Hans Poppe: 'Kwa Okwi yanga wameliwa'..!!

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
617
1,000
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Sc ya Dar es salaam,Zacharia Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi,Yanga Sc wameingia mkenge kumsajili Emmanuel Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa nani mtani jembe pekee,lakini zaidi ya hapo hatacheza jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.Kapteni huyo wa zamani wa JWTZ amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoille du Sahel ya Tunisia na hawezi kuchezea Yanga."Mimi sina wasiwasi.naangalia tu sarakasi zao nikiwa najua wataangukia wapi,yule mchezaji yanga wameingizwa mkenge na FUFA(shirikisho la soka Uganda).Kwa sababu Etoille walimtoa kwa mkopo Sc Villa na ndiyo maana hata FUFA walipotaka kumtumia katika CHAN,wakaambiwa haiwezekani kwa kuwa yule ni mchezaji wa Etoille"alisema Hans Poppe.
Mmmh Shughuli ipo!!! pole kwa atakayepoteza!
 
Yombayomba

JF-Expert Member
Aug 23, 2006
818
195
Hans Pope, anawapoza wapenzi wasiulize pesa za uuzwaji wa wachezaji kama Samata, Ochan, na huyu ambazo zote mpaka leo hazijulikani nani alipokea.

Kuhusu Okwi swala lake ni kama la Ronaldinho, aliuzwa lakini timu ikashindwa kumlipa mshahara miezi 6, akafunja mkataba na kuhamia timu nyingine na FIFA ikabariki. Okwi hakulipwa mshahara kwa miezi mitatu, ikapidi arudi kwao na FIFA ikamruhusu kujiunga na Villa, sasa swala la kulipwa pesa linamuhusu vipi Okwi?

Hivi huyu Hans pope ni mzima kichwani kweli???
 
Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
1,500
Etoile du Sahel walishavunja mkataba kwa kukataa kumlipa mshahara kwa miezi 3 ndipo FIFA ikamruhusu kwenda SCV huku akisaka timu aitakayo hata kama ni Simba, yeye kaamua kwenda Yanga ndipo FUFA bila ajizi wametoa ITC. Kama Simba hawajalipwa pesa na EdS wanaweza kuendelea kudai huku Okwi akiwa Yanga akitupia bao katika nyavu za Simba.
 
kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
617
1,000
Tusubiri tuone! Ni kweli Okwi alishindwa kutumika michuano rasmi ya CHAN! Ni kweli alikuwa Sc Villa kwa mkopo!Ni kweli Yanga hawakuwa na ujasiri kutangaza usajili huo mapema! Ni kweli hata dau la $ 20, 000 haliakisi dhamani halisi ya Okwi! Mnnh yaweza kuwa ni mkenge kweli?
 
Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,424
2,000
HANS POPPE AWAAMBIA YANGA SC; “KWA OKWI WAMELIWA”
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi, Yanga SC wameingia mkenge kumsajili Emmanuel Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe pekee, lakini zaidi ya hapo hatacheza Jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza Yanga.
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
HANS POPPE AWAAMBIA YANGA SC; "KWA OKWI WAMELIWA"
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza Yanga.
Aliwezaje kichezea Villa? Kauli hiyo anaisemea Etolie au Simba? Hao Etoile wenyewe hawana mdomo?
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
Tusubiri tuone! Ni kweli Okwi alishindwa kutumika michuano rasmi ya CHAN! Ni kweli alikuwa Sc Villa kwa mkopo!Ni kweli Yanga hawakuwa na ujasiri kutangaza usajili huo mapema! Ni kweli hata dau la $ 20, 000 haliakisi dhamani halisi ya Okwi! Mnnh yaweza kuwa ni mkenge kweli?
Ni kweli Etoile hawakumlipa mishahara yake Okwi. Ni kweli mchezaji asipolipwa mishahara, FIFA inamruhusu kuhamia timu nyingine bila ya masharti. Ni kweli hilo ndilo lililomtokezea Drogba kule China na FIFA kumbariki ahamie Galatasaray kwa sababu hiyo. Ni kweli kwamba ama hukuwa ukiyajua haya au unadanganya umma makusudi kwa utashi wako.
 
Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,424
2,000
Huyo kapteni kila msimu anapigwa bao kuanzia Yondani,Twite ,Ngasa.Anachoweza ni kununua magarasa
hayo magarasa anayonunua nyie ndo mnakuja baadae kuyalaghai kwa pesa na nyumba na kuyanunua?? timu nzima ya yanga haina scout team yani wanasubiri simba watafute wao waje na pesa zao za unga kuja kuhujumu
 
Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,624
2,000
hayo magarasa anayonunua nyie ndo mnakuja baadae kuyalaghai kwa pesa na nyumba na kuyanunua?? timu nzima ya yanga haina scout team yani wanasubiri simba watafute wao waje na pesa zao za unga kuja kuhujumu
Hao maskauti ndio walimdanganya na kuwanunua kina Akufor,Mbiyavanga,Waluya,Ochieng,Shiboli,Henry Joseph,Humud
Mbona huzungumzii Maftaha,Kiemba,Berko,Ngasa,Mapunda
 
TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,798
0
HANS POPPE AWAAMBIA YANGA SC; “KWA OKWI WAMELIWA”
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi, Yanga SC wameingia mkenge kumsajili Emmanuel Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe pekee, lakini zaidi ya hapo hatacheza Jangwani kwenye michuano yoyote rasmi.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza Yanga.

Simba inaubia na Etoile du Sahel? au ndo maana mliwasamehe deni lenu?
 
kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
617
1,000
Ni kweli Etoile hawakumlipa mishahara yake Okwi. Ni kweli mchezaji asipolipwa mishahara, FIFA inamruhusu kuhamia timu nyingine bila ya masharti. Ni kweli hilo ndilo lililomtokezea Drogba kule China na FIFA kumbariki ahamie Galatasaray kwa sababu hiyo. Ni kweli kwamba ama hukuwa ukiyajua haya au unadanganya umma makusudi kwa utashi wako.

Issue ya Okwi inautofauti na ya Drogba, Hapa kuna 3rd part ambaye ni Simba! Na ndio maana hakuruhusiwa kutumika CHAN kama mchezaji wa ndani kutoka SC Villa! Upo hapo! Tusubiri tu.muda utaongea kama ilivyokuwa ile issue ya Ngasa! Mwisho ilibainika kasaini mara 2!!
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
Issue ya Okwi inautofauti na ya Drogba, Hapa kuna 3rd part ambaye ni Simba! Na ndio maana hakuruhusiwa kutumika CHAN kama mchezaji wa ndani kutoka SC Villa! Upo hapo! Tusubiri tu.muda utaongea kama ilivyokuwa ile issue ya Ngasa! Mwisho ilibainika kasaini mara 2!!
Kwani Galatasaray wakimuuza Drogba, timu itayomnunua si ndio itakuwa third party? Ilimradi ameuzwa kihalali kwa second party, basi second party ina haki ya kumuuza kwa rhird party, third party kwa fourth party..... Hadi mwisho wa dunia. Sasa utofauti na hili la Okwi ni upi? Lakini unajua kwamba FIFA ni mtandao mmoja ambapo uhamisho hufanyika kwa kutumia Mfumo wa Mlingano wa Uhamisho, Transfer Matching System? Mchezaji yeyote mwenye utata hawezi kupitishwa na mfumo huo, kumbuka Asamoah alivyoshindwa kusajiliwa Yanga mara ya kwanza. Kwa hivyo uhamisho ukifanywa na FA ya nchi yoyote mwanachama wa FIFA, kama huu wa FUFA kwa Okwi, unakuwa umefanywa na FIFA yenyewe. Upo?
 
Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,496

Unaijua TMS?
 
Masuke

JF-Expert Member
Feb 28, 2008
4,613
1,250

Kama yote hayo yamefanyika kwa nini FUFA wanataka ufafanuzi kutoka FIFA?
 
Joo Wane

JF-Expert Member
Mar 14, 2007
616
1,000
Suala la okwi kusaini yanga iwe halali au si halali nadhani viongozi wa simba na kamati yote ya utendaji wanapaswa kuondoka. Ninavyojua fifa huwa hawacheleweshi kutoa maamuzi sasa siku zote viongozi walikuwa wapi wakati walishasema pesa ya okwi italipwa mwezi september mwaka huu. Na waandishi wa habari wa tz wanazo hizo kumbukumbu mpaka picha za viongozi wawili wa simba wakitoka makao makuu ya etoile du sahel kudai hizo pesa zilikuwa magazetini(tunaomba mtuwekee maana wengine tushachana yale magazeti). Ni mara ya kwanza kusikia eti mchezaji anauzwa bila hata kulipwa advance. Na huu nahisi ni mwanzo tu hata kapombe nafikiri itakuwa ni bongo movie part two ya hii sinema ya okwi. Ukweli unauma ila mimi kama shabiki wa simba nasema viongozi wetu wanzungumza sana kuliko vitendo na ninaomba kwenye mkutano mkuu wa katiba kipengele cha sifa ya uongozi kiwe kujua kusoma na kuandika tu ili dalali arudi tuanze kufurahi kama zamani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom