Hapa, Waziri Mkuu Majaliwa anakosea sana

Hapa, Waziri Mkuu Majaliwa anakosea sana

Waziri Mkuu hajakosea. kazi yake ni kusimamia maamuzi ya serikali. Kama serikali imeamua kuhamia Dodoma immediately, unataka Waziri Mkuu afanye nini? leave him alone, he is just doing his job.

Mkuu, nimesoma humu kuwa JPM amesema hili zoezi likamilike baada ya miaka minne. Sasa kulikoni amri ya miezi miwili?
 
Hii nchi bila mitulunga haiendi;
na iwapo JPM atafeli kuhamia Dodoma ndo mwisho
hakuna kiongozi atakayekuja mwenye udhubutu tena;

Twendeni Dodoma, hata Yerusalemu haikujengwa siku moja.
 
Mkuu, nimesoma humu kuwa JPM amesema hili zoezi likamilike baada ya miaka minne. Sasa kulikoni amri ya miezi miwili?

Nimekupata Mkuu. Lakini Waziri Mkuu hajasema wakianza kuhama mwezi wa 9 watamaliza kuhama mwezi wa 9 au wa 10. Bado watachukua muda mrefu sana kuhamisha wizara na watumishi wote. Kwa hiyo nafikiri tunamhukumu bila sababu.
 
Serikali kuhamia Dodoma ni habari nzuri sana kwa wakazi wa Dar. Peleka Serikali Dodoma haraka...
 
Nimekupata Mkuu. Lakini Waziri Mkuu hajasema wakianza kuhama mwezi wa 9 watamaliza kuhama mwezi wa 9 au wa 10. Bado watachukua muda mrefu sana kuhamisha wizara na watumishi wote. Kwa hiyo nafikiri tunamhukumu bila sababu.

Inawezekana. Kama ni hivyo yeye si anajua Kiswahili? Kwa nini asitoe maagizo kwa namna inayoeleweka? Hivi unajua mkanganyiko uliopo katika Wizara kwa sababu ya hiyo amri yake? Ina maana hana taarifa za mkanganyiko huo ili autolee maelezo?

Yeye ameshindwa nini kusema waanze mawaziri, na wakurugenzi na makamishina nk, kisha wengine wafuate katika kipind cha miaka minne ijayo, na labda makatibu wakuu wabaki kwanza?

Hata hivyo, kuhamisha vipengele pengele vya wizara ni kuleta usumbufu usio na maana. Yeye angesema kwa namna aliyosema JPM, kwamba katika kipndi cha miaka minne kila Wizara iwe imehamia Dodoma, kuanzia labda mwaka kesho, na Wizara ziniletee uratatibu utakaoonyesha jinsi gani watakuwa wamehama kabisa ndani ya miaka minne, kama alivyoelekeza raisi.

Na bado hajatueleza kuna mpango gani wa kuhamisha ofisi za balozi. Maana huwezi kuhamisha serikali ukaacha ofisi za balozi nyuma.

Leo hii utawaambiaje Ubalozi wa Marekani hameni ndani ya miezi miwili? Viwanja vya ofisi za ubalozi vilishatolewa? Je waliishahimizwa kujenga ofisi za Ubalozi Dodoma?

Kwanza kwa jinsi bado Dar ni centre of business, ilibidi kwanza waimarishe usafiri wa treni kati ya Dar na Dodoma, na hata kuweka treni za mwendo kasi. Hivi unajua serikali ikihamia Dodoma tuliopo Dar tutakuwa tunaenda Dodoma ku-apply for visa? Umefikiria congestion itakayokuwapo barabara ya kwenda Dodoma? Mabasi yetu ndio haya, yanaendeshwa kwa mbwembwe na kuchinja watu kila siku!
 
“It always seems impossible until it's done’’― Nelson Mandela.

Sisi tumezoea sana porojo kiasi kwamba hata mtu akiwa serious tunadhani ni porojo.

Madawati tu kwenye shule zetu ilikuwa ni porojo kwa muda mrefu na hata Rais Magufuli aliposema suala la uhaba wa madawati lazima tulimalize kwa muda mfupi, kuna wengine walidhani ni porojo zile zile za miaka mingi.

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!
The difference between the two is yawning.
It seems the last sentence best fits you.
 
mkuu ye si amesema atahamia dodoma na mawaziri na wizara zitafuata
Sasa mawaziri watakuwa wanafanyaje kazi bila wataalam. Au kwa video conferences.
Ukurupukaji at its best.
 
Nani amekuambia ofisi zote zitahamia Dodoma ndani ya miezi miwili?

Rais amesema zoezi litachukua miaka minne kuanzia alipozungumza.
Nimejiridhisha pasi na shaka ya kwamba MsemajiUkweli ni taahira! Tafuta h0tuba ya PM usikilize ndo uje hapa ubwabwaje, yeye kasema wizara zote ziwe zimehamia ifikapo Septemba. Huku ni kukurupuka kwa nini wasifanye kwa awamu? Kwa mfano mkasema kwa uchache ifikapo Desemba wizara 2 ziwe zimehamia Dodoma? Hili likawa zoezi la kila mwaka! Hapa kukurupuka tu!!
 
1. Kutokua au kutoheshimu vipaumbele katika utekelezaji wa mipanga ya serikali.
2. Kutojali utaalamu au professionalism katika uendeshaji......wanasiasa wa serikali hii wanadhani wanajua kila kitu.
3. Wasaidizi wa mkuu hawana au awapewi nafasi ya kutoa michango yao so ili walinde ajira wameamua kufanya kila kitu mkuu anachotaka. Naamini chini ya kapeti huwa wanacheka sana.
4. Filosofia inayoongoza nchi sio " KAZI" ila kujionesha kuwa unafanya kazi ivyo wajihusisha zaidi na matukio ya kumake headlines ata kama tija yake ni ndogo.
 
Sio kila kitu ukosoe....... Kwan Suala la kuhamia dodoma limeanza jana au leoo? Tangu wameambiwa wahamie dodoma walijiandaaje toka miaka hiyoo? Hiyoo miez miwil ni mingi maana Suala la kuhamia dodoma ni la miaka ming nyuma tatzo watz ni wazito katika ku focus future [emoji326] na utekelezaji wetu mpaka tusukumwe mm naona ni sahihi awasukume hivyo hivyo la sivyoo issue ya kuhamia dodoma itabak maneno na stori...... Mambo uliosema ni ya msingi na yalitakiwa yafanyiwe kazi since tamko la kuhamia dodoma limetamkwa.....
 
tangu magufuli atangaze suala la madawati ni miezi mingapi? na mpaka leo bado. kisha compare suala la madawati na suala la kuhamisha ofisi zote ndani ya miezi miwili. kujenga ofisi tu, hiyo miezi miwili sio chochote!
Wanataka kutuambia wananchi tuchangie Gharama za serikali kuhamia Dodoma kama tulivyochangia madawati. Halafu tunaitwa watu maskini na hohehahe. Tutayaona yatakayojitokeza halafu tutaongeza muda. Kwani nani wa kuuliza? Kuna mwenye swali?
 
Waziri Mkuu ametoa amri kwamba katika kipendi cha miezi miwili serikali yote iwe imehamia Dodoma.

Japokuwa suala la kuhamia Dodoma limekuwa la muda mrefu, lakini kutoa miezi miwili Wizara ziwe zimehama ni kufanya kazi kutumia nguvu ya siasa badala ya lojiki (lack of rational thinking), hasa ukizingatia mambo yafuatayo;
  • kuhamishia serikali Dodoma ni zaidi ya waziri na katibu mkuu (ambao wengi wana nyumba tayari Dodoma) kuhamia Dodoma. Wizara ni watu
  • kuhamishia serikali Dodoma inatia ndani kuhamishia ofisi zote za ubalozi kwenda Dodoma (je nao unawapa miezi miwili?)
  • kuna suala la kupata majengo na vyumba vya ofisi kwa wafanya kazi
  • kuna suala la malipo ya kuhamisha wafanya kazi na vyombo vyao
  • kuna suala la kuhamisha furniture, computer za ofisini toka Dar kwenda Dodoma
  • kuna suala la kusuka mfumo wa mawasiliano katika ofisi mpya huko Dodoma
  • kuna suala la wafanyakazi kupata sehemu za kukaa huko Dodoma
  • kuna suala la kutatua mambo yanayohusu familia, kama mke au mume ndie anaehama, au kama mke na mume wote ni wafanya kazi hapa Dar wataathiriwaje na kuhama huku
  • kuna suala la watoto wa wafanyakazi hawa walioko mashuleni hapa Dar kuhamia Dodoma
  • kuna suala la baadhi ya familia kutatua suala la nyumba zao watakazoziacha Dar
  • kuna suala la kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu kuhama badala ya kuwahamisha kama vile tuko kwenye state of emergency
  • kuna suala la kuimarisha usafiri wa treni kati ya Dodoma na Dar, ikiwezekana treni za kwenda kasi, kwa kuwa Dar bado itabaki kuwa centre of business na kutakuwa na safari nyingi sana kati ya Dodoma na Dar. Hata viza za kusafiria tutafuata Dodoma. Kufikiria kwamba tutatumia barabara ya Dodoma kama ilivyo ni kuamua kuua watanzania huenda mamia kila mwezi - madereva wetu wa mabasi tunawafahamu - kichaa kapewa rungu. Barabara hii ilishatuulia waziri mkuu, Sokoine.
  • nk
Ukizingatia mambo kama hayo hapo juu, utaona wazi kwamba Waziri Mkuu alitakiwa kutoa miezi kwa kiwango cha chini kabisa, sita, ili kuwe na maandalizi yenye utaratibu ili watu weze kuhama kwa mpangilio, na sio kuhamisha watu kama vile kupeleka kikosi cha jeshi mpakani baada ya kuvamiwa na nchi jirani. Hivi viongozi wetu huwa hawayaoni haya wanapotoa amri? Nashangaa sana awamu ya tano ya uongozi wa Tanzania imejaa amri ambazo zinatolewa kushoto, kulia na katikati bila kufanyiwa tafakari za kina. Hivi kweli hiyo ndiyo filosofia ya "Hapa Kazi Tu"?

Na cha ajabu, Waziri Mkuu anasema kwamba "hatuchezi mchezo wa siasa hapa, tutapitisha sheria katika Bunge mwezi Septemba kufanya suala la kuhamia Dodoma liwe rasmi" (we are not playing politics here...we will pass legislation in parliament in September to make the move to Dodoma official)

Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, kama sheria itafikishwa Bungeni Septemba, siku zote hizi suala la kuhamia Dodoma halikuwa rasmi? Na kama sheria ya kuhamia Dodoma itapelekwa Bungeni Septemba, kwa nini Waziri Mkuu anatoa amri juu ya jambo ambalo bado si rasmi kisheria?

Hivi kwa nini viongozi wetu wanadhani kila jambo linahitaji amri kama za kijeshi ili litekelezwe? Je, kutoa amri bila kufikiria athari za kisosholojia na kiuchumi (socio-economic impacts) sio ubwana ambao tuliupinga kwa muda mrefu sana? Frankly, I was expecting much better from my prime minister than this kind of reckless leadership style.

Ushauri wa bure kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni kwamba nguzo na nguvu ya taifa lolote iko katika muungano wa kifamilia. Unapovunja familia unavunja nguvu ya taifa. Huko nyuma empire ya Roma ilivunjika kwa sababu ya mvunjiko wa kifamilia. Kwa hiyo hili suala linahitaji utaratibu mzuri, gradual relocation implementation labda katika kipindi cha mwaka mzima, likifanyika kwa kuhamisha wafanya kazi katika kila wizara kwa awamu kulingana na impact zao katika kuendesha Wizara. Sio kuwaambia watu funga virago ondoka nenda Dodoma haraka. La sivyo utaona barua nyingi za kujiuzuru kazi au hata mivunjiko katika familia. Na watu wa ubalozi je, au umeamua serikali yote itakuwa Dodoma na wao wabaki Dar?

Na vyama vya wafanyakazi iweje viko kimya katika hili?
Mleta mada umesema mheshimiwa anakosea "hapa" kwani ameshawahi kupatia wapi? Sirikali ya "wakurupukaji" na "mizuka"!
 
Sio kila kitu ukosoe....... Kwan Suala la kuhamia dodoma limeanza jana au leoo? Tangu wameambiwa wahamie dodoma walijiandaaje toka miaka hiyoo? Hiyoo miez miwil ni mingi maana Suala la kuhamia dodoma ni la miaka ming nyuma tatzo watz ni wazito katika ku focus future [emoji326] na utekelezaji wetu mpaka tusukumwe mm naona ni sahihi awasukume hivyo hivyo la sivyoo issue ya kuhamia dodoma itabak maneno na stori...... Mambo uliosema ni ya msingi na yalitakiwa yafanyiwe kazi since tamko la kuhamia dodoma limetamkwa.....

Hivi Mkuu unaposema tangu waambiwe wahamie Dodoma walijiandaaje toka miaka hiyo unamaanisha nani hasa? Hawa watendaji wakuu wa kila wizara, kama mawaziri, walikuwapo wakati huo? Kwa nini tunawasema kama vile wao ndio wamesababisha hili kutotendeka? Au unawalaumu hawa wafanyakazi wa kawaida waliokaa miaka zaidi ya ishirini katika wizara kwamba kwa nini hawakuhamia Dodoma?

Kwani Raisi Magufuli alipokuwa waziri mbona hatukusikia anahamisha wizara yake kwenda Dodoma? Ina maana Mkapa na JK walimkatalia?

Basi kawalaumu maraisi na ma-PM waliopita. Lakini kuwashupalia watendaji wa wizara waliopo sasa juu ya suala la kuhamia Dodoma ni sawa na mbwa mwitu aliemwambia mwanakondoo wa miezi miwili kuwa atamla kwa kuwa mwaka juzi alimtukana!
 
Samahani sikujua kama nazungumza na MTU mjinga kiasi hiki. Hujui kabisa serikali nini na inafanyaje kazi. Mwee...

Hujamuelewa...ana maanisha mawaziri wetu wengi wanawa-ignore watalaamu katika wizara na wao kufanya maamuzi bila maelekezo ya wataalamu kama vile wao ndio wanajua kila kitu. Utakuta waziri anaagiza pantoni au ndege bila ushauri wa wataalamu.
 
Nyie pingeni tu lakini serikali itahamia Dodoma mpendemsipende,Raid kaza Uzi hapo hapo kuna watu humu wanapata faida kubwa kwa serikali kubaki Dar tena wachache,wanamiradi yao inategemea serikali,allowance zao za safari ya Dodoma kila panapokuwepo shughuli za kiserikali Dodoma,upuuzi huu wa kuwanyima huduma watanzania walio wengi huduma kuwa karibu yao hatuwezi kufanya awamu ya tano
 
Nahayo
Tafta vitu vya kulinganisha na wala sio hilo, je shule za Dodoma zimeongeza madarasa mangapi kwa kila shule kwa mwaka huu? au unadhani watoto watakaohamia uko watasoma vipi ? Nyumba za kupanga nazo vipi? hii ni kutaka kuongeza ugumu wa maisha kwa watumishi wa umma na kwa kifupi ni aina flani ya UKATILI
Nahayo ndio maamuzi magumu sio ya hiyo Lowasa wenu,Tunachoangalia ni idadi ya wanaofaidika na kuhamia Dodoma ni wa ngapi watapata huduma karibu,sio nyie wa Dar ni biashara zenu zinazotegemea mteja serikali muwe wabunifu.
 
Hii nchi haiwezi enda mbele bila nguvu ya ziada ya kiongozi na kufanya maamuzi bila kumsikiliza MTU Watanzania kila kitu wanajifanya wajuaji na kuja na vitheory vya ilimradi kumvunja Moyo kiongozi,wengi wanaotetea serikali kubaki Dar niwalewale wenye masirahi na serikali kubaki Dar yaani wajanjawajanja wa Dar.haiwezekani tunaangalia watanzania walio wengi wapate huduma karibu.
 
Back
Top Bottom