Handbag ya Madam

Aisee umenifurahisha unavyohesabu..Eti Umemkuta mara 15 au mara 13...Kwanini unahesabu kiasi hicho. Unapaswa kumwambia kuwa hupendelei anavyofanya
 
Pole sana, mumeo atakau hajatulia ila wivu unamtafuna, siku zote mwizi hapendi huibiwa, Kuna jirani yangu mmoja, mumewe alikua anampekua hadi kwenye chupi, anamnusa kila kona ya mwili. kumbe yule mwanaume alikua ni mhuni sana huko nje, na katika mawazo yake alidhania kua kile anachokifanya kwa wanawake wengine huko nje ndio hicho hicho anachofanyiwa mkewe na vidume vya nje , aliendeleza ugomvi na wivu usio na maana kwa mkewe, ndugu wamesuluhisha wakachoka, sasa hivi wameshatengana.
 
tafuta namna ya kumfanya akuamini. kuna kitu lazima.
 
Mwanaume anayechunguza handbag ya mwanamke ana tatizo kubwa...mwishoe atakagua make-up zako nk..! si kawaida,mweeeh!
 
ukute kashauriwa na waganga wa kienyeji.............maana siku hizi kuna upuuzi mwingi wa kuleta utajiri. wee unaona bora kipi, akubali kukutoa wewe sadaka, aambiwe asilale kitandani au awe anakagua pochi yako kila siku?
 
bora uwaeleze wanaume wenzangu wenye tabia kama hizi
inakera sana kupekua pochi za mke wako ni aibu pia
lazima ajue wanawake mnahifadhi vitu vingi kwa pochi na ni kama siri yako mwenyewe
huyu alikuwa anapekua hata nguo za mama yake pia.
rafiki yangu alinisimulia alimshauri ndugu yake kutokupekua pochi ya mke wake kwani shemji yake alimshtaki mbele ya wazazi akadai anamuingilia familia yake baada ya kumshauri sio ustaarabu.
kama walivosema kila unapotoka job uwe unampa kabisa apekue
popote unapomkuta mpe kabisa atajisuta ataacha
 
Wengine Hawana hata hao Wa kuwakagua.. Wanagugumia kila siku kusaka hata wa kuwasumbua wanaambulia 'used' .. Amakweli Kazi ukiwa nayo Mbaya ..
 
Why do we all marry?
Because romance is not
the only element of life.
We should also know horror,
terror, suspense, irony,
stupidity & tragedy of LIFE
 
wewe mwache tu aendelee na hiyo tabia,maana ni mwanaume asiyejiamini,na mara nyingi wanaume wenye tabia hii ni wale wenye mahusiano mengine ya nje,anahisi na wewe unatoka nje,wewe wala usimuulize,endelea kumwacha apekue simu na pochi zako, usimuulize tena maana unavyomuuliza ndo kwake yeye anadhani kweli una mambo yako!kupekuliwa ni wengi tu tunafanyiwa hivyo na wala hatukereki maana sina cha kuficha!najiamini!vumilia tu mdogo wangu,wenzio tunapekuliwa hadi visivyosemeka na akimaliza unampa bonge la busu na tabasamu pana!anavimbaje bichwa!
 
ni sawa tu na kupekua sms na phonebook ya simu zako,sasa fanya hivi we ukirudi tu toka job mpelekee pochi mwambie sachi dia
 
naima take it easy, mwenzio nikifika tu kama nimemkuta nambwagia cm naenda jikoni! kama hayupo akinikuta baada ya salam nambwagia cm nakaa mbali naye kabisa. manake sitaki apate tabu nishajua ndio ugonjwa wake kunipekua, lkn nina amani sana wala sioni tatizo. ndio walivyo my dia.
 
Asanteni wote nawashukuru kwa maoni yenu,mbarikiwe sana
 

Hiyo red dah imenigusa mie hutendwa hivyo kila mara mpaka siku hizi vitu vyangu naweka ofisini naacha huko kabisa na hata pesa natembea na ya kutumia siku hiyo hiyo tu
 
Nimekuwa nikifuatilia uzi huu kwa umakini sana, nimefurahishwa na jinsi ya wanandoa walivyofunguka kiufasaha juu ya machungu ya ndoa. Lakini ukiletwa uzi unaosema ndoa ni karaha wataitetea ndoa utafikiri wanazifurahia ndoa zao. Hakuna watu wanafki kama waliyooa/olewa, machoni mwa watu wanajifanya wanapendana, lakini mmh.... Ndoa!!
 
Asante kaka, naona wengi kweli wamenishauri nimpatie kabisa mkoba nitakuwa nafanya hivo

Mmmh! binafsi sikubaliani na ushauri huu, it's like you want to solve a problem by creating another problem, si vizuri kabisa
 
Asipochungulia handbag ya mkewe akachungulie ya mamake ama dada zake? Muache aji-enjoy bwana, mapenzi ni ukichaa. Kama huna cha kuficha, usitie shaka. As long as akimaliza ukaguzi anarudisha kila kitu alivyokuta na anafunga zipu ama bakoli, akhuuu! Muache mtoto wa mwanamke mwenzio akuonee wivu kifaa chake bwana! Wenzio hata wakitoka kazini salamu hawapewi!
 
Hivi unamaanisha? Nikajua unatania aisee! Kwangu hata maid asie muaminifu simuwezi, bora kahaba! Nina colleague anafungiaga hela ofisini ama anatupa tumuwekee. Ila yeye mumewe haibi, anazipangia matumizi! Unakaaje na mwanaume mwizi!!!! Uwiiii! Si unaishi kama stendi!
Hiyo red dah imenigusa mie hutendwa hivyo kila mara mpaka siku hizi vitu vyangu naweka ofisini naacha huko kabisa na hata pesa natembea na ya kutumia siku hiyo hiyo tu
 

My friend I realy mean it my dear take it from me..........ni kero ajabu yaani hata mimi nafungia pesa ofisini maana home hakukaliki pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…