Hapa Lowassa hatoki...

pia mwigilu hana adabu. ukifuatilia jimboni kwake utasikia anatembea na wake za watu, je huyo mtoa matusu atawatoa c.c.m au atawafundisha kina nape kutukana watu., pia amejaa majigambo na majivuno ya elimu kna kwamba kasoma uchumi pekee yake tz
 
jf na wanacdm ndo wamechangia kupanda chati kwa kijana mwigulu.ilikua ni kumsema daily,kumbe ndio wanamfagilia.
Na hiyo ilitokana na uchaguzi wa igunga na peformance yake kwenye bunge la bajeti iliyowafanya cdm wamchukie kwelikweli.

....... pia ni mchumi mahiri sana, nadhani next from Lipumba
 
Reactions: Ame

wewe na mwigulu wote vimeo,wimbo wa dhaifu kulalamika na ataishia kulalama tu hana la kufanya cz ni DHAIFU,na huyo mw3igulu ni kalaza na ataishia kuporomosha matusi tu,amuulize makamba mkuu(alizimika kama mshumaa).
 

Huu mfumo ndiyo ambao wengine tumeamua kuuvalia njuga kuuvunja. Ni aibu sana kuona watu wanapenda kula wasichokipanda na hii inatokana na system mbaya ya siasa kushika hatamu badala ya uchumi kushika hatamu through production functions. Ndiyo maana inaogopesha kusikia watu wanamshangilia mchumi aliyeshindwa kutofautisha financial na economic analysis katika budget kama tofauti hizi hakuziweza ataishauri vipi serikali na ukumbuke kwakua chama ndiyo kimeshika hatamu inamaana uchumi unategemea wanasiasa badala ya wachumi...

Si kweli hakuna wachumi wazuri Tanzania ama watendaji wengine; ila hao wazuri mara nyingi siyo wanasiasa na hasa ukizingatia siasa ya Tanzania isivyo ya kistaarabu so wengine wameamua ama kunyamaza kimya ama kuhamia nchi zingine ndiko unakosikia Botswana, South Africa, Namibia etc ndiyo mihimili katika chumi za nchi hizo..Sasa hawa watu kwanini hawawezi kusaidia nchi yao? Kwasababu hawajapewa nafasi na walio na nafasi wengi ni wapiga debe.

Tumeona mfano wa akina Prof Mhongo sheria inayosaidia kufilisi nchi ndiyo inayoshinda dhidi ya dhamira njema ya viongozi na wengine wanashangilia pale haki inaposhindwa mbele ya sheria inayolinda uovu....Can you imagine that? What is the use of sheria? Kungekuwa na social capital hakuna haja ya sheria lakini pale sheria inaposhindwa kutimiza malengo badala ya kuangalia what was the intesion watu wanaangalia blindly bila objectivity yoyote. Nilifurahi kusikia Prof. aliposema hatokaa aombe msamaha wezi....To me kila mtu mwenye akili timamu akisimamia maneno yake na dhamira kama prof itafika wakati hawa mafisadi watakimbia wenyewe na kutuachia nchi yetu...Lakini tukiendelea kwa mtindo huu wa watu wanaofahamu mambo wanaji-exclude nakujiona haiwahusu basi ndiyo wote tuna ongozwa na kila mwenye uwezo wa kuongea vizuri hata kama hajui how to bring into action anachokiongea.
 


Mi ninavyo wacheki nyote wawili mnaishi kwa hisia huku mwingine akiwa na mapenzi na mwingine akiwa na chuki; what is the difference between two of you?..You are all one and the same! Utaifa wako unaouelezea uko wapi hapa? Kwamba EL siyo fisadi? Atleast wengi wetu kwenye mahakama ya umma tumesikia anagawa sadaka kubwa kubwa makanisani na misikitini pengine hilo tu linatosha ss kuwa na evidance kama mtumishi wa umma mbona hafanani na ss? Ama yeye anamshahara wa scale ya tofauti na ss wengine? Mahakama inayosema hivyo ni ya umma (magazeti yakiwa mouth piece yake na hakuwahi shitaki hata moja) wewe unasema akiitwa mahakamani ipi ile unayo iamini wewe au hata hii ya umma ambao inamtuhumu?
 
....... pia ni mchumi mahiri sana, nadhani next from Lipumba

Iwapo magazeti yalisema ukweli kwamba mchumi wa CCM atabadilishwa kwa sababu ameshindwa kusimamia rasilimali za chama, what else do yo need to prove kwamba yeye ni mchumi wa elimu tu lakini sio vitendo; Ni vigumu kuamini jinsi gani mtu anapewa mali zote za CCM azisimamie, mali ambazo Nape wakati fulani alisema zinafikia thamani ya kama sijakosea, Billioni 50, na bado ashindwe kufanya something meaningful out of it???

Ni kama mzazi kumsomesha mwanae vizuri sana kwenye masuala ya uchumi, kisha akampa kazi kwenye moja ya makampuni yake yenye mafanikio kiuchumi na yanayojiendesha kwa faida, halafu baadae anamkabidhi biashara zake zote azisimamie - majengo, mashamba n.k, lakini mtoto huyu anashindwa ku deliver, tena kwenye soko ambalo halina ushindani; Ni ajabu sana;
 

When it comes to youths, inazidi kudhihirika kwamba CCM is increasingly becoming the Magnate for the Corrupt Wakati Chadema is increasingly becoming the Magnate for the Talented; Hii inachangiwa sana na utamaduni wa CCM wa leadership succession compared to strategy ya Chadema ya leadership recruitment;

Mbaya zaidi, vijana wa CCM wamerithishwa dhana ya leadership na wakubwa zao kwamba its all about being self serving, ignorant, dishonest and stubborn; ndio maana many youths in CCM (not all of them) consistently perceive these as key features of leadership, na matokeo yake ndio hayo, the more they practice such, the more they get rewarded; Kwahiyo kwa kijana kuwa ignorant, dishonest and stubborn in CCM, IT PAYS!!!

Overtime, they will come to pay the price of political expediency, but until then, mtaendeleo kuona hoja zetu hazina mashiko; Itakuwa ni vichekesho miaka kumi na tano tokea sasa kwani vijana hawa watakuwa bado in middle aged na wenye political ambition na pia nguvu za kufanya kazi wakati hawa watawala wanaowatumikia watakuwa vikongwe vinavyo kula pensheni, na wakiwafuata wakati huo kwa mwendelezo wa kutumikia wakubwa badala ya chama na wananchi, watachoambulia ni kuambiwa "Mimi ni Mstaafu Bwana, Niache Nipumzike". Sijui wataficha wapi nyuso zao;
 
Reactions: Ame
Wote hao ni vilaza hakuna wa kumwongoza mwenzake njia. Mwigulu, Meghji, Nape!!! hakuna jipya.
 

Kwa kuongezea tu ni kama ifuatavyo kuhusu Katibu Mkuu mpya wa CCM:
Abdulahman Kinana kama sijachanganya alishawahi kuwa waziri, mojawapo ya wizara ilikuwa ya ujenzi katika awamu za kabla ya Mkapa na Kikwete. Alitoswa kwa sababu ya kashfa ya ubadhilifu wa pesa za ujenzi mabilioni ya pesa yaliyeyuka na ndio unaona amebaki kuegemea upande wa chama kwani serikalini alishanuka.
 
Reactions: Ame

Kwni ccm wana sera mpya basi? sera yao kuu kwa sasa ni chukua chako mapema, sasa wameshtukiwa unafikiri watakuja na sera gani zaidi ya vijembe?
 

chadema ndio wanamuhofia a ndio wamekua wakimtaja taja,sana humu,sio ccm ambao walishamalizana nae kwa kumtoa kwenye kamati,yeye pia anajua hana ushawishi tena ccm ndio mana hakugombea u nec kupitia kapu(viti 10 vya bara)ambako ndiko kipimo cha juu cha kukubalika na kuwa na mtandao mpana chamani ndio mana akakimbilia kule wilayani kwa watoto sio huku kwa wakubwa wenzake!
 

vipi zile kata tatu mlizoshinda juzi zinaonyesha dalili zozote kwamba mtafufuka tena?
 

kinana waziri wa ujenzi! hii siikumbuki kama imewahi kutoka hapa tanzania labda umechanganya taarifa kamanda,jipange
 
Mkuu MCHAMBUZI nishabiki wa Makamba ndo maana juzi amesema anafaa hata kugombea uraisi as if sasa Ikulu ya TZ imekua sehemu ya kwenda kukuzia vijana.

januari hizo kura zenyewe za ujumbe wa nec kupitia kapu-viti kumi vya bara amepita kwa mbeleko ya babake mzee makamba,kwa mliofuatilia mkutan mkuu ule mzee makamba aling'ara sana kwa wajumbe na ilionyesha bado ana mvuto,ushahidi ni huu,tizama then upime kama kuna mjumbe angeweza kumnyima kura mtoto wa huyu mzee au yeyote aliyepigiwa debe na huyu mzee
 
Last edited by a moderator:
NAKUFAGILIA... Tatizo letu "small minds...", ndiyo maana kila wakati LO WASSA LOWASSA LOWASSA. ONA mkuu, ukipost thread ya issues bila watu kama kina LOWASSA au NCHEMBA wa SLAA: hakuna atayerespond, believe me. Lakini wataje hao uone, oooooh, utapata responces 700 - UPUUZI. Na mimi nakuhakikishia kuwa, ni kutokana na hali hiyo ndiyo maana CCM wameicha JF iendelee kwani haigusi achilia mbali kubomoa misingi/mihimili ya utawala wa CCM ambayo ni rushwa, ujinga, mabavu, mfumo wa uteuzi, katiba nk. ONA hata nafasi tuliyopewa ya kujadili katiba mpya, tumeiacha ipotee, kumbe hakukuwa na hoja zozote za maana, ila tu kwamba katiba ibadilike. HAYA ENDELEENI KUJADILI KINA LOWASSA, hakuna kitakachobadilika: NASHAURI, MASUALA YAJADILIWE kama mfumo wa kodi, elimu, makazi bora (hata hii nayo SLAA ameicha ipotee, jamani? Inaskitisha) nk hapo kutakuwa na jambo la maana.

Huyu Lowasa ni nani ktk nchi hii, kwa nini mna mwogopa kiasi hicho? Utakuta kila mleta mada Lowasa,lowasa,lowasa
 

kama hapo kwenye njano ndiVyo! ,swali la kizushi VIPI HAPO KWENYE RANGI YA SHATI LAKO LA KIJANI (ni gamaba au).
 
Nadhani sifa ya uongozi siku hizi CCM ni kuwa na uwezo wa KUVITUKANA VYAMA VYA UPINZANI. Hivi besides hilo la kuchukiwa na upinzani ni lipi lingine linalomfanya huyu bwana Mwigulu to fit in this very serious and vital position kwa mkabala wa chama chochote cha siasa? Ndio maana kila siku ccm wanabadilisha safu ya juu ya uongozi, simply because wanachagua watu wenye uwezo wa kutukana wapinzani. Job description ya Secretary general ni pana mno kupewa mtu ambaye hata uwezo wake wa kujenga hoja unatia shaka. Ukumbuke sio tu ata deal na wapinzani nje ya chama, bali anahitajika mtu mwenye uwezo wa kimkakati na kiushawishi kutuliza migongano ndani ya chama. Ninachoona mimi mpaka sasa CCM hawajui MCHAWI WAO NI NANI. Mchawi wa CCM si CHADEMA , bali ni umbu la kiuongozi na kimaadili ndani ya CCM yenyewe! In my opinion CCM kilipoteza siku nyingi sifa ya kuwa chama cha siasa. Why? kwanza chama chochote cha siasa kinakuwa na miiko, kwa CCM hapendwi mtu ila pochi yako.Ukiwa jamabazi, sawa, jangili sawa, gaidi sawa , so long huwapingi WAKUU WA CHAMA. Kifupi CCM ni mkusanyiko wa wachumia tumbo, ndio maana migogoro ndani ya ccm ni ya ULAJI ZAIDI KULIKO MASLAHI YA NCHI. Matajiri wamekikamata chama na ndio wanaoamua nani awe kiongozi kwa MASLAHI YAO BINAFSI. Pili wanachama wa ccm wenye NYADHIFA waliowengi ni MASHABIKI zaidi na si watu ambao wanauelewa wa hatima ya nchi yetu.There is NO difference between them and simba and yanga fans, who never knew why are they simba or yanga! If you ask them they will simply tell you "IT IS WITHIN THEIR BLOOD" na ccm ndio hivyohivyo.Hawajui wanasimamia nini nje ya maslahi yao ya kiuchumi, ndio maana Tanzania ndio nchi pekee mwanasiasa anaweza shinda kwa kuwa na mvuto wa SURA without sifa nyingine ya ziada. Tatizo ni wapiga kura wa ccm hawana VISION ya aina gani ya viongozi wanatuwekea. Hii ndio maana tunazalisha viongozi ambao wanajiita wazalendo lakini hawajui hata UHALALI WA TZ KUMILIKI ZIWA NYASA MPAKA WAENDE KUWAULIZA WAZEE WA KYELA! Hii ndio sababu ndani ya ccm kuna watu wana nguvu ambayo inawatisha hata wao ccm lakini ukichunguza hupati sababu ya MAANA ya hawa watu kuwa na nguvu hiyo! Hawana lugha ya ushawishi, no personal vision on how are they going to lead us out of these terrible and unnecessary problems! They simply say VIJANA WENGI HAWANA AJIRA HII NI JANGA KWA TAIFA, the next day watu wanawaona wanafaa kuwa MARAIS by just mentioning the problem without telling us hw are they going to solve it. UKiangalia changamoto zote hizi ndani ya taifa , halafu tunawapa dhamana watu wepesi ambao hawana walilolifanya zaidi ya kutembea na bendera ya Taifa wakati hawana utaifa zaidi ya kutukuza MTOA MLO WAO CCM, napata shaka kama tutafika tunakotaka kufika. Kuna watu wengi tu nchi hii ndani na nje ya ccm ambao angalau wangeweza kutuongoza vizuri, tatizo mfumo wa kiutawala ndani ya ccm hauwapi nafasi sababu SI WATU WA HEWALA! Ili uwe kiongozi ccm , shurti uwe mtu wa YES kwa mabwana wakubwa hata kama wanayosema hayana sense! Ndio maana ni TZ pekee unaweza sikia kiongozi anashinda kwenye uchaguzi kwa asilimia 100%, huu ni utani usio mithilika! Haiingii akilini kwamba watu almost 3000 hakuna hata mmoja anayepingana nao mawazo. Unategemea nini kwenye chama cha jinsi hiyo? Je , unahitaji kuwa na PhD kujua hiki ni chama cha kisanii na cha wanafiki?
 
kinana waziri wa ujenzi! hii siikumbuki kama imewahi kutoka hapa tanzania labda umechanganya taarifa kamanda,jipange

Labda kama kulikuwa na Abdulahman Kinana mwingine, lakini jina hili na kashfa hii haijaondoka kichwani mwangu, yalisemwa mengi tu, si mbali sana kutoka kipindi cha Akina Mwingira kununua dege kubwa baada ya kutua tu halikuruka tena kitendo ambacho kilimpa rejection serikalini for good.
 

kinana alikua waziri wetu wa ulinzi mzee sio ujenzi labda vidole vimekuteleza ulinzi ukasema ujenzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…