Hanspope atua katika ‘Mikono salama’; Mahakama ya Kisutu yamwachia kwa dhamana...

Usiku ulikuwa mrefu, hatimaye kumekucha. Katua, kanaswa! Wanaye...

Tutarajie nini kitafuata?

========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (13:30hrs)
========
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ameachiwa kwa dhamana baada ya kufikishwa Mahakama ya Kisutu kujibu mashtaka 10 yanayomkabili

========
UPDATE: Oktoba 16, 2018 (9:30am)
========

Baada ya kumsaka kwa muda mrefu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Takukuru imemkamata Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hanspoppe alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.

Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.

“Na vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata. Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani kesho (leo).”

Pamoja na Hanspoppe, mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Franklin Lauwo ambaye naibu mkurugenzi huyo wa Takukuru alieleza kuwa amekwishawasiliana nao na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya kurejea nchini akitokea Pakistan.

Hanspoppe ataunganishwa katika kesi inayomkabili rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ya madai ya kughushi na utakatishaji fedha ambayo inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
Safi sana, kwaTZ ya leo wapigaji wote wataucheza mziki wa JPM.
 
Singh Seth huwezi kumlinganisha na Hans Pope ambae ni mjela-jela wa kitambo. Singh hajawahi kupitia shuruba zozote maishani, hajawahi hata kufanya kazi za kuajiriwa, Hans Pope alikuwa mjeda, tena sio mjeda wa kizembe, this combat veteran tried to enforce term limits wakati wa udikteta wa Mwalimu, do you know how much of a ballsy man you have to be to even think of doing that?

Makamishna wa Magereza wa sasa walikuwa sekondari wakati Hans Pope anaingia Keko, maaskari jela walikuwa hawajazaliwa, walipomtema jela he picked himself up from the muck and built a multi million dollar business in oil industry, jamaa ni mjeshi in the truest sense.

Leo unamwambia akaishi Jamaica sijui North Korea kukimbia kesi ya kodi ya kubambikwa? Sio Hans Pope.
hakuna mtu yeyote bongo anaweza kuidindia system ikimuhitaji.. ukiona unafanya vitu wanakuacha ujue hapajawa na ulazima wa kukuchukua, hiyo hata hanspope anajua
 
hakuna mtu yeyote bongo anaweza kuidindia system ikimuhitaji.. ukiona unafanya vitu wanakuacha ujue hapajawa na ulazima wa kukuchukua, hiyo hata hanspope anajua
Ni kweli kabisa, na si bongo tu ,nchi yoyote ile system ni kitu kingine, hasa wakiwa na shida na wewe
 
hakuna mtu yeyote bongo anaweza kuidindia system ikimuhitaji.. ukiona unafanya vitu wanakuacha ujue hapajawa na ulazima wa kukuchukua, hiyo hata hanspope anajua

wapi nimesema system ikikuhitaji itashindwa kukuchukua?

au ni wapi nimesema Hans Pope kuna vitu anafanya wanamwacha?
 
Kesi ambazo serikali inapoteza muda ni pamoja na hii pamoja na ya Habbider na Ruge. Mwisho wa siku hizi kesi wahusika watashinda. Ximefungukia kwa mbwembwe bila kuhusisha akili timamu
acha serikali ipoteze muda ila siku inamalizana nao sidhani kama yule mhindi atakanyagisha puto lake kwenye ardhi ya ukanda wote wa EA tena
 
nataka kujua hasa kwanini unamuita combat veteran?

well, combat veteran ni mtu aliyetoka vitani. Anaweza kuwa kuruta, generali, mgambo, raia, in fact Tanzania ilituma raia wengi kuliko askari Kagera. Umeniuliza alikuwa na cheo gani jeshini, captain, for what it's worth.

Sasa huyiu askari mpiganani ambae amelala magereza yote ya Tanzania tokea akiwa na miaka ishirini-na unamwambiaje aende Jamaica kukimbia kesi ya kizushi ya kodi ya kununulia majani ya uwanja? Especially mtu ambae familia yake ilimwaga damu kwa nchi hii, baba yake alichinjwa Uganda kwa sababu ya bifu za Nyerere na Amin mwaka 72 baada ya kutekwa akikagua mipaka Kagera akiwa RPC, miaka 6 kabla ya vita yenyewe... Hawezi kwenda Jamaica kuogopa udikteta wa visasi, mtu ameshawahi kwenda jehanum na kurudi.
 
unaweza ku guarantee usafi wake?
 
Back
Top Bottom