sasa mshaharaa wa quantity surveyor utafananishaa na huo wa real estate! Alafu co wote wanaotaka kuajiriwaa ndugu wengine wana uwezo wa kujiajiri.! So ndugu uciwe na mawazo hasi kwa wenzako..!
NB; ARDHI ULIHAMIA NINI COZ KUNA THREAD MOJA HUKO NYUMA ULICHANGIA KWAMBA UMESOMA UDSM., NASHINDWA KUI-ATTACH HAPA COZ NATUMIA CIMU.! SO MKUU FAFANUA KIDOGO..! MWANA ARU MWENZANGU
Kipindi ambacho naanza chuo hakukuwa na Ardhi, kulikuwa na UCLAS - UDSM, na wengi wetu tulikuwa tukiishi mabibo hostel pamoja na wanafanzi wa MUCHS kwa sasa MUHAS. Nadhani hapa umenielewa.
Kuhusu Real estate, ndio maana nimesema ni vyema kuuliza ili ujifunze uwe nondo kuliko ku-speculate mambo.
Real estate inahusisha taaluma zote za ardhi, yani kila taaluma ipo humo (kasoro BAF). Unaposema real estate una maanisha uwekezaji kwenye ardhi (yaani kuendeleza ardhi kutoka kwenye utupu na kuiwekea jengo).
Kabla ujenzi haujafanyika, ni lazima tafiti ifanyike ili kujua kama ujenzi huo ni potential na una tija (kama ni kwa ajili ya "property investment"). Kazi ambazo hufanywa na mashirika ya kijamii yote nchini, Wakala wa ujenzi wa serikali TBA, makampuni binafsi pamoja na shirika la nyumba la taifa NHC. Hawa wote wana jenga kwa ajili ya kupata faida kutokana na ujenzi huo (Propepty investment).
Ni nani anaefanya tafiti na kupendekeza kuwa mradi utalipa?, si mwingine, bali ni Real estate investment analyst (uwa tunaitwa consultants), na tafiti zetu uitwa Feasibility Studies. Hivyo uchambuzi wote wa jinsi jengo linalo tarajiwa kujengwa upo humo kwenye feasibility study. Gharama za kufanya utafiti utolewa na client, sisi ni kula pesa tu.
Wapi anakuja QS?
QS anakuja pale ambapo gharama halisi za ujenzi zinapo hitajika (bill of quantities), na hii ina msaada kwa client kwani ma-contractor uwa wanazidisha gharama za ujenzi, hivyo hawa QS ni muhimu ku-verify costs kama ni za kweli au zimezidishwa, huku uwa wanalipwa 10% of the construction costs ambayo ina mjumlisha yeye QS, ENGINEER na ARCHTECT au kwa pamoja tunaita professional fees.
Hivyo, kuhusu nani anakula pesa, nadhani jibu utakuwa umepata, feasibility study ni tafiti (minimum it consumes 7 days, hivyo hizo per diem zake ni kula kuku tu). Kijana, suala la mkwanja usiliseme kabisaaa, unajua kwanini nimejipa jina la Billion?! Sio show off.