Hapa uchawi unahusika?

Hapa uchawi unahusika?

Mimi nikisikia hadithi ya dini naona kama watu wamekata tamaa ya maisha.We umeshamjua mbaya wako ni mme wa dada yako alafu unamchelewesha! Nakwambia utazunguka makanisa yote na utotatua tatizo masta simama kiume. Ningekua mimi uyo jamaa angeshakua marehemu siku nyingi kwa mikono yangu acha kulia lia nenda front man
JELA inakusubiri
 
"Hakika shetani hana mamlaka juu ya wale walioamini na wanaomtegemea Mola wao" (Quran 16:99)
"Wala mchawi hafaulu popote afikapo" (Quran 20:69)
"Msiogope, Bila shaka MIMI ni pamoja nanyi; nasikia na naona" (Quran 20:46)
"Mwenyezi MUNGU ni mlinzi wa wale walioamini, Huwatoa katika giza na kuwaingiza kwenye Nuru" (Quran 2:257)

Ndugu yangu mtegemee Mwenyezi MUNGU tu; Muamini Yeye tu, utauona Mkono wa Mwenyezi MUNGU katika maisha yako. Mimi nimeuona mkono wake nawewe utauona. Soma Zaburi 23 na Quran 2:255 utapata nguvu mpya ya kuzidi kumtegemea Mwenyezi MUNGU.

Kaka umemaliza,mungu akubariki
 
Habari ya kazi wakuu!,

Mimi ni kijana wa miaka 31 na nimehitimu degree ya uhasibu mwaka 2011. Mwaka huo huo nlipata kazi kwenye kampuni binafsi na maisha yakawa yanaenda vema tu mpaka mwaka 2014 mwezi wa 3 ndipo maisha yakabadilika nakuwa hayaeleweke.

Ni kwamba mwaka 2012 niliingia katika ugomvi na dada angu wa baba na mama mmoja tukazozana juu ya mali za urithi wa wazazi wetu. Dada alinipigia simu na kuahidi kuwa atanikomesha na shemeji yani mume wa dada akasisitiza lazima niwajue (ieleweke shemeji ni nmganga wa kienyeji) basi siku chache nikafukuzwa kazi bila sababu za msingi,nikapata kazi tena lkn nikafukuzwa pia na matatizo yakawa yanaendelea yani watu wananichukia bila sababu mara ugomvi na mke wangu hauishi tena usio na kichwa wala miguu,ndoto za ajabu ajabu hasa kuota napigana na watu nisiowajua au nawajua,kila nachofanya hakifanikiwi hata kama nitakuwa makini sana,hivi sasa sina muelekeo wa maisha na kila kitu hovyo kabisa...

Je, naweza nisaidiwa vipi kujiondoa ktk janga hili?,kuna uwezekano kweli mtu akavuruga mipango yako kimazingara?

WEKA PICHA FASTA MKUU.
 
Umeingia hofu kuu. Woga umekutawala. Uchawi upo ILA kwa maelezo yako ni wazi kuwa hujarogwa wewe...
 
Habari ya kazi wakuu!,

Mimi ni kijana wa miaka 31 na nimehitimu degree ya uhasibu mwaka 2011. Mwaka huo huo nlipata kazi kwenye kampuni binafsi na maisha yakawa yanaenda vema tu mpaka mwaka 2014 mwezi wa 3 ndipo maisha yakabadilika nakuwa hayaeleweke.

Ni kwamba mwaka 2012 niliingia katika ugomvi na dada angu wa baba na mama mmoja tukazozana juu ya mali za urithi wa wazazi wetu. Dada alinipigia simu na kuahidi kuwa atanikomesha na shemeji yani mume wa dada akasisitiza lazima niwajue (ieleweke shemeji ni nmganga wa kienyeji) basi siku chache nikafukuzwa kazi bila sababu za msingi,nikapata kazi tena lkn nikafukuzwa pia na matatizo yakawa yanaendelea yani watu wananichukia bila sababu mara ugomvi na mke wangu hauishi tena usio na kichwa wala miguu,ndoto za ajabu ajabu hasa kuota napigana na watu nisiowajua au nawajua,kila nachofanya hakifanikiwi hata kama nitakuwa makini sana,hivi sasa sina muelekeo wa maisha na kila kitu hovyo kabisa...

Je, naweza nisaidiwa vipi kujiondoa ktk janga hili?,kuna uwezekano kweli mtu akavuruga mipango yako kimazingara?
hapo ni kukimbilia kwa Yesu tu,hakuna jingine
 
Back
Top Bottom