Kama unahitaji maombi nifate inbox.
Maombi si jibu ndugu yangu, Jibu sahihi ni yeye kumtegemea Mwenyezi MUNGU kwa asilimia mia moja, Na huwezi kumtegemea Yeye kama humuamini; Kwa hivyo, Ufunguo Mkuu ni Imani, Kumuamini Mwenyezi MUNGU ndio Ufunguo Mkuu kabla hata ya kumtegemea. Baada ya kumuamini ndio amuombe Mwenyezi MUNGU moja kwa moja, hakika Mwenyezi MUNGU anasikia na anaona, sio lazima fulani akamuombee, huko ni kumtegemea muombezi baadala ya Mwenyezi MUNGU. Akiwa na wasiwasi usiku wa manane pia akupigie wewe simu ili umuombee? Mfundishe namna ya kumtegemea Mwenyezi MUNGU na jinsi gani yeye mwenyewe aombe msaada kwa mwenyezi MUNGU kwa kutumia neno lake, Hakika Mwenyezi MUNGU ni mwaminifu wa neno lake na wala yeye havunji miadi.
Neno linasema
"Na waja wangu watakapo kuuliza khabari Zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba. Basi nawaniitikie Mimi, nawaniamini Mimi, iliwapatekuongoka” (Quran 2: 186).
"Na Anayemcha Mwenyezi MUNGU Humtengenezea njia ya kutokea” (Quran 65: 2). Na anayemtegemea Mwenyezi MUNGU Yeye humtosha” (Quran 65: 3).“Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kusali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu” (Quran 2: 45). Aya hizi ni za Quran, kama huiamini, soma Biblia, kuna aya nyingi sana zinadhihirisha nguvu za Mwenyezi MUNGU, ni wewe tu kuamini na kuanza kutumia. Soma zaburi 23 na Quran 2:255 utapata faraja hata kama mashetani wenye pembe ndefu wamekuzunguka. Ili roho wa MUNGU na awe ndani yako muda wote sharti zake zipo kwenye (Zaburi 1:1-3), hizo ni universal principles, si dini, bali ni neno la Mwenyezi MUNGU.
Off-course kuna mambo mengi kabla hata ya kufanya hayo, anatakiwa afanye toba huku akisamehe wote waliomkosea ili naye apate kusamehewa. Aisiwe vuguvugu vinginevyo shetani atamshinda, Achague kuwa wamoto au wabaridi. Vita ya kiroho ni kama vita ya kawaida ya kimwili, kama huna silaha, utashindwa tu.