Hapa kuna future kweli?

amazon

Member
May 30, 2012
55
13
Habari zenu wana MMU?
Mimi ni dada ambaye nimepata mpenzi kama miezi mitatu hivi imepita. Kitu kinachonifanya niombe ushauri wenu ni kwamba, huyu kaka kwanza mawasiliano yake sio mazuri ni mpaka nimuanze na hata nikimtext anachukua kama masaa mawili ndio anajibu meseji.. Anajitetea kwamba yuko bize sana. Anapafahamu ninapoishi na huwa anakuja kunitembelea lakini ninapomwambia anipeleke kwake anasema atanipeleka kwa sasa ni mapema mno kufanya hivyo.

Kitu kingine nilipomueleza kwamba mimi niko serious na huu uhusiano, akaniambia kwa nini tusichukulie kama tuu tunastareheshana isitoshe tuna muda mfupi tangu tumeanza hivyo tusiji commit mapema! Na akanieleza nisipende sana mambo ya kuolewa kama vipi tuzae tu.

Napata wasiwasi na huyu kaka kama kweli ana mpango na mimi. Naombeni ushauri wenu maana nimeshaanza kukata tamaa..
 
BUT still miezi mitatu ni mapema mno kumlazimisha mtu alete posa au a behave like husband to be..
mwache akusome kwanza
au tafuta mwenye 'deperation ya ndoa' kama wewe

mpe mtihani mmoja tu
no sex untill ujue anaishi wapi
hapo utapata jibu
 
jiongeze, kama unataka ndo kimbia ila kama unataka good tyme kula bata mtoto.
 
mnh hata kama ni mapema,huyo ni player anakaba pande zote ili usipate ushahidi kuwa ni player/part time....achana naye huu muda unaopoteza na huyo mpuuzi ujue unajizibia chances zako za kumpata mtu/mr right......
 
Asante The Boss, nitafuata ushauri wako
 
jiongeze, kama unataka ndo kimbia ila kama unataka good tyme kula bata mtoto.

Tatizo nimekufa nimeoza, halafu ndio mwanaume pekee aliyekubali tukapime Afya. Wengine nilikuwa nawaacha maana hawakutaka kupima VVU.Hivyo nilimuona anajali.
 
kwani kinahusika na commitment?
we wote ukliowahi kuwagaia illikuwa ni commitment?
hujawahi kugawa for pleasure?

hapa najaribu kuunganisha....kama keshatoa kipapa....na pozi ndo hizo.....mbona ni alama rahisi sana kuzielewa.....
 
mnh hata kama ni mapema,huyo ni player anakaba pande zote ili usipate ushahidi kuwa ni player/part time....achana naye huu muda unaopoteza na huyo mpuuzi ujue unajizibia chances zako za kumpata mtu/mr right......

Asante Neema. Nyumbani kwake hajanipeleka lakini huwa ananikaribisha Ofisini kwake. I know where he works. Ananiambia ananisoma hivyo atanipeleka kwake when the time is right.
 
Tatizo nimekufa nimeoza, halafu ndio mwanaume pekee aliyekubali tukapime Afya. Wengine nilikuwa nawaacha maana hawakutaka kupima VVU.Hivyo nilimuona anajali.

aisee kumbe kupima afya siku hizi dili sana?
nitaanza na mimi hii style lol
 
hapa najaribu kuunganisha....kama keshatoa kipapa....na pozi ndo hizo.....mbona ni alama rahisi sana kuzielewa.....

wewe hujajibu swali
umeshawahi for pleasure?
kama bado niku pm
upate experience ya 'sex ya bila kudanganywa kuna commitment'...lol
 
Kwa kweli The Boss ni muhimu sana maana wanaume wengi hawataki hii kitu kabisa ya kupima, wanaogopa

kuwa makini saana
mtu kama kicheche hata kupima sio ishu
usisahau virus vina mda wa kutoonekana
unaweza pima na usione hadi miezi ipite
 
dada yangu kwan kwake anaishi na wazazi wake kiasi akikupeleka atakuwa amekupeleka kwa wazazi?kama ndio hata akuonyeshe basi kwa mbali upaone angalau..mhh huyu ameshakwambia uchukulie km mnastareheshana sasa unasubiri nini kwake km unataka ndoa??kuwa serious na maisha yako..mtafute mtu sahihi kwa mtazamo wangu huyu hakuna kitu...
 
he he he, pole.
Una miaka mingapi?

Maplayer wengi wanakubali kupima ili wafaidi zigo na uwaamini zaidi.

Strategy, strategy strategy.

Tatizo nimekufa nimeoza, halafu ndio mwanaume pekee aliyekubali tukapime Afya. Wengine nilikuwa nawaacha maana hawakutaka kupima VVU.Hivyo nilimuona anajali.
 
kuwa makini saana
mtu kama kicheche hata kupima sio ishu
usisahau virus vina mda wa kutoonekana
unaweza pima na usione hadi miezi ipite

Asante The Boss.. Inawezekana kweli akawa ni kicheche maana ninachojua mkiwa wapenzi kuna ile mawasiliano ya mara kwa mara. Mi ndio huwa naanzisha mawasiliano..Najiuliza sana kama ananipenda kweli. Ingawa yeye anasema ananipenda ila tatizo alishatendwa hivyo anaogopa kukurupuka wakati huu..
 
he he he, pole.
Una miaka mingapi?

Maplayer wengi wanakubali kupima ili wafaidi zigo na uwaamini zaidi.

Strategy, strategy strategy.

Asante my dear! Naanza kufunguka. Nashukuru sana kwa JF kwa kweli.. Itabidi nianze kujipanga upya.
 
wewe hujajibu swali
umeshawahi for pleasure?
kama bado niku pm
upate experience ya 'sex ya bila kudanganywa kuna commitment'...lol

na pia hujaelewa jibu....suluhisho hapa sio mimi kutoa au kutokutoa uroda.....ni hivi.... amazon dia....kuna wanaume wanyenyekevu sana kabla hajakumega.....hiyo kupima sio ishu.....shida yake akishakupata ndo ntolee......stuka....
 
Last edited by a moderator:
na pia hujaelewa jibu....suluhisho hapa sio mimi kutoa au kutokutoa uroda.....ni hivi.... amazon dia....kuna wanaume wanyenyekevu sana kabla hajakumega.....hiyo kupima sio ishu.....shida yake akishakupata ndo ntolee......stuka....

siku hizi una busara hadi basi..
 
Back
Top Bottom