Hapa nimebambikizwa au nimeibiwa mtoto?

Hapa nimebambikizwa au nimeibiwa mtoto?

Alvin A.

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2016
Posts
2,865
Reaction score
3,640
Habari za asubuhi ya jumapili wadau,

Kisa kipo hivii,

Ilikua mwaka 2015 nilisafiri kwenda mkoa wa Arusha wilaya ya Loliondo kutafuta riziki, huko nikakutana na mdada mzuri saaana mweupe kaenda hewani na shepu ya maana ni mdada wa Kiarusha/Mmasai, tukaJUANA kwa siku kadhaa then nilipomaliza kilichonipeleka huko, nikarudi zangu kwangu Iringa, tukaendelea na mawasiliano ya hapa na pale.

Hakuwahi kunipiga mzinga hata siku moja ila nlikua najiongeza mara kadhaa nlimuwezesha kiasi kidogo cha pesa coz show zake nlizielewa sana.

Baada na miezi kadhaa akaniambia kwamba amelazwa Mt. Meru hospital, nikampa pole na kumtumia kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu, baada ya kama siku 4 akaniambia ameruhusiwa na anarudi kwao Monduli.

Miezi mitatu baada ya kuruhusiwa hospitalini akaniambia kwamba ana mtoto, nilishangaa maana hakuwahi kuniambia ana mimba, nikampa hongera zake, akaitikia na kuniambia kwamba mwanae anafanana sana na mimi, sikutilia maanani, nikamwambia labda kwakua alinipenda ndomana mtoto anafanana na mimi.

Baada ya wiki 1 alipoona siunganishi matukio, akaamua kunichana kwamba mtoto ni wakwangu, duuuh! Nilistuka sana na kuanza kuhesabau siku, kwa kuwa tulipiga picha na nliziweka Dropbox ikabidi nizisake kujua tarehe nilizokutana nae.(picha huwa zina tarehe na saa ya picha kupigwa)

Nikaona zinaoana na siku alizolazwa Mt. Meru, nikasema mbona hukuniambia siku zote hizi ili nijue, akadai hakutaka kujipa stress maana huenda ningekataa na pia akadai yeye alipanga kuzaa na mimi kwa sababu ya muonekano wangu na kwamba mtoto ni wa kwake na sio wetu.

Nilipatwa na mshangao sana, nikawa namuomba picha ya mtoto maana alikua na miezi 3 na wiki kadhaa ili nijiridhishe kama labda anafanana ni mimi akagoma katakata. Nikamuuliza sa alikua na sababu gani kuniambia kwamba ana mtoto wangu na hali hakutaka hata nimjue? akasema amefanya ivo ili nijue nina mtoto na si kwa dhumuni la mimi kuhusika na mtoto.

Nilikasirishwa sana na hiyo tabia nikapanga kwenda kumsaka Monduli maana napajua nlisomaga A-level Moringe miaka ya 2000, nlipomweleza wazo hilo akaniambia atanitumia picha.

Nikasubiri kama wiki 2 akatuma picha za mtoto anayekaribiana umri na yule mtoto ila sura, rangi na muonekano vinatofautiana sana na jinsi aliponisimulia pindi aliposema mtoto wake aliyezaa na mimi na kwamba anafanana na mimi rangi hadi sura, mi nina rangi nyeupe kiasi na yeye ni mweupe saana, sa picha ya mtoto aliyotuma ni ya mtoto mweusi tii ana komwe kubwa kama mkenya (sina nia ya kumdharau huyu mtoto wa kwenye picha).

Nikahisi hapa nachezewa mchezo ili nisiende, nikasisitiza nia ya kwenda, akaniambia anabadilisha namba ya simu na kweli akawa hapatikani tena hadi leo, kwa kuwa Monduli ni kubwa saana kuanzia mto wambu, Monduli Juu, vijijini na sikujua nampataje nikashindwa kumtafuta na nimepoteza mtoto.

Wanawake bwana!! Kama aliamua kuzaa mimi ili apate copy yangu si angekaa kimya? sasa napata shida kuona sijahusika katika maisha ya damu yangu, baadae mtoto aje kunitafuta ukubwani aseme baba yake alimkataa, pengine akamuacha kwa bibi yake akaenda kusaka maisha kwingine mtoto wangu akapata taabu na baba yake nipo.

Maoni yenu wadau
 
Loliondo ni 400 Km kutoka Arusha na yeye alikua ameenda mara moja kufanya biashara sitaweza kumtress maadam namba sijabadilisha nasubiria muujiza kama atanitafuta
Nenda kwenye vijiwe mlivyokuwa mnakutana watakuwa na taarifa zake
 
Mkuu nilikutana naye kwa siku kama 5 hivi tunaachana sina contact ya mtu mwingine yeyote wala hakuwahi kunitafuta kwa namba ngeni zaidi ya aliyokua anatumia sijaipote kwasababu ipo Google drive ina imeshablokiwa na bado siifuti tu
Huna namna vinginevyo uwe na detailed information kumhusu huyo mama wa mtoto wenu ili ujipange uende ukahangaike hadi umpate uungane na damu yako
 
Mkuu nilikutana naye kwa siku kama 5 hivi tunaachana sina contact ya mtu mwingine yeyote wala hakuwahi kunitafuta kwa namba ngeni zaidi ya aliyokua anatumia sijaipote kwasababu ipo Google drive ina imeshablokiwa na bado siifuti tu
Picha zake yeye mama wa mtoto unazo? Kama unazo ,jipange uwe na fungu la kukuwezesha kukaa kule walau kwa wiki ukihangaika kumpata.

Assume ni nduguyo (mama) kwa mfano, ukipambana unampata ila kama hauna hata picha yake ni shida
 
Picha zake yeye mama wa mtoto unazo? Kama unazo ,jipange uwe na fungu la kukuwezesha kukaa kule walau kwa wiki ukihangaika kumpata.

Assume ni nduguyo (mama) kwa mfano, ukipambana unampata ila kama hauna hata picha yake ni shida
Ninazo mkuu ntalifanyia kazi wazo lako
 
Back
Top Bottom