Hapa kuna ndoa kweli?

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Ni msichana wa miaka 21 mwenye mpenzi wa kiume mwenye miaka 32. Wapo mikoa tofauti jambo ambalo kuonana kwao inaweza kuwa ni mara moja kwa mwaka.

Mara kadhaa msichana amegundua kuwa mwanaume si mwaminifu kutokana na mara kwa mara kutafutwa na wanawake wengine baada ya wanawake wa jamaa kufuma sms za huyu aliye mbali.

Kubwa zaidi msichana amegundua kuwa mwanaume huyu amekuwa na mahusiano na mwanamke ambaye wapo kwa muda mrefu sana tangu enzi za kusoma hadi leo.

Msichana wa 21 years alipogundua hilo, mwanaume akaomba msamaha kuwa amekosea lakini yeye anamchagua huyo binti wa 21 na hamtaki huyu waliyedate naye kwa muda mrefu.

Binti aliongea na mwanamke wa mkaka huyo na akamjulisha kuwa wanagombana sometimes lakini hawajawahi kuachana na hilo halipo. Pia ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa, ni kawaida ya mwanaume huyu kuwa na tamaa ila anapomaliza haja zake uwa anarudi kwa mwanamke wake ambaye wamevumiliana kwa shida na raha ingawa hawajaoana.

Binti wa 21 years yupo njia panda. Anadai yeye yuko mbali na haoni umuhimu wa kuwa huyu mwanaume ukizingatia kwa sasa anasoma mwaka wa mwisho.

Mwanaume amekazana kuomba msamaha sana kwa binti.

Ushauri wenu ndugu zangu.

Pia soma: Ukaribu unaua hisia (Mapenzi ya mbali yananoga)

Wanawake: Madhara ya Mapenzi ya Mbali, Kuweni Makini na Mapoozeo!
 
Red flags kibaoooooo!
Bado tu binti anaomba ushauri?

Ana options mbili;
1.Aendelee nae, ila ajue mwanaume wake ni MALAYA, MBWA... Asitegemee kuwa atabadilika kwenye ndoa au popote pale, na asije kusumbua watu/wazee/wachungaji kila siku kuomba kusuluhishwa/ushauri.

2.Akimbie fasta, asigeuke nyuma.
 
Hivi unategemea majibu ya positive kwa mwanamke alieachwa juu ya ex wake? Tena anakupa muda wake wa kuongea na wewe juu ya ex wake na tabia zake za kumuacha na kumrudia.


Mbuzibee 🐐
 
Hivi unategemea majibu ya positive kwa mwanamke alieachwa juu ya ex wake? Tena anakupa muda wake wa kuongea na wewe juu ya ex wake na tabia zake za kumuacha na kumrudia.


Mbuzibee 🐐
Mkuu naona hata mwanamke angenyamaza hizo tabia mbovu zinaonekana ziko wazi. Mfano kama nimeelewa vizuri binti analalamika kuwa ameshatafutwa sana na wanawake baada ya jamaa kukutwa na msg na wanawake zake.

Thats means hata huyo mwanamke ambaye yupo wote tangu... naye anadanganywa kama binti ama pengine hajamuacha huyo mwanamke kwa kuwa anaweza kumvumilia.

Hakuna malengo hapo. Mwanaume anaonekana bado ni mvulana na hajielewi.

Dada acha kuingilia mapenzi ya namna hii na hivi uko mbali utakuja kushangaa jamaa ameshaanzisha familia na huna la kumfanya.
 
Red flags kibaoooooo!!!
Bado tu binti anaomba ushauri?
Ana options mbili;
1.Aendelee nae, ila ajue mwanaume wake ni MALAYA, MBWA... Asitegemee kuwa atabadilika kwenye ndoa au popote pale, na asije kusumbua watu/wazee/wachungaji kila siku kuomba kusuluhishwa/ushauri.
2.Akimbie fasta, asigeuke nyuma.
Hivi hakuna neno jingine zaidi ya hilo la mbwa??
 
Back
Top Bottom