Handwritten or typewritten?

Handwritten or typewritten?

Sidhani kama hata Serikalini huu ni utaratibu,sasa andika uone pia inavyo kula kwako.
Mtu kaishapiga bia zake halafu umletee muandika wa kulaza sijui kupinda,ataichukua na kuitupilia mbali.
Barua zaidi ya melfu halafu mtu akubali kupata tabu na muandiko wako.Akisoma mstari moja tu akiona macho yanamsumnua anaitupa.
We kumbuka hata wakati tupo shule waalimu siku za mitihani wanasisitiza kwamba,jaribuni kuandika muandiko mzuri,maana wasahihishaji wa baraza la mitihani hawana muda wa kusumbuka kwenye miandiko migum yenye usumbufu,unakuta hata kama umepata vizuri lakini anakukata au anapotezea.
Sasa hata Barua za kazi ni sawa,unawezakuwa una vigezo vyoote,lakini barua yako tu ikakukosesha kazi,Yaani kama ungeona jinsi maboss wanavyokuwa wanazipitia barua basi ungesema kweli kazi ipo.Yaani akiona sehem haielewi vizuri tu basi anaitupa,maana mezani zipo telee zinamsubiri.Ndio maana mfumo wa CV na Oral Interview umekuwa unatumiaka sana kwenye ulimwengu wa sasa.
Kama utaandika kwa mkono na unahisi muandiko wako sio mzuri,basi tafuta mtu mwenye hati nzuri,maana kuna watu wanamiandiko utafikiria Keyboard ipo mkononi,yaani kama mashine kumbe mkono.Ila wengine kama sie basi utafikiria bata kapita.
Mie wakati nasoma nilikuwa namuandiko sio mzuri,ila kuna jamaa yangu alikuwa mkali sana kwenye hati,basi nilikuwa nikimuandikia Barua ya kumtongoza Dem lazima nimpe yeye acopy kwa muandiko wake,Dem akiona hivi anasema duhh unamuandiko mkali kweli,.hahaha Iseee hizi balehe hizi zinapitia mbali sana.
hahahahaha UHAMIAJI ilikuwa vipi?? Maana walikuwa na maombi zaidi ya 20 elfu but walichambua nakumbuka walisema barua ziandikwe kwa mkono pia, so sidhani kama wingi waaplication ni tija but inategemea tu na matakwa ya mwajiriii.
 
kwa nafasi zilizo nyeti hand written, TISS hupewa jukumu la kumchambua mtu kwa maandishi aliyo andika kwa mkono wake na wana uwezo mkubwa wa kumtambua mtu kwa maandishi yake kama ana faa au ni boya!!!!!

Ooh...kwa hiyo hawa obviously wataprefer za mkono si ndivyo?
 
Mkuu vote nyingi zimeenda kwa Mkono,sasa ilikukwepa usumbufu Andika kwa mkono ila angalia muandiko wako kama sio mzuri tafuta mtu akuandikie.
 
Good... hii point nimeiwaza toka last week! miandiko mingine migumu sana kusoma, ni bora iandikwa kwa mashine then sehemu ya signature ndiyo ipigwe ka mkono..
.
handwriting.jpg
 
Sidhan kama barua zinasomwa kweli nadhan kikubwa wanaangalia vyeti tu na experience if any bt ni mubimu kuzingatia maelekezo otherwise iachape tu
 
Wakuu nitoe ushuhuda wangu, tokea hii mada imeanzisha na mimi nilikuwa sielewi haya makitu ila leo nimepata jibu. Niliomba kazi utumish katika idara ya e-governancy, nilichapa barua, sikuandika kwa mkono na nimeitwa kufanya interview tareh 17, Hiyo naweza kusema ukichapa sio vibaya . Pia nilikuwa sijajua kuhusu matumiz ya transcripts bila cheti, sikutuma copy ya cheti cha chuo nimetumia academic transcripts na vyeti vya sekondari. Kitu kingine ni kwamba nilikuwa na wasiwasi kuhusu kuthibitisha vyeti, mim sikuthibitisha copy za vyeti mahakamani na bado nimeitwa.
 
Mkuu abbaczo hilo lipo ila inategemea na busara za mwajiri,sidhan kama kuna utaratib official wa kuandk.
 
Back
Top Bottom