Hapa kuna ukweli wowote? Tusaidiane tafadhali!

Mi mtu wa February ila sidhan kama ni beautiful katika maisha....au sijaelewa inamaanisha nini
 
31/12

shughuli yangu wanaijua mtaani kwetu
nahisi kuna ka ukweli kuhusu mwezi wangu wa kuzaliwa
 
Miezi ya Kuzaliwa kwa Watu na tabia zao za ukweli na za asili ambazo 100% zimethibitishwa kuwa ni kweli.

January - Most Wanted
Ukitaka kuwatafuta ' Wasiojulikana ' au Watu wenye ' Maasi ' mengi wengi utawapata mwezi huu.

February - Beautiful
Ni Watu wazuri wazuri hasa katika maisha.

March - Attractive and Charismatic
Ni Watu wenye mvuto na karama fulani ambayo wamejaaliwa na Mwenyezi Mungu na chochote kile wakifanyacho kitakubalika tu huku wakiwa na ushawishi mkubwa na uliotukuka katika maisha. Kama ukiwa umekasirika au umeudhiwa au umeboreka au huna furaha fanya upesi sana kaa karibu na Mtu unayemjua amezaliwa huu Mwezi utafurahi mwenyewe na roho yako. Wachekeshaji wengi wazuri na wenye Vipaji huzaliwa huu Mwezi japo miezi mingine hubahatisha.

April - Faithful
Hapa huwezi kukuta Mtu mwizi au msaliti kwani hawa ni Watu waaminifu mno Kimaisha

May - Caring
Hawa ni Watu ambao wanajua mno Kujali wenzao hasa pale wakigundua fulani hana furaha au amani na huwa hawachoki kumjali Mtu.

June - Player
Kama ikitokea tu unatafuta ' Tapeli ' yoyote aliyetukuka duniani usihangaike sana kwani wengi wao wanapatika katika huu mwezi. Hawa wanaweza wakakutapeli huku Wewe unayetapeliwa ukawa unawachekea na ukiwaamkia Shikamoo. Na hata kama ikitokea tu umeibiwa kitu chochote kile hakikisha ' Suspect ' wako wa Kwanza awe Mtu aliyezaliwa huu Mwezi kwani wana ' Kipaji ' pia cha Uwizi pamoja na mwenzake Udokozi.

July - Loving
Wana Upendo sana kwa Watu wote.

August - Hot
Hapa ndiyo makao makuu ya Watu wenye ' Hasira ' sana na ukiwa nao Watu wa Mwezi huu uwe pia tayari muda wowote Uso wako ' Kuumuka ' kwa Manundu yatokanayo na Ngumi za uhakika.

September - Gorgeous
Kama ukiwa labda unatafuta mwenza wako awe wa Kiume au wa Kike mwenye mvuto zaidi na aliye vizuri Kimapenzi / Kimahaba Kitandani basi usihangaike sana Wewe ' Jipendekeze ' tu au ' Jigongegonge ' kwa waliozaliwa huu mwezi utapata raha na utamu wa Mkuyenge au Mbunye.

October - Lovely
Hawa Watu wana tabia ya Kung'ang'ania Kupenda na usiombe upendwe na Watu waliozaliwa huu Mwezi utajuta kwani wanaupendo ambao baadae hupelekea kuwa ' Kero ' kwa Wewe uliyependwa au aliyekupenda. Na wale wanaojiua sana na Kuumizwa na Mapenzi wengi wao huzaliwa huu Mwezi.

November - Amazing
Hawa ni Watu wenye ' vituko vituko ' sana maishani na usishangae Mtu wa Mwezi huu akakunyooshea ' Bastola ' halafu akakupiga nayo ya ' Ugokoni ' kisha hapo hapo akakuomba radhi huku akiwa analia. Hawa hawaoni hata ' aibu ' Kujamba mbele ya Wakwe zao na wakiulizwa Wewe umejamba akakubali ndiyo. Wana maajabu mengi mno wengi wao ' mishipa ' yao ya haya / aibu ilikatwa wakiwa Wodini wakati wanazaliwa.

December - Genius
Hakuna Watu ambao ni Werevu / Vipanga duniani kama ambao wamezaliwa huu Mwezi na kama Wewe una Mtu aliye karibu nawe hapo aliyezaliwa huu Mwezi halafu hana akili basi jua pengine huyo atakuwa si Binadamu wa kawaida na pengine unakaa hapo na ' Jini ' bila Wewe kujua. Ni Watu wenye upeo mkubwa na hili halina ubishi.

Naomba mirejesho yenu tafadhali juu ya miezi mliyozaliwa ili kuanzia sasa tukiujua Mwezi wako na maandiko yako humu wala tusiwe tunapata ' taabu / shida ' ya Kukutafakari kwani tutawahi tu kuchungulia katika huu ukweli.

Nawasilisha.
Mtoa mada hili halina ukwel wowote...ni takwimu iliyotolewa bila research yeyote ni m2 kakaa 2 na kuandika
 
Akuna ukweli katika hilo mkuu,mi nimiongoni nilio zaliwa ndani ya Oct/15.rakini cjawa kupenda wala kupendwa.na hata nikiwa na rafiki wa atuelewani kabisa,tens namashaka na tabia hii cjui kama nitakuja KUOA.mana wanawake PASUA KICHWA.
 
mwezi wangu kuna ukweli :). kwa mwezi wa March umeelezea sifa zao vyema ila kwenye mahusiano ni wagumu kucommit ni raha kuwa nao kama marafiki tu wana natural charm.
 
Oyoooooo February

Michael Jordan born on Feb
Rihanna born on Feb
Cr7 born on Feb.
Goldie born on Feb....
 
mwezi wangu kuna ukweli :). kwa mwezi wa March umeelezea sifa zao vyema ila kwenye mahusiano ni wagumu kucommit ni raha kuwa nao kama marafiki tu wana natural charm.

Naona Mkuu umeamua bila uwoga wala aibu ' Kutuchana ' tuliozaliwa mwezi ' March ' haswa. Haya bhana!!!!!!!
 
August nimetishaaaaa

Halafu kuna kitu kingine nilisahau wa waliozaliwa huo mwezi wa Nane ( 8 ) August kwamba pia wana ' Roho Mbaya ' sana, Wauwaji na Wakatili. Ni hayo tu Mkuu na hongera kwa Kuzaliwa mwezi August.
 
Halafu kuna kitu kingine nilisahau wa waliozaliwa huo mwezi wa Nane ( 8 ) August kwamba pia wana ' Roho Mbaya ' sana, Wauwaji na Wakatili. Ni hayo tu Mkuu na hongera kwa Kuzaliwa mwezi August.
Wala hujakoseaa kuna kipindi huwa nataman kumuua x wangu
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom