Makundi 4619,
Mimi sio kiongozi wa CCM, sina hata ujumbe wa shina, ni mwanachama tu wa CCM lakini utambulisho wangu kwanza ni Utaifa kupitia kadi ya kupiga kura, suala la CCM huja baadae; Ndio maana hata katika uchaguzi wa ubunge 2010 nilimpigia kura Halima Mdee (Chadema) kwani mgombea wetu CCM Angela Kiziga, sikuona kama alikuwa anatosha kuliko Halima Mdee; Lakini ngazi ya Urais, nilimpigia Kikwete kura yangu hasa kutokana na uelewa wangu kwamba, failure zake kipindi cha 2005 2010, zilichangiwa sana na hujuma za watendaji!
Nilianza kuvutiwa na siasa za Dr. Slaa baada ya 2010, ingawa mimi bado ni mwana CCM; Navutiwa sana na siasa zake za kistaarabu, kwani ingekuwa ni mtu mwehu, baada ya 2010 nchi hii isingekalikai; Tunahitaji Kiongozi wa namna hii, na ikifika 2015, iwapo Dr. Slaa atakuwa mzima wa afya, ana kura yangu, au Lissu, unless CCM ije na jina lenye uwezo, na majina hayo yapo ila kwa siasa zetu, so far nadhani yatapigwa tu chini; Na hii inaniingiza kwenye point yangu ya msingi kujibu swali lako kuhusu Kinana na Mangula;
Watu hawa wawili nadhani wameitwa kujakusaidia CCM ipate mgombea anayekubalika na jamii, sio anayekubalika na Chama; Again, kwa mtazamo wangu kama mwanachama, CCM sisi tunaweka sana ushabiki mbele kuliko chochote; Utamaduni wetu umekuwa ni kuheshimu, kusujudia na kutii cheo cha mtu au kiti, hatuangalii au kupima uwezo wa mtu anayeshikilia kiti, tunaangalia zaidi madaraka yake na kumpigia vigele gele kwa wingi tukisindikizwa na nyimbo za Komba; ndio maana viongozi wengi wa CCM wakistaafu tu, wanapoteza mvuto na pia heshima ya wanachama wa ccm, kwani walikuwa wanashabikia kiti (sio mtu), lakini vile vile kitaifa viongozi wengi wakistaafu wanaondoka na heshima zao; Ni mara chache sana kwa CCM kuwa na viongozi bora, wengi ni bora viongozi, na tena ukiwa ni mteule wa Rais au Kipenzi cha cha mwenyekiti, hata kama hauna uwezo, wewe tayari wanachama wanakuona ni mungu mtu; Sasa Mangula na Kinana hawa wakiwa miungu mtu, haitatokana na sababu nyepesi tu kwamba wanapendwa na mwenyekiti, bali umungu mtu huo kama wataupata ni kutokana na track record yao ya utendaji;
Ndio maana Kinana na Mangula ni tofauti bora viongozi ambao nimewajadili hapo juu kwani wakiwa hata nje ya chama umuhimu wao kwa CCM bado unakuwepo; Kwa mtazamo wangu, Kinana, Mangula, wote waliamua kustaafu kutokana na Siasa Uchwara za CCM, lakini wameamua kurudi baada ya kuhakikishiwa kwamba chama kitarudi kwenye mstari na wao watakuwa mstari wa mbele kwenye project ya kufanikisha hilo; Ni sahihi kwa wao kukubali kurudi kwani hawakukimbia chama bali siasa zake uchwara; nadhani wameahidiwa kupewa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha hii project, vinginevyo sidhani kama wangekubali kwani wanajua wazi kwamba waliondoka au walikuwa waondoke kweney uongozi wakiwa bado wana heshimika, ni kama Kobe Bryant Kustaafu leo, ataondoka akiwa bado yupo juu, na wanajua kwamba bila ya uangalifu, kurudi kiholela holela, heshima yao waliyojijengea over the years ingekuwa eroded right away;
Tukubali tu ukweli kwamba Mwenyekiti ameshindwa kutibu majeraha ndani ya chama na ndio maana ameona awaingize hawa watu; Lakini mimi nina tatizo kidogo juu ya hili na nitarudia tena:
Jimwili hili linaloitwa CCM limefanyiwa marekebisho kwenye kichwa, lakini shingo ambayo ndio hugeuza kichwa kushoto, kulia, juu, chini, shingo ambayo hutikisa kichwa kuitikia ndio au hapana, shingo hii imebakia intact; Licha ya kichwa kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale kama vile macho, pua, masikio,n.k, shingo ile ile na bado itaendelea kugeuza kichwa kwa jinsi inavyotaka, na nadhani tunajua shingo ni kina nani katika muktadha huu; Changamoto kubwa ya Kinana na Mangula ni kukabilianana shingo hii, na nadhani aidha hawakulitazama hilo, au wameona ni jambo rahisi kulirekebisha, we dont know, time will tell;
Vinginevyo kuhusu uteuzi wa Kinana na Mangula, Kikwete has done the right thing, lakini sina uhakika kama he has done things right kwani maneno yake kwenye hotuba ya ufunguzi juzi Dodoma kidogo yalinishtua pale aliposema kwamba tatizo la CCM ni makundi kugombea Urais, nje ya hapo, Chama hakina tatizo lingine lolote ambalo ni kubwa; Mimi naamini CCM ina matatizo makubwa zaidi ya haya makundi kwani inakabiliwa na ombwe la itikadi, haina dira, imesaliti historia yake (ya TANU), na azimio la Zanzibar lililouwa azimio la Arusha mwaka 1992 limefungulia mlango wa SOKO HURIA HOLELA & UFISADI kwani mpaka leo, CCM kama chama hakina sheria au kanuni yoyote yenye meno kudhibiti mapungufu ya soko huria ambayo yanazidi kuumiza wananchi, au mapungufu ya azimio la zanzibar ambalo linatoa mianya kwa viongozi kufisadi nchi; Ni kama vile CCM imeamua kuachia kanuni ya laissez-faire itawale katika kila kitu ndani ya nchi yetu;