Handbag ya Madam

weka chura umo...akiinvgiza mkono anakutana na kitu kina dank dank bas aatapata mengneo...atakoma
afu atakuona mwanga
 
weka chura umo...akiinvgiza mkono anakutana na kitu kina dank dank bas aatapata mengneo...atakoma
afu atakuona mwanga

mmhh Rose1980 mwenzio akionekana mwanga si ndio mwanzo wa kuachika.. na hivyo unavyokonyeza isijekuwa unataka kuchukua nafasi.
 
Naiman tupo wengi tunaokerwa
na hali hii ,mimi mume wangu ana the same tabia mimi sijawahi kumwuliza
ila naona nitaanza kwani mimi sijawahi hata kugusa pochi yake unless
kama natafuta kitu na awe amenituma

Wategesheeni viwembe wakijikata wataacha.
 
hayupo imara mume wako,na mara nyingi hizo ni tabia za watu wasiojiamini na wanaoshinda vijiweni wakidanganyana upuuzi,mchane tu kuwa wewe sio style za watu anaowadhani hivyo asikuweke kwenye mizani
 
Kuchunguzana kwenye Mahusiano ni jambo la kawaida sana..
Ila sema kuna wengine wanachunguza vibaya hadi kuleta hisia mbaya..
Ninachokiona kwa mumeo ni 'inferiority compex'..kutojiamini..yaan anaogopa hadi kivuli chake..
Na hii inatokana na stori anazoambiwa pengine na marafiki zake kuhusu wake zao..ukumbuke wanaume tunapenda sana kupiga stori sana zinazohusu mapenzi..Ushauri wangu..Nenda nae taratiibu na kama ukija na mkoba mtupie kabisa magotini mwake..yaaan jifanye kama hiyo hali ya kupekuliwa ni sehemu ya maisha yenu..with time atakuzoea...
 
Maumivu ya kichwa huanza taaaratibu.....
 

Sijui aina gani ya uchunguzi wa kizamani anaoufanya huyo bwana, maana hata kama ungekuwa na nia mbaya na tayari umeshamuona akifanya hivyo mara kadhaa sidhani kama ungeweza kuweka kitu kibaya.
Kwa kuwa ni mumeo jaribu kukaa naye chini tena kwa mara nyingine na kumueleza kwa upendo kuwa haufurahishwi na hilo zoezi na kama hautaona mabadiliko kwa sababu wewe hautapungukiwa na kitu, akirudi we mtupie hilo bag lako alikague mpaka achoke ili uilinde ndoa yako.

HP
 

Pole sana dada yangu,jaribu kutafuta muda wewe na huyo mume wako ukae chini umueleze kinaga ubaga the way anavyokukera na hiyo tabia,pia hutaki imani/uaminifu wake kwako aujenge ktk vitu rather akuamini wewe kama wewe cuz kama ushajua anakupekua daily kwenye handbag yako,ana password yako ya fb na yahoo kama ni kumkwepa unaweza kumkwepa tu na wala asijue chochote kwasababu binadamu unavyozidi kumbana/kumfuatilia ndivyo na yeye anavyozidi kutafuta means ya kuescape,pia binadamu hachungwi hivyo kama mnyama,try to convince him,at the end of the day atakuelewa tu.
 
Muosha huoshwa! Alijuaje maji ya asali matamu kama na yeye si muonjaji, sasa kuonja yeye anadhani kila mtu mramba asali??? Wengine huramba mshubiri"!! Anatia aibu na tabia zake mbaya! Mkanyeeeeeee, mwisho atanza kukufuata hata kwenye vikao vya wakina mama mtaani, maana mwana umleavyo dada!! Mkanye mapemaaaaaaaaaa!
 

Anaweza kuwa anakupenda sana au kuna hisia fulani pia kasikia so ndo anafanya uchunguzi! Ila inaonekana ana wivu sana, na vipi kuhusu wewe ukichukua simu yake?
 
Hiyo pochi haina ata vipodozi labda hand lotion tu ambayo ata chumbani ipo

basi kamnunulie na yeye hand bag umpe kama zawadi, huenda ikawa anakutamani sana na hand bag yako, kuna watu wameubwa kutamani vitu visivyotamanika, labda na yeye ni mmoja wao.
 
Hiyo tabia ipo kila upande mimi mke wangu huwa anapenda sana kupekuwa kwenye mifuko yangu ya suruali na kupekua kwenye simu yangu huwa namuacha tu simuulizi chochote, sikuizi naona amepunguza sasa naona ameridhika. Nakushauri dawa ni kumuacha apekue kila anapotaka kupekua wasiwasi wako ni nini kama huna matatizo na unajiamini muache ataridhika na ujue anakupenda sana mpaka anakuwa na hofu ya kuhujumiwa.
 
Mpitanjia, naona huyu mtu kwa hali hii aliyojiwekea inawezekana ata akikaa offisini ananiwazia mabaya tu mda wote, sasa hii hali itakuja kumuathiri bila sababu ya msingi
Ni kweli hali hiyoinaweza kuja kumuathiri... lakini kwa upande mwinginefurahi maana inaonekana huyo jamaa kapenda kweli
 

Bra-joe, tafsiri ya Mke kumnunulia Mume hand-bag au kitu chochote cha kike ni mbaya sana na inaweza kumletea kupewa talaka. Badala ya kupata nafuu ya ndoa, anaweza kujikuta akivunja ndoa yake kabisa! Nashauri asifanye hivyo kamwe!
 
Last edited by a moderator:
Mi nakushauri ukae nae chini muongee kwa upole kabisa bila ishara yoyote ya kukasirika lazima atakupa sababu ya yeye kufanya hivyo na kupekua pochi yako na simu,naamini hakuwa na tabia hiyo mwanzoni au mlipokuwa wachumba.....lazima kutakuwa visababu vya yeye kufanya hivyo anashindwa tu kuuliza ss anatafuta ushahidi,kaa muongee yaishe hataishia hapo huyo......i can say lazima utakuwa ulimpa doubt somewher bila hata ya ww kujua.
 

Kama ni hivyo, ujue inawezekana ni wivu tu hana lolote! Ila nakushauri we jitahidi uendelee kuwa mwaminifu kwake na uwe smart kwa kila ufanyalo (Isije kuwa anatafuta sababu ya kukuchokoza ili atimize malengo yake fulani!) kuanzia simu, hand bag, mitandao ya kijamii nk ili asiwe na sababu ya kukukuta na kosa. Mvumilie na mpe muda baada ya muda fulani atakuja kuprove kuwa huna hicho kitu kibaya anachokitafuta toka kwako. Ila kwenye safari zenu za outing nk jaribu mara kwa mara kumkumbusha kuwa unampenda na yuko pekee yake na wewe upo kwa ajili yake hivyo aendelee kutuliza moyo. :redface:
 
basi kamnunulie na yeye hand bag umpe kama zawadi, huenda ikawa anakutamani sana na hand bag yako, kuna watu wameubwa kutamani vitu visivyotamanika, labda na yeye ni mmoja wao.
Ama kweli!!!!
 

Asante nimekuelewa
 
Bra-joe, tafsiri ya Mke kumnunulia Mume hand-bag au kitu chochote cha kike ni mbaya sana na inaweza kumletea kupewa talaka. Badala ya kupata nafuu ya ndoa, anaweza kujikuta akivunja ndoa yake kabisa! Nashauri asifanye hivyo kamwe!

HP, kipi bora, kuendelea kuishi katika ndoa kwa huzuni na manyanyaso au kupewa talaka na kwenda kuishi maisha ya furaha na huru? Koti hili naona linam-bana huyu mdada ndiyo maana kaja hapa kuomba ushauri, huenda akivuliwa atafurahi.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…