Jomse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 275
- 92
Ninachukua fursa hii kumshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha leo tarehe 19/8 tumetimiza miaka 15 ya ndoa yetu. Tumebarikiwa kupata watoto 5. Tumepitia misukosuko na dhoruba nyingi sana lakin ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka leo bado tupo pamoja. Katika miaka hii kumi na tano nimejifunza kuwa Safari ya ndoa ni kama alivyoimba Maneti ina papa na nyangumi kibao lakini ukimshirikisha Mungu mnasonga mbele. Ningeyaandika mengi sana lakini sipendi kuwachosha.