, "Kiongozi akipatikana kwa mazoea atafanya kazi kwa mazoea. Vita ya kwanza tunayotaka kuikomesha katika nchi yetu ni kufanya kazi wa mazoea. Tunahitaji mambo matatu; mabadiliko, mbinu za kufanya mabadiliko na utayari wa kufanya mabadiliko."

Kuhusu umri alisema: "Wengine wanaongelea umri wamesahau kuwa Katiba inasema umri wa kugombea ni miaka 40, hata vitabu vitukufu vimeandika kwamba umri wa miaka 40 ni sahihi mtu kupewa utume na unabii, Mussa alipofikisha miaka 40 aliaminiwa kwenda kuwakomboa ndugu zake."

Alisema hata Mwalimu Julius Nyerere alikuwa rais akiwa na miaka 40, tena akitoka kufundisha sekondari.
"Watu wanataka kuwatoa Watanzania katika ajenda kwa kuzungumzia vitu vyepesi. Eti wanasema ukimaliza kuwa rais wakati bado kijana utafanya nini. Nifanye nini tena wakati nitakuwa nimeshamaliza kazi. Najipambanua kwa ajenda yangu na wale watakaoniangalia wataangalia ajenda yangu," alisema.

Mipango yake
"Kwa miaka 50 tumekuwa tegemezi, sasa imetosha tunakwenda kujitegemea. Kujitegemea ni kila mmoja kulipa kodi anayostahili," alisema.

Alisema wakati wa watu wachache kubeba mzigo wa kodi umefikia mwisho na kwamba kila mtu anayestahili kulipa atailipa, awe mdogo au mkubwa.

"Tunakwenda kuachana na utaratibu wa kukimbizana na wauza vitumbua kuwadai kodi. Kujitegemea ni nidhamu ya matumizi na sasa tunakwenda kuziba mianya ya rushwa," alisema.

Alisema ili uchumi umilikiwe na Watanzania wenyewe, lazima njia za kuwapatia watu kipato ziboreshwe kwa sababu uchumi wa nchi unakua lakini wananchi bado wanalia umaskini.

"Njia ya kuwatoa hapo walipo ni kuongeza thamani ya mazao na kazi wanazozifanya kwa sababu asilimia 70 ya Watanzania ni wakulima. Lazima wakulima watafutiwe pembejeo na masoko. Tunatakiwa kutumia sekta binafsi ili kuwa na viwanda vingi nchini," alisema na kutoa mfano:

"Pamba ya Tanzania inaweza kutumika kutengeneza sare za shule, za jeshi na viatu kutoka katika viwanda vilivyopo nchini. Tuna wanafunzi zaidi ya milioni nane na kila mwaka wanaandikishwa shule, kwa nini tulilie soko la nje halafu sare zao tunanunua nje."

Kuhusu mafuta, Nchemba alisema kilimo cha alizeti kikiboreshwa kitazalisha ajira nyingi na hilo linaweza kufanyika pia katika sukari, kahawa, chai na korosho.

"Awamu ya tano, nchi itaingia katika uchumi wa viwanda na vijana watafanya kazi kwa kupokezana," alisema.

Mwigulu aligusia suala la Watanzania kutozwa kodi zisizokuwa na kichwa wala miguu na zisizoendana na uzalishaji wa biashara husika, huku akitolea mfano mama ntilie na wamachinga.

"Wakubwa wakitaka kuwekeza wanapewa likizo ya miaka 10 ya kulipa kodi lakini anayefungua saluni anatozwa kodi wakati akiwa anapaka rangi jengo hata biashara hajaanza," alisema na kushangiliwa.
Rushwa.

Akizungumzia rushwa alisema: "Rushwa hupofusha macho ya wenye akili na kurejesha nyuma maendeleo na hupindisha ukweli na kuwanyima haki maskini."

Alisema awamu zote nne za Serikali zimejitahidi kupambana na rushwa, ila awamu ya tano itakuja na njia tofauti kwamba atakayethibitika kupokea au kutoa rushwa atachukuliwa hatua haraka ili iwe fundisho.

"Sasa hivi mtu akikamatwa na rushwa kesi zimekuwa na mlolongo mrefu. Tutabadilisha Sheria namba 11 ya Kupambana na Rushwa ili kuipa meno Takukuru iweze kushughulika na suala hili na atakayebainika atafilisiwa, kufukuzwa kazi na kufungwa," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • 20150531_161615.jpg
    20150531_161615.jpg
    20.5 KB · Views: 3,782
Mwigulu Nchemba Leo anatarajia kutangaza nia ya Urais katika ukumbi wa Nyerere hall chuo cha Mipango Dodoma, nitakuwa natoa updates kwa kinacho endelea kwenye ukumbi huu wa Nyerere hall chuo cha Mipango.
 
Naona hii sasa imekuwa ndio fashion na utamaduni kwa wana-CCM wanaosaka uraisi.

Muda huu ninapoandika kuna magari aina ya coaster yamekodishwa ili kubeba wanafunzi wa chuo kikuu na kuwapeleka Chuo cha Mipango Dodoma kwenye tukio la Mwigulu kutangaza nia.

Nasikitika kuona hata wanafunzi wa vyuo vikuu nao hawajitambua!

Binafsi nimebaki naangali tu tukio hili nikiwa kwenye gate kubwa la kuingilia na kutoka hapa chuoni.
 
Kakodi mengi sana kwa kweli naona yamejaa hapa UDOM na wanafunzi wanazidi kumiminika kuingia kwenye gari.

Nchi hii ni shidaaaaa!!!!!
 
mkuu na wewe si uko hiko chuo tunategemea update kutoka kwako
 
Karibu sana mwigulu.ila Mimi naamini unajitengenezea crblty kwa ajili ya baadae.ki ukweli kwa sasa uwezi unamabifu.ya ajabu AF kama dikteta flan.ila unafanya Sana'a yako vizuri.keep it up...
 
Naona hii sasa imekuwa ndio fashion na utamaduni kwa wana-CCM wanaosaka uraisi.

Muda huu ninapoandika kuna magari aina ya coaster yamekodishwa ili kubeba wanafunzi wa chuo kikuu na kuwapeleka Chuo cha Mipango Dodoma kwenye tukio la Mwigulu kutangaza nia.

Nasikitika kuona hata wanafunzi wa vyuo vikuu nao hawajitambua!

Binafsi nimebaki naangali tu tukio hili nikiwa kwenye gate kubwa la kuingilia na kutoka hapa chuoni.

Mkuu hapo ndo utajua ni kwa kiasi gani wasomi wa Tanzania wanavyotumika kuzuia mabadiliko ya kweli kwenye nchi hii
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom