KERO Kuna changamoto ya VERIFICATION ya Vyeti vya NDOA Ruangwa

KERO Kuna changamoto ya VERIFICATION ya Vyeti vya NDOA Ruangwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Napatikana Wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi ,nilifunga ndoa mwezi wa pili mwaka huu, hapa hapa wilayani, na cheti cha ndoa tulipata hapa hapa, cha kushangaxa ni kwamba ukitaka kujisajili na mifumo ya serikali kama vile bima ya NHIF inataka uwe na mamba ya uthinitsho wa ndoa.

Namba hiyo ni kama Verification ya cheti cha ndoa, hilo sio tatzo sana, ingawa cheti unacho , itakubidi ulipie Jumla ya shilingi elfu 90 za kitanzia ili kupata namba hiyo na ni malipo ya serikali, unapewa control namba unalipia hiyo sio shida pia.

Sasa process zote hizo nilifanya tangu mwezi wa nne mwaka huu, cha kushangaza ni kwmba hadi leo ukiwapigia simu pale wilayani , wanasema namba hiyo ya verification bado , kitu ambacho kinachelewesha shughuli nyngne ziemdelee kma vile kupata bima ya mke wangu na matibabu, ,kuna uzembe unaoendeleq kuhusu hii process nzima ya verification.

1)Kwanza nahoji, kwanini tunalipia pesa ili kuthibitisha wakati cheti tumepatiwa na serikali hio hio, na

(2) Pili miezi 6 imepita mpaka sasa verification haijafanyika na pesa tumeshalipia , huu ni uzembe au utaratibu upi? Wakati Halmashauri zingne baadh ita watu wakilipia wanapata namba zao ndani ya mwezi tu?


Naomba hili liangaliwe na uhakika sio Tanzania nzima, kuna uzembe fulani kwenye Halmashauri husika unaedelea
 
Huu ujinga nimekutananao na mpaka sasa nimeliwa 50k yangu na sijapata cheti hicho wala verification number. Ila nashukuru nimefanikiwa kupata NHIF ya wife, Manager wa Mkoa hapa alinisaidia.. RITA hawafanyi fair kabisa hawa watu. Ety wamenikula 50k yangu halafu wanataka nilipie tena 40.
 
Huu ujinga nimekutananao na mpaka sasa nimeliwa 50k yangu na sijapata cheti hicho wala verification number. Ila nashukuru nimefanikiwa kupata NHIF ya wife, Manager wa Mkoa hapa alinisaidia.. RITA hawafanyi fair kabisa hawa watu. Ety wamenikula 50k yangu halafu wanataka nilipie tena 40.
Hawafanyi fair kabisa, sijui changamoto yao ni nini haswa!
 
Nadhani haijakaa sawa, yaani mamlaka ya Serikali ndiyo imetoa cheti husika, kisha unaambiwa ulipie tena fedha ili mamlaka nyingine ya Serikali kutoa verification nao. Kwakweli hili jambo lina ukakasi sana na halina afya kabisa. Tunakwamishana sana kwakweli
 
Back
Top Bottom