Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake

Testar

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,461
12,214
Mtu alimuumba Mungu katika fikra zake ili awe kielelezo cha mambo yote yaliyokosa majibu kwa upeo wa watu.
Mungu alipewa sifa zote za kiutu kama vile huruma, chuki, upendo, ukatili, hasira, wivu, majuto, ushindani n.k.
Kutokana na sifa ya ushindani kuwa ni kipimo cha nguvu za Mungu, mtu alimuumbia Mungu mshindani, naye ameitwa Shetani.Mtu akajijengea imani kuwa matendo yote anayoyatenda anongozwa na Mungu iwapo ni mema au na Shetani iwapo ni mabaya.

Mungu na Shetani sii vitu halisi bali ni 'Idea' za watu.Mungu na Shetani hawajawahi kuonekana, kusikika, kuhisika, ama kushikika popote.
Idea ya uwepo wa Mungu imekuwa ikirithishwa kwa watu [Theists] wakiwa kwenye umri mdogo zaidi na kwa vitisho vya ya kwamba kama wasipomwamini Mungu basi wataishi maisha ya tabu pamoja na kuingia kwenye moto wa milele watakapokufa[Hakuna uthibitisho hata chembe wa kuwepo kwa hivyo vitisho].

Kutokana na watu mbalimbali kujitengenezea picha tofauti kwenye fikra zao juu ya Mungu, yameibuka makundi mbalimbali ya watu wenye mitazamo tofauti juu ya sifa za Mungu, sheria zake pamoja na mapenzi yake kwa watu. Makundi hayo ni dini na madhehebu yasiyo na idadi yanayodai kumwamini Mungu mmoja lakini jambo la kushangaza huyo Mungu ana waongoza watu kwa utofauti mkubwa sana.Hizo dini na madhehebu yake zimekuwa zikihubiri sifa chanya za Mungu na hasi za Shetani ambazo haziendani na uhalisia.

Idea ya uwepo wa Mungu na Shetani imekuwa ikiaminishwa kwa watu badala ya kueleweshwa hivyo kukosekana kwa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mungu pamoja na mpinzani wake Shetani.
Pindi mahojiano juu ya uwepo wa Mungu yanapoibuka, Mungu hutetewa na watu badala ya kujitetea mwenyewe.

Mungu na Shetani sii halisi[kweli] bali ni fikra za watu ambazo hazina uhalisia wowote.
Nje ya fikra za watu hakuna Mungu wala Shetani..........Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake.
 
Naona shibe ndo inakusumbua wewe, ni kufuru mbaya kupindukia unaposema eti hakuna Mungu na Kwa dharau zaidi unasema eti Mungu aliumbwa na binadamu.
Kama umekosa mada bora ukae kimya vinginevyo huu mwaka huwezi kuumaliza, Utakufa.
 
akuna kutubu kwa sababu kutubu pia kumezushwa tu na hao, hao waliozusha vitu ambavyo havipo, labda nisisitize tu HAKUNA MUNGU, SHETANI, IBILISI, WALA MOTO UWE WA GESI, KIBIRITI, KUNI PETROLI WALA WA KUCHEMSHIA CHAI.
I concur with you brother, asipotubu hakika adhab yake ni moto wa Jehanam
 
Naona shibe ndo inakusumbua wewe, ni kufuru mbaya kupindukia unaposema eti hakuna Mungu na Kwa dharau zaidi unasema eti Mungu aliumbwa na binadamu.
Kama umekosa mada bora ukae kimya vinginevyo huu mwaka huwezi kuumaliza, Utakufa.
Kama ambavyo huna uhakika juu ya shibe ama njaa kwangu, ndivyo usivyo na uhakika juu ya uwepo au kutokuwepo kwa Mungu.
Tangu nikiwa mdogo watu walinitabiria kifo.Kuna watabiri wengi walikufa wakisubiri kifo changu kitokee.
Nyie ambao mna guarantee ya immortality endeleeni kututabiria kifo lakini mkae mkijua kifo ni haki ya kila kilicho hai.
 
akuna kutubu kwa sababu kutubu pia kumezushwa tu na hao, hao waliozusha vitu ambavyo havipo, labda nisisitize tu HAKUNA MUNGU, SHETANI, IBILISI, WALA MOTO UWE WA GESI, KIBIRITI, KUNI PETROLI WALA WA KUCHEMSHIA CHAI.
Sawa kabisa Mkuu.......Mimi ningependa kujua kwakuwa Mungu na Shetani ni roho, ilikuwaje wakaingia kwenye ulimwengu wa kifizikia.
 
Mleta hoja umeleta vizuri maana umeweka na ushahidi wa shaka yako juu ya uwepo wa Mungu. Wajibuji hatupaswi kukutisha bali tukujibu kwa ushahidi ulio wazi. Niseme tu kwa ufupi, In vigumu kuthibitisha uwepo wa Mungu lakini nivigumu zaidi kuthibitisha kutokuwepo kwake, tunachoweza kuonesha uwepo wa Mungu ni kutaja maumbile, kanuni na mienendo iliyopo ambayo sio kazi ya mikono ya Mtu.
 
50 Reactions
Reply
Back
Top Bottom