Hapa nimebambikizwa au nimeibiwa mtoto?

Hapa nimebambikizwa au nimeibiwa mtoto?

Hilo nalo nshaliwazaga saana, kama anahudumiwa nakuishi maisha mazuri well and good, ila kama anapata tabu na baba yake napata kariziki kakutosha atakua anamuonea sana mtoto
Yawezekana mtoto ni wako kabisa ila alishapatikana mtu akabambikiziwa kwakuwa ana pesa na anahudumia vizuri.
 
Hivi akiwa ndo mwenye akili na mafanikio katika watoto wako utapokea mpunga wake?
 
Inategemea na mama yake kamweleza nini kuhusu mimi, maana sina kosa so far.
Hivi akiwa ndo mwenye akili na mafanikio katika watoto wako utapokea mpunga wake?
 
We jamaa pesa unaichungulia saaaaana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Imagine unakula bata saana halafu damu yako somewhare inateseka how would you feel?
Angekuwa anakula pesa kote kote[emoji23][emoji23][emoji23]
 
We jamaa pesa unaichungulia saaaaana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Imagine unakula bata saana halafu damu yako somewhare inateseka how would you feel?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Damu yako ujue nayo ina maisha mazuri kuliko unayoweza kuipa ndo maana imepelekwa kwingine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089]
 
Vyovyote vile nikianza na supu na bia na nyama choma na offer kadhaa kwa watu tuliokaa meza moja na kamchepuko haifiki saa sita usiku. Najijua nikiamua kupiga kibiriti hela, ndo maaana hainiumi
Unazimaliza peke yako au na malaya
 
I feel u mkuu, mtoto anajengewa awe na chuki na baba mtu bila kujua hata sababu ila end of the day kama ni damu yako itakutafuta tu
Kweli mkuu mimi nineishi maisha ya uswahilini naona watoto wanavyoteseka kwa maamuzi ya wazazi so staki damu yangu iteseke pia, watoto wa namna hii wanakua na resentment saana kwa baba zao wakidhani walitelekezwa
 
Hapo mkuu hata sina shida moyo wangu mweupeee!! Ni kama mtu anayesili mtoto wa maskini, yule maskini anamtoa kwa moyo mweupe akijua mtoto ataishi maisha mazuri
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Damu yako ujue nayo ina maisha mazuri kuliko unayoweza kuipa ndo maana imepelekwa kwingine[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089]
 
I feel u mkuu, mtoto anajengewa awe na chuki na baba mtu bila kujua hata sababu ila end of the day kama ni damu yako itakutafuta tu
I wish some day aje hata akiwa mkubwa ntampanga hadi anielewe ila kovu litakuwepo, na kama alikosa elimu na ameishi magumu, atakuwa ananiangalia kama mie ndo sababu
 
Sasa wewe badala ya kusema Unatuma pesa ya Matumizi unataka upeleke lisura tena???[emoji23][emoji23][emoji23] Hakuna mwanamke asiependa helaa ila kuomba ndo tatizo so hiyo ndo ilikuwa njia yake uendelee kumpa chochote kitu..

HAKUNA MWANAMKE WA KITANZANIA ATAKUTUNZIA MIMBA YAKO KIMYA KIMYA... HATA KAMA HANA UHAKIKA ATABAHATISHA TU UKIKUBALI INAKULA KWAKO!
Mbona mimi nina mpango kama huwa wa huyo dada?!
Nipate mbegu tuu yatosha!
 
Mbona mimi nina mpango kama huwa wa huyo dada?!
Nipate mbegu tuu yatosha!
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] Mungu anawaona mnavyotufisha kwa watoto wenu[emoji57]
 
Hamna kitu hapo....SANUKA
Habari za asubuhi ya jumapili wadau,

Kisa kipo huvii,

Ilikua mwaka 2015 nilisafiri kwenda mkoa wa Arusha wilaya ya Loliondo sana kutafuta riziki, huko nikakutana na mdada mzuri saaana mweupe kaenda hewani na shepu ya maana ni mdada wa Kiarusha/Mmasai, tukaJUANA kwa siku kadhaa then nilipomaliza kilichonipeleka huko, nikarudi zangu kwangu Iringa, tukaendelea na mawasiliano ya hapa na pale.

Hakuwahi kunipiga mzinga hata siku moja ila nlikua najiongeza mara kadhaa nlimuwezesha kiasi kidogo cha pesa coz show zake nlizielewa sana.

Baada na miezi kadhaa akaniambia kwamba amelazwa Mt. Meru hospital, nikampa pole na kumtumia kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu, baada ya kama siku 4 akaniambia ameruhusiwa na anarudi kwao Monduli.

Miezi mitatu baada ya kuruhusiwa hospitalini akaniambia kwamba ana mtoto, nilishangaa maana hakuwahi kuniambia ana mimba, nikampa hongera zake, akaitikia na kuniambia kwamba mwanae anafanana sana na mimi, sikutilia maanani, nikamwambia labda kwakua alinipenda ndomana mtoto anafanana na mimi.

Baada ya wiki 1 alipoona siunganishi matukio, akaamua kunichana kwamba mtoto ni wakwangu, duuuh! Nilistuka sana na kuanza kuhesabau siku, kwa kuwa tulipiga picha na nliziweka Dropbox ikabidi nizisake kujua tarehe nilizokutana nae.(picha huwa zina tarehe na saa ya picha kupigwa)

Nikaona zinaoana na siku alizolazwa Mt. Meru, nikasema mbona hukuniambia siku zote hizi ili nijue, akadai hakutaka kujipa stress maana huenda ningekataa na pia akadai yeye alipanga kuzaa na mimi kwa sababu ya muonekano wangu na kwamba mtoto ni wakwake na sio wetu.

Nilipatwa na mshangao sana, nikawa namuomba picha ya mtoto maana alikua na miezi 3 na wiki kadhaa ili nijiridhishe kama labda anafanana ni mimi akagoma katakata. Nikamuuliza sa alikua na sababu gani kuniambia kwamba ana mtoto wangu na hali hatuka hata nimjue? akasema amefanya ivo ili nijue nina mtoto na si kwa dhumuni la mimi kuhusika na mtoto.

Nilikasirishwa sana na hiyo tabia nikapanga kwenda kumsaha Monduli maana napajua nlisomaga A-level Moringe miaka ya 2000, nlipomweleza wazo hilo akaniambia atanitumia picha.

Nikasubiri kama wiki2 akatuma picha za mtoto ananyekaribiana umri na yule mtoto ila sura, rangi na muonekano vinatofautiana sana na jinsi aliponisimulia pindi aliposema mtoto wake alizaa na mimi na kwamba anafanana na mimi rangi hadi sura, mi nina rangi nyeupe kiasi na yeye ni mweupe saana, sa picha ya mtoto aliyotuma ni ya mtoti mweusi tii ana komwe kubwa kama mkenya (sina nia ya kumdharau huyu mtoto wa kwenye picha).

Nikahisi hapa nachezewa mchezo ili nisiende, nikasisitiza nia ya kwenda, akaniambia anabadilisha namba ya simu na kweli akawa hapatikani tena hadi leo, kwa kuwa Monduli ni kubwa saana kuanzia mto wambu, Monduli Juu, vijijini na sikujua nampataje nikashindwa kumtafuta na nimepoteza mtoto.

Wanawake bwana!! Kama aliamua kuzaa mimi ili apate copy yangu si angekaa kimyaa sasa napata shida kuona sijahusika katika maisha ya damu yangu, baadae mtoto aje kunitafuta ukubwani aseme baba yake alimkataa, pengine akamuacha kwa bibi yake akaenda kusaka maisha kwingine mtoto wangu akapata taabu na baba yake nipo.

Maoni yenu wadau
 
Back
Top Bottom