Hapa, Waziri Mkuu Majaliwa anakosea sana

Mkuu kama unaelewa Kingereza soma hapa chini; IPPMedia. Na hata kama amesema key government functions, niambie zipi kati ya government functions sio key? Azitaje basi tujue kuna watu au wizara zinatakiwa kupunguzwa kwa sabu sio za msingi (key) ilii tubane matumizi. Wengine tunachoelewa ni kwamba all government functions are key.

View attachment 371917
Tuache uvivu. ..maneno mengi miaka 42... ukisoma MITHALI 26:13. ...kila siku ni sababu tu...
 
“It always seems impossible until it's done’’― Nelson Mandela.

Sisi tumezoea sana porojo kiasi kwamba hata mtu akiwa serious tunadhani ni porojo.

Madawati tu kwenye shule zetu ilikuwa ni porojo kwa muda mrefu na hata Rais Magufuli aliposema suala la uhaba wa madawati lazima tulimalize kwa muda mfupi, kuna wengine walidhani ni porojo zile zile za miaka mingi.

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!

1. Kwanza, binafsi sikumbuki kama hili lililkuwa hata kama liliwekewa mkakati maalumu wa kibajeti ingalau ktk bunge la bajeti lililomalizika mwezi juni!

2. Pili, huu ni mpango ambao uko kwa takribani ya zaidi ya miaka 40 na ulishindikana. I don't know sbb ni nini hasa. Labda ni utashi wa kisiasa tu ulikosekana kuanzia enzi za Nyerere, Mwinyi, Ben Mkapa na JK......

Huyu jamaa from no where, toka kichakani tu anatutangazia kuwa serikali nzima sasa ihamie Dodoma na PM naye from no where anasema by september, serikali ndiyo itapeleka mswaada bungeni.......

Hofu yangu si nyingine bali kuna viashiria vyote vya kushindwa kwa hii plan, lakini pia ni kuvurugika kwa mambo mengi......
 
Waende Dodoma aisee...we have lost enough already by continuing being in Dar. Tanzania inatakiwa ikue sio kudumaa sehemu moja.
Sawa, ila kimikakati ndugu... sio kukurupuka bila kufikiria impact ya jambo lenyewe.
 
“It always seems impossible until it's done’’― Nelson Mandela.

Sisi tumezoea sana porojo kiasi kwamba hata mtu akiwa serious tunadhani ni porojo.

Madawati tu kwenye shule zetu ilikuwa ni porojo kwa muda mrefu na hata Rais Magufuli aliposema suala la uhaba wa madawati lazima tulimalize kwa muda mfupi, kuna wengine walidhani ni porojo zile zile za miaka mingi.

He who knows not and knows not that he knows not is a fool!
Aweke salary slips zake hadharani kama alivyoahidi....la sivyo atakuwa mzee wa porojo
 
TUNA IMANI NA LOWASSA OYAAA OYAAA OYAAAA UKIONA ILE VIDEO NDIO UTAMJUA HUYU WMKUU KAMA NAE NI YES SIR. EXPECT NOTHING BRO
 
Serikali iliyopita iliwekeza sana kwenye infrastricture.... je mnajua kwamba kuna MDA 72 zimeunganishwa kwenye network moja inajulikana kama serikali mtandao (govt network) na taasisi hizo baadhi zikiwa zimekarabatiwa LAN zake pamoja na VoIP mradi huu ni mkopo wa WB. Je unapata tafsiri gani hapo? Je serikali itakopa tena kwa ajili ya kulay down infrastructure nyingine dodoma???
 
Kuhamia Dodoma kwa Wizara zote na wafanyakazi wao,na vitengo vyote ni bajeti nene sana na ya kutisha!
Bajeti gani ilitenga pesa hizi za kuhamia Dodoma?
Hawa watu wanakurupuka tu
Aibu sana jamani!
 
Ccm wamgehamia wao huko dodoma wasihangaishe nchi ma uchumi...
Kwanza tangazo lile ni batili limetangazwa kwenye mkutano wa ccm na walengwa ni ccm.
Hivyo ccm hameni tu makao yenu.
Dodoma haiwezi kuhudumia ukuaji wa mji.
Vumbi tupu
Maji shida
Maginjwa ya mscho yaso isha
Ukame hata mboga kupanda mtihani
Hakuna maji.
Mji hauko ready
Hakuna chochote cha kuvutia
Kama DART ilichukua miaka 12 tusidanganyane
Hakuna airport
Kati ya nchi sio issue
London haiko kati
Washington haiko kati
Cairo haiko kati
Otawa haiko kati
Pretoria haiko kati
Kampala haiko kati
Delhi haiko kati
Tokyo haiko kati
Tunis haiko kati
Algers haiko kati
Tripol haiko kati
Beirut haiko kati.
Wazungu walifanya upembuzi yakinifu na kuweka Dar ndio capital..hawakukosea
Tuache kuhangaika.. tuwekeze nguvu katika uchumi wetu na elimu.
Hakuna balozi yupo tayari kwa sasa kwenda didoma wakati wameshajenga Dar...
 
Ukiona kuhama ni vigumu si ubaki wakati wenzio wanahama
 
Kwanini dodoma kwanini basi wasijenge hizi wizara karibu kila mkoa na hawa watu au wafanyakazi wasirundikane huko dodoma,Tz bado ina maeneo wanataka wai promo tena Dodoma baada ya miaka kadhaa tena kuwe na maongamano kama Dar
 
hahaha!!! ila viwanja vitapanda bei sana asee, waliowahi wameula ila watakaoenda sasa itakuwa noma! inanikumbushia mtwara wakati wa vuguvugu la gesi. viwanja vilipanda bei kuliko dar. halafu hamna kitu mpaka leo
Mkuu, si ndio biashara? Lazima ukubali ku risk sometimes; unaweza ukajenga na ukafanikiwa lakini pia unaweza kujenga na IKALA kwako ingawa umenifurahisha sana na historia ya Mtwara kaka!
 
Huyu waziri sindiyo alitoa amri ya sukari isiuzwe zaidi ya 1800/= na mpaka sasa inauzwa 2800/=! Simshangai kutoa amri hyo lkn utekelezaji ni 0%
 
Ukijiona wewe kwenye nafasi yako ya kazi huna mtu wa kumtumbua kama jipu basi ujue wewe sio key function na ofisi yako itakuwa ofisi ya kata kifunction sie tukienda dodoma

Hapana Mkuu. Government functions ni neno la ujumla zaidi, akimaanisha wizara au idara au taasisi ya serikali, sio kazi moja moja. Kwa hiyo kwa kusema only key government functions ziende Dodoma, ana maana kuna idara, au tasisi au wizara nyingine sio muhimu sana kwenda Dodoma. Ndio maana nikasema atutajie ni zipi kati ya government functions anaona sio key functions - yaani wapo wapo tu kama wafanyakazi hewa, hata wasipokuwapo halitaharibika neno!
 
Huyu waziri sindiyo alitoa amri ya sukari isiuzwe zaidi ya 1800/= na mpaka sasa inauzwa 2800/=! Simshangai kutoa amri hyo lkn utekelezaji ni 0%

Hahaha! Kama anapenda kutoa amri amri ajiunge nasi kure ndani ya jesi, kure hakuna kuraramika, kuria ria wara kurara rara, ni amri moja tu mura, unarara mbere.
 
Waziri Mkuu ametoa amri kwamba katika kipendi cha miezi miwili serikali yote iwe imehamia Dodoma.

Japokuwa suala la kuhamia Dodoma limekuwa la muda mrefu, lakini kutoa miezi miwili Wizara ziwe zimehama ni kufanya kazi kutumia nguvu ya siasa badala ya lojiki (lack of rational thinking), hasa ukizingatia mambo yafuatayo;
  • kuhamishia serikali Dodoma ni zaidi ya waziri na katibu mkuu (ambao wengi wana nyumba tayari Dodoma) kuhamia Dodoma. Wizara ni watu
  • kuhamishia serikali Dodoma inatia ndani kuhamishia ofisi zote za ubalozi kwenda Dodoma (je nao unawapa miezi miwili?)
  • kuna suala la kupata majengo na vyumba vya ofisi kwa wafanya kazi
  • kuna suala la malipo ya kuhamisha wafanya kazi na vyombo vyao
  • kuna suala la kuhamisha furniture, computer za ofisini toka Dar kwenda Dodoma
  • kuna suala la kusuka mfumo wa mawasiliano katika ofisi mpya huko Dodoma
  • kuna suala la wafanyakazi kupata sehemu za kukaa huko Dodoma
  • kuna suala la kutatua mambo yanayohusu familia, kama mke au mume ndie anaehama, au kama mke na mume wote ni wafanya kazi hapa Dar wataathiriwaje na kuhama huku
  • kuna suala la watoto wa wafanyakazi hawa walioko mashuleni hapa Dar kuhamia Dodoma
  • kuna suala la baadhi ya familia kutatua suala la nyumba zao watakazoziacha Dar
  • kuna suala la kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu kuhama badala ya kuwahamisha kama vile tuko kwenye state of emergency
  • nk
Ukizingatia mambo kama hayo hapo juu, utaona wazi kwamba Waziri Mkuu alitakiwa kutoa miezi kwa kiwango cha chini kabisa, sita, ili kuwe na maandalizi yenye utaratibu ili watu weze kuhama kwa mpangilio, na sio kuhamisha watu kama vile kupeleka kikosi cha jeshi mpakani baada ya kuvamiwa na nchi jirani. Hivi viongozi wetu huwa hawayaoni haya wanapotoa amri? Nashangaa sana awamu ya tano ya uongozi wa Tanzania imejaa amri ambazo zinatolewa kushoto, kulia na katikati bila kufanyiwa tafakari za kina. Hivi kweli hiyo ndiyo filosofia ya "Hapa Kazi Tu"?

Na cha ajabu, Waziri Mkuu anasema kwamba "hatuchezi mchezo wa siasa hapa, tutapitisha sheria katika Bunge mwezi Septemba kufanya suala la kuhamia Dodoma liwe rasmi" (we are not playing politics here...we will pass legislation in parliament in September to make the move to Dodoma official)

Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, kama sheria itafikishwa Bungeni Septemba, siku zote hizi suala la kuhamia Dodoma halikuwa rasmi? Na kama sheria ya kuhamia Dodoma itapelekwa Bungeni Septemba, kwa nini Waziri Mkuu anatoa amri juu ya jambo ambalo bado si rasmi kisheria?

Hivi kwa nini viongozi wetu wanadhani kila jambo linahitaji amri kama za kijeshi ili litekelezwe? Je, kutoa amri bila kufikiria athari za kisosholojia na kiuchumi (socio-economic impacts) sio ubwana ambao tuliupinga kwa muda mrefu sana? Frankly, I was expecting much better from my prime minister than this kind of reckless leadership style.

Ushauri wa bure kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni kwamba nguzo na nguvu ya taifa lolote iko katika muungano wa kifamilia. Unapovunja familia unavunja nguvu ya taifa. Huko nyuma empire ya Roma ilivunjika kwa sababu ya mvunjiko wa kifamilia. Kwa hiyo hili suala linahitaji utaratibu mzuri, gradual relocation implementation labda katika kipindi cha mwaka mzima, likifanyika kwa kuhamisha wafanya kazi katika kila wizara kwa awamu kulingana na impact zao katika kuendesha Wizara. Sio kuwaambia watu funga virago ondoka nenda Dodoma haraka. La sivyo utaona barua nyingi za kujiuzuru kazi au hata mivunjiko katika familia. Na watu wa ubalozi je, au umeamua serikali yote itakuwa Dodoma na wao wabaki Dar?

Na vyama vya wafanyakazi iweje viko kimya katika hili?
CDA walikwisha andaa kila kitu miongo kadhaa iliyopita....
Basi ni kibri tu cha kutotaka kuhamia...stareheee
 
Waziri Mkuu hajakosea. kazi yake ni kusimamia maamuzi ya serikali. Kama serikali imeamua kuhamia Dodoma immediately, unataka Waziri Mkuu afanye nini? leave him alone, he is just doing his job.
 
Nani alikwambia hadi viti na meza vitahamia Dodoma ?
 
Kuwa watashindwa au hawatashindwa sidhani kama ni issue hapa!!

Hivi unafikiri uamuzi huu umeangalia effect zake Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii (Politically, Economically and Socially)!!
Kwahiyo we ulitakaje ?

Kama hujui kitu kaa kimya
 
Back
Top Bottom