Hata kama hayakufanyika, ufafanuzi gani unaotakiwa? Kama yamefanyika, ndio swala limemalizika. Kama hayakufanyika, hakuna uhamisho hapo. Jawabu ya hayo wanayo FUFA wenyewe. Hakuna namna yoyote ambalo jambo hili lingeizidi FUFA kiasi cha kutaka ufafanuzi FIFA. Nina mashaka hata kama ufafanuzi huo umetakiwa kweli. Ni waandishi tu kujaribu kulikuza hili jambo ambalo alhamdulillahi, linauza kweli magazeti yao!Kama yote hayo yamefanyika kwa nini FUFA wanataka ufafanuzi kutoka FIFA?
Hata kama ni kwa kilugha cha kabila la mgombea tu?Suala la okwi kusaini yanga iwe halali au si halali nadhani viongozi wa simba na kamati yote ya utendaji wanapaswa kuondoka. Ninavyojua fifa huwa hawacheleweshi kutoa maamuzi sasa siku zote viongozi walikuwa wapi wakati walishasema pesa ya okwi italipwa mwezi september mwaka huu. Na waandishi wa habari wa tz wanazo hizo kumbukumbu mpaka picha za viongozi wawili wa simba wakitoka makao makuu ya etoile du sahel kudai hizo pesa zilikuwa magazetini(tunaomba mtuwekee maana wengine tushachana yale magazeti). Ni mara ya kwanza kusikia eti mchezaji anauzwa bila hata kulipwa advance. Na huu nahisi ni mwanzo tu hata kapombe nafikiri itakuwa ni bongo movie part two ya hii sinema ya okwi. Ukweli unauma ila mimi kama shabiki wa simba nasema viongozi wetu wanzungumza sana kuliko vitendo na ninaomba kwenye mkutano mkuu wa katiba kipengele cha sifa ya uongozi kiwe kujua kusoma na kuandika tu ili dalali arudi tuanze kufurahi kama zamani.
Huyo kapteni kila msimu anapigwa bao kuanzia Yondani,Twite ,Ngasa.Anachoweza ni kununua magarasa
hayo magarasa anayonunua nyie ndo mnakuja baadae kuyalaghai kwa pesa na nyumba na kuyanunua?? timu nzima ya yanga haina scout team yani wanasubiri simba watafute wao waje na pesa zao za unga kuja kuhujumu
Suala la okwi kusaini yanga iwe halali au si halali nadhani viongozi wa simba na kamati yote ya utendaji wanapaswa kuondoka. Ninavyojua fifa huwa hawacheleweshi kutoa maamuzi sasa siku zote viongozi walikuwa wapi wakati walishasema pesa ya okwi italipwa mwezi september mwaka huu. Na waandishi wa habari wa tz wanazo hizo kumbukumbu mpaka picha za viongozi wawili wa simba wakitoka makao makuu ya etoile du sahel kudai hizo pesa zilikuwa magazetini(tunaomba mtuwekee maana wengine tushachana yale magazeti). Ni mara ya kwanza kusikia eti mchezaji anauzwa bila hata kulipwa advance. Na huu nahisi ni mwanzo tu hata kapombe nafikiri itakuwa ni bongo movie part two ya hii sinema ya okwi. Ukweli unauma ila mimi kama shabiki wa simba nasema viongozi wetu wanzungumza sana kuliko vitendo na ninaomba kwenye mkutano mkuu wa katiba kipengele cha sifa ya uongozi kiwe kujua kusoma na kuandika tu ili dalali arudi tuanze kufurahi kama zamani.
Okwi si mchezaji wa
Simba, inashangaza kuona Kapteni anajitia kimbelembele, Simba
walishaamuuza bila kujali walipewa pesa au la. Hata kama hawajalipwa ni
uzembe wao ilikuwaje TFF wakatoa ITC kwenda Tunisia kama siyo Rage na
wapambe wake waliothibitisha kumuuza huko. Zaidi ya yote, Simba haina
ubavu tena wa kumzuia Okwi asijiunge na timu yoyote. Wanaoweza kumzuia
ni EdS pekee. Hata hivyo Okwi akiendelea kukipiga Yanga itaathiri nini
Simba kudai madai yao kwa EdS? Kinachowauma Simba ni kwamba hawajapata
hata senti kutoka EdS, Okwi kahamia Yanga wasiyoipenda halafu muda si
mrefu wataanza 'kulokota' mipira kwenye nyavu zao kutoka miguuni mwa
Okwi. Hivi Simba hamkumbuki 'movie' ya Ngassa kutoka Yanga - Azam -
Simba - Yanga, mmesahau eee, kweli mkuki kwa nguruwe kwa mwanadamu
...
Etoile du Sahel walishavunja mkataba kwa kukataa kumlipa mshahara kwa miezi 3 ndipo FIFA ikamruhusu kwenda SCV huku akisaka timu aitakayo hata kama ni Simba, yeye kaamua kwenda Yanga ndipo FUFA bila ajizi wametoa ITC. Kama Simba hawajalipwa pesa na EdS wanaweza kuendelea kudai huku Okwi akiwa Yanga akitupia bao katika nyavu za Simba.
Usahihi upi wa kisheria? Kudai mchezaji asiyekuwa wako?Hans yuko sahihi kabisa kisheria make Okwi si mchezaji wa Villa.
hapo kwenye blue ndipo nimepapenda zaidi japo panawaumiza watani kimtindo
Sisi wana Yanga
tunafahamu sana machungu ya Okwi aliyotutendea, sasa ni wakati wa wana
Simba nao kujua makali yake, kwa aina ya magoli kipa walionao, hakuna
shaka 'watalokota' mipira isiyopungua 6 katika nyavu zao pale hizi timu
zitakapokutana. Nimesikia dogo kawaambia Waganda kuwa anakuja Tanzania
kuifunga Simba bao 6 na hivyo kuweka rekodi ya karne kuwa mchezaji wa
kwanza nchini Tanzania kuchachafya timu pinzani (mtani) kwa nyakati
tofauti kwa bao nyingi. Sasa hii habari ndiyo wana Simba hawataki kabisa
kuisikia. Jana Rage mwenyewe amekiri kuwa taarifa za Okwi kusajiliwa
Yanga hazijampendeza mwana Simba yeyote ndani na nje ya
Tanzania.
Okwi wanayemlilia Simba hivi sasa.unamzungumzia Okwi wa Simba 5 bila au Okwi wa CECAFA CHALENJI
ulichoandika hapa na alichosema Hans Pope na nilivyosmsikia kupitia radio ni tofauti kabisa. Pope amesisitiza Okwi si mchezaji wa Simba na ana haki ya kuuzwa isipokuwa wao kama Simba wanashikana koti na Tunisia ili iwalipe. Sasa haya uliyoyaweka mhhhhh
Kwani Galatasaray wakimuuza Drogba, timu itayomnunua si ndio itakuwa third party? Ilimradi ameuzwa kihalali kwa second party, basi second party ina haki ya kumuuza kwa rhird party, third party kwa fourth party..... Hadi mwisho wa dunia. Sasa utofauti na hili la Okwi ni upi? Lakini unajua kwamba FIFA ni mtandao mmoja ambapo uhamisho hufanyika kwa kutumia Mfumo wa Mlingano wa Uhamisho, Transfer Matching System? Mchezaji yeyote mwenye utata hawezi kupitishwa na mfumo huo, kumbuka Asamoah alivyoshindwa kusajiliwa Yanga mara ya kwanza. Kwa hivyo uhamisho ukifanywa na FA ya nchi yoyote mwanachama wa FIFA, kama huu wa FUFA kwa Okwi, unakuwa umefanywa na FIFA yenyewe. Upo?
Kapombe nae anaenda Yanga..dah!