Hapa, Waziri Mkuu Majaliwa anakosea sana

Hapa, Waziri Mkuu Majaliwa anakosea sana

Nani amekuambia ofisi zote zitahamia Dodoma ndani ya miezi miwili?

Rais amesema zoezi litachukua miaka minne kuanzia alipozungumza.

Mkuu kama unaelewa Kingereza soma hapa chini; IPPMedia. Na hata kama amesema key government functions, niambie zipi kati ya government functions sio key? Azitaje basi tujue kuna watu au wizara zinatakiwa kupunguzwa kwa sabu sio za msingi (key) ilii tubane matumizi. Wengine tunachoelewa ni kwamba all government functions are key.

upload_2016-7-27_22-42-24.png
 
Waende Dodoma aisee...we have lost enough already by continuing being in Dar. Tanzania inatakiwa ikue sio kudumaa sehemu moja.
 
hawa c.c.m hawana akili kweli!ingekuwa hayo madawati yametolewa kutoka ktk bajeti rasmi ya serikali,at least wangekuwa na jeuri ya kujisifu!sasa cha ajabu madawati yenyewe tumewachangia,halafu wanajifanya wajanja kuchukua sifa zote!dadeki
madawati yenyewe kila halmashauri imedeal na shule zake na mpaka sasa zipo halmashauri zimeshindwa kutimiza malengo na hata hapo waache kila idara ijipange kivyake kulingana na watumishi ilionao.
 
Kama tuliweza kuhama kutoka Analojia kwenda digital kabla ya muda na kwa muda mfupi itashindikana nini serikali kuhamia Dodoma?
 
“It always seems impossible until it's done’’― Nelson Mandela.

Wrong application! Mandela never said it is possible for every thing to be done like yesterday. It was eventually possible to have democracy and a black president in South Africa - but do you know how long that took?

All we are saying is that it is not rational and realistic to issue an order that ministries should move to Dodoma within the next two months. Indeed, it is possible for ministries to move to Dodoma. We never refuted that.
 
Omba omba wa kigogo wamepunguziwa Safari za kuja Mkoani Dar es salaam kwa kuwa watabaki Jijini Dodoma
 
Mkuu kama unaelewa Kingereza soma hapa chini; IPPMedia. Na hata kama amesema key government functions, niambie zipi kati ya government functions sio key? Azitaje basi tujue kuna watu au wizara zinatakiwa kupunguzwa kwa sabu sio za msingi (key) ilii tubane matumizi. Wengine tunachoelewa ni kwamba all government functions are key.

View attachment 371917
Mimi sifahamu kiingereza lakini ninaona unaleta porojo zile zile ambazo serikali za CCM zilizopita walikuwa wanatulisha kuanzia mwaka 1976 kuhusu kuhamia Dodoma.
 
hawa c.c.m hawana akili kweli!ingekuwa hayo madawati yametolewa kutoka ktk bajeti rasmi ya serikali,at least wangekuwa na jeuri ya kujisifu!sasa cha ajabu madawati yenyewe tumewachangia,halafu wanajifanya wajanja kuchukua sifa zote!dadeki
Hamna UKIWA yoyote aliyechangia madawati
 
Wahamie haraka watuachie mji wetu mashuhuri wa kibiashara. Watumishi wa serikali wenye nyazifa kubwa na mishahara yao hiyo kukaa dar kunachochea ufisadi coz mishahara midogo lkn wanataka kuishi kama akina Bakharesa kisa wanakaa nao karibu. Wakikaa Dodoma watakuwa mbali na matycoon hivyo watapunguza tamaa ya ushindani na watu wenye hela zao, mawazo ya kupiga deal hela za serikali yataondoka...Ngosha anaakili sana anabana vyanzo vya ufisadi kila kona...
 
Kuna ulazima gani wa kulazimisha kuhama katika mwezi mmoja? July ishaisha, wanatakiwa wahamie Sepetember.

Unamuamisha waziri na msaidizi wake ila team na mafaili yake yote yamebaki DSM.
 
Mamlaka ya usitawishaji makao Dodoma (CDA) unajua ilianza lini??

Bavichaaa ifike mahali muwe mnatumia akili za panzi naona za nyumbu zinawaaibisha sana.

Kwahiyo wao wameshajenga majengo ya kupokea wizara zote?
 
Unamuamisha waziri na msaidizi wake ila team na mafaili yake yote yamebaki DSM.
Maigizo zaidi.

Ile mikutano yote ya mawaziri na wakuu wa idara na mashirika ya umma itakuwaje?

Waziri itabidi aje Dar kila mkutano?

Au hao viongozi wamfuate Dodoma?

Tunahesabu gharama hizi?
 
Nani amekuambia ofisi zote zitahamia Dodoma ndani ya miezi miwili?

Rais amesema zoezi litachukua miaka minne kuanzia alipozungumza.

Kama Rais alisema zoezi litachukua miaka 4 kwa nini hawa wengine wanataka lifanyike ndani ya wiki moja?! Ni kujipendekeza ama nidhamu ya woga??!!
 
Mbona mm nilihamishwa kwenda mkoani nikapewa wiki mbili.. Au ndo UKUTA umeanza? Kama sijasahau raisi alishasema maandalizi ya awali yameshafanyika.. Sasa was was wako ni nini.. Thrn ww unayelalamika unafanya kaz Wizarani au mwakilishi wao... Kama huijui system thrn acha kujifanya mjuaji na kuandika andika
 
Nani amekuambia ofisi zote zitahamia Dodoma ndani ya miezi miwili?

Rais amesema zoezi litachukua miaka minne kuanzia alipozungumza.

jpm anasema sawa ila wateule wake wanakurupuka, tizeba anaenda wiki ijayo. hahahaha!!! kazi ipo kweli kweli.
 
Maigizo zaidi.

Ile mikutano yote ya mawaziri na wakuu wa idara na mashirika ya umma itakuwaje?

Waziri itabidi aje Dar kila mkutano?

Au hao viongozi wamfuate Dodoma?

Tunahesabu gharama hizi?

Hadi sasa sijaona fungu lililoidhinishwa na bunge kuhusu serikali kuhamia dodoma.
 
jpm anasema sawa ila wateule wake wanakurupuka, tizeba anaenda wiki ijayo. hahahaha!!! kazi ipo kweli kweli.

Ataondoka na wafanyakazi walio chini yake? Familia yake je? Au yeye mwenyewe?
 
mtakubaliana nasi tu,sisi kina gogo la shamba pale tuliposema kwamba,miaka hii mitano ni ya majuto
 
Wakurupukaji wawili wamekutana. Hawatafakari wala hawataki ushauri kutoka kwa washauri wao. Hili la kuhamia Dodoma ni janga kubwa la Taifa. Hakuna bajeti iliyotengwa, Dodoma haiwezi kukidhi mahitaji mbali mbali ya Wafanyakazi wa Serikali kama Dar. Na motisha wa Wafanyakazi utaanguka vibaya sana.

Waziri Mkuu ametoa amri kwamba katika kipendi cha miezi miwili serikali yote iwe imehamia Dodoma.

Japokuwa suala la kuhamia Dodoma limekuwa la muda mrefu, lakini kutoa miezi miwili Wizara ziwe zimehama ni kufanya kazi kutumia nguvu ya siasa badala ya lojiki (lack of rational thinking), hasa ukizingatia mambo yafuatayo;
  • kuhamishia serikali Dodoma ni zaidi ya waziri na katibu mkuu (ambao wengi wana nyumba tayari Dodoma) kuhamia Dodoma. Wizara ni watu
  • kuhamishia serikali Dodoma inatia ndani kuhamishia ofisi zote za ubalozi kwenda Dodoma (je nao unawapa miezi miwili?)
  • kuna suala la kupata majengo na vyumba vya ofisi kwa wafanya kazi
  • kuna suala la malipo ya kuhamisha wafanya kazi na vyombo vyao
  • kuna suala la kuhamisha furniture, computer za ofisini toka Dar kwenda Dodoma
  • kuna suala la kusuka mfumo wa mawasiliano katika ofisi mpya huko Dodoma
  • kuna suala la wafanyakazi kupata sehemu za kukaa huko Dodoma
  • kuna suala la kutatua mambo yanayohusu familia, kama mke au mume ndie anaehama, au kama mke na mume wote ni wafanya kazi hapa Dar wataathiriwaje na kuhama huku
  • kuna suala la watoto wa wafanyakazi hawa walioko mashuleni hapa Dar kuhamia Dodoma
  • kuna suala la baadhi ya familia kutatua suala la nyumba zao watakazoziacha Dar
  • kuna suala la kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu kuhama badala ya kuwahamisha kama vile tuko kwenye state of emergency
  • nk
Ukizingatia mambo kama hayo hapo juu, utaona wazi kwamba Waziri Mkuu alitakiwa kutoa miezi kwa kiwango cha chini kabisa, sita, ili kuwe na maandalizi yenye utaratibu ili watu weze kuhama kwa mpangilio, na sio kuhamisha watu kama vile kupeleka kikosi cha jeshi mpakani baada ya kuvamiwa na nchi jirani. Hivi viongozi wetu huwa hawayaoni haya wanapotoa amri? Nashangaa sana awamu ya tano ya uongozi wa Tanzania imejaa amri ambazo zinatolewa kushoto, kulia na katikati bila kufanyiwa tafakari za kina. Hivi kweli hiyo ndiyo filosofia ya "Hapa Kazi Tu"?

Na cha ajabu, Waziri Mkuu anasema kwamba "hatuchezi mchezo wa siasa hapa, tutapitisha sheria katika Bunge mwezi Septemba kufanya suala la kuhamia Dodoma liwe rasmi" (we are not playing politics here...we will pass legislation in parliament in September to make the move to Dodoma official)

Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, kama sheria itafikishwa Bungeni Septemba, siku zote hizi suala la kuhamia Dodoma halikuwa rasmi? Na kama sheria ya kuhamia Dodoma itapelekwa Bungeni Septemba, kwa nini Waziri Mkuu anatoa amri juu ya jambo ambalo bado si rasmi kisheria?

Hivi kwa nini viongozi wetu wanadhani kila jambo linahitaji amri kama za kijeshi ili litekelezwe? Je, kutoa amri bila kufikiria athari za kisosholojia na kiuchumi (socio-economic impacts) sio ubwana ambao tuliupinga kwa muda mrefu sana? Frankly, I was expecting much better from my prime minister than this kind of reckless leadership style.

Ushauri wa bure kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni kwamba nguzo na nguvu ya taifa lolote iko katika muungano wa kifamilia. Unapovunja familia unavunja nguvu ya taifa. Huko nyuma empire ya Roma ilivunjika kwa sababu ya mvunjiko wa kifamilia. Kwa hiyo hili suala linahitaji utaratibu mzuri, gradual relocation implementation labda katika kipindi cha mwaka mzima, likifanyika kwa kuhamisha wafanya kazi katika kila wizara kwa awamu kulingana na impact zao katika kuendesha Wizara. Sio kuwaambia watu funga virago ondoka nenda Dodoma haraka. La sivyo utaona barua nyingi za kujiuzuru kazi au hata mivunjiko katika familia. Na watu wa ubalozi je, au umeamua serikali yote itakuwa Dodoma na wao wabaki Dar?

Na vyama vya wafanyakazi iweje viko kimya katika hili?
 
Tatizo hatujui hata vipaumbele katika utekelezaji wa mipango yetu.
 
Back
Top Bottom