Hana shukrani, hadi yamkute makuu

Hana shukrani, hadi yamkute makuu

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,007
Reaction score
168,592
*CC:
Madame B, cacico, gfsonwin, mwaJ, Mwita Maranya, majany, Kaka Kiiza, Asprin, watu8

Kulikuwa na mwanaume aliyekuwa
anampenda sana mke
wake,Wanandoa walikuwa na
watoto watatu,mwanaume
alijitahidi kumpatia mkewe kila kitu
ambacho kilichokuwa nadni ya
uwezo wake lakini mwanamke
hakuonyesha kujali,aliweza
kumnunulia nguo lakini neno
ambalo mkewe angeweza kulitamka
ni kwamba "si unatimiza wajibu
wako kama mwanaume" muda
mwingine alikuwa akimletea basi
mwanamke anamrushia nguo yake
na kumwambia unaniletea nguo
ambayo haina hata thamani(bei
nafuu) kwani umenionaje?lakini
yule mwanaume alikuwa anacheka
na kumwambia SIKU MOJA
NTAKUWA TAJIRI NA NTAKUPATIA
CHOCHOTE UTAKACHOKIHITAJI
MKE WANGU MPENZI
,yule mwanamke haikuwa kutokea
hata siku moja akampigia simu
mumewe labda itokee anahitaji kitu
toka kwa mumewe na ilipotokea
ombi lake lisipotekelezwa na
mumewe basi kinachofuata ni
ugomvi tena sio wa siku moja,.
Siku moja jion mumewe aliporudi
toka kazini alibeba nyama kilo
moja akitarajia akamsuprise
mkewe,alipofika na kafurushi kake
mkewe akampokea, akaanza
kumfokea eh! eti na wewe unajiita
mwanaume,mwanaume gani?
unabeba hako ka kilo ka nyama
bila mafuta wala vitu vingine?
akachukua kale kafurushi ka nyama
akakatupa jalalani...mwanaume
akajisikia vibaya mno lakini
hakuacha/wala kupunguza mapenzi
kwa mkewe
siku moja mwanaume akajisikia
maumivu mguu wake wa
kushoto,yale maumivu yakazidi
ikabidi aende hospitali
akagundulika anaumwa KANSA
lakini hakuwa na uwezo wa kupata
tiba iliyo nzuri kwa hiyo ile kansa
ikaendelea kumtesa,,lakini
japokuwa alikuwa mgonjwa
hakuacha kuendelea kuihudumia
familia yake kwa kadri ya uwezo
wake ,
miaka miwili baadae hali ikazidi
kuwa mabya zaidi akapelekwa
kwenye mashirika ya misaada
ikabidi akatwe ule mguu,lakini
pamoja na kukatwa haikusaidia
kwani wadudu waliendelea
kumshambulia kwa kuwa alichelewa
kupata tiba ikabidi amuite mkewe
na kumuachia husia mke wangu
"naomba uwatunze wanangu" hapo
hapo akavuta pumzi ya mwisho na
kukata roho,,mke na watoto walilia
sana...
mieiz miwili kupita mke akaenda
kwenye kaburi la mumewe akaanza
kulia huku akisema..."mume wangu
ulijitahidi kadri ya uwezo wako
kunijali na kunipa chochote
kilichokuwa ndani ya uwezo wako
lakini sikutambua thamani yako
hadi ulipokufa,,sasa mimi ndo wa
kuihudumia familia kwa
chakula,mavazi,elimu na
mengineyo,nakumbuka hadi siku
nilipotupa kilo ya nyama lakini leo
sielewi hata pa kupatia walau nusu
kilo ya nyama,,mwanaume
uliyenipenda hata nilipokuonyehsa
dharau nakuomba UNISAMEHE
SANA ,,NIMEKUKUMBUKA MUME
WANGU HATA WATOTO PIA
WAMEKUKUMBUKA NAJUA
UNANISIKILIZA NAOMBA
UNISAMEHE SANA KWA
KUTOZIKUBALI JUHUDI ZAKO
ULIPOKUWA HAI"..............
FUNDISHO:SIKU ZOTE KUBALI/
SHUKURU KILE ULICHOPEWA
HAIJAISHI NI KIKUBWA AMA
KIDOGO
:MAPENZI SIO NI KIASI GANI YA
TULICHONACHO BALI NI JINSI GANI
TUNAGAWANA KILE KIDOGO
TULICHOBALIKIWA NA MUNGU..
 
Last edited by a moderator:
Well said Buji Buji: Kina dada zetu hujisahau sana linapokuja suala la kipato, na hupenda comparison na majirani. Mtu unaweza ukajitutumua haswa na vihela vyako vichache kununua zawadi ila response utakayopata utakoma na roho yako. Ohh nataka designer clothes, shoes za italy, perfume ya france , wine ya south africa wakati ndio kwanza tumeanza maisha na anaona kipato changu ni cha kawaida. At the same time anakwambia ooh tujenge , tununue gari etc.
Bottom line is--- Lets learn to be Thankful for all things and appreciate the present moment, hoping for a better, bigger tomorrow!!
 
Well said Buji Buji: Kina dada zetu hujisahau sana linapokuja suala la kipato, na hupenda comparison na majirani. Mtu unaweza ukajitutumua haswa na vihela vyako vichache kununua zawadi ila response utakayopata utakoma na roho yako. Ohh nataka designer clothes, shoes za italy, perfume ya france , wine ya south africa wakati ndio kwanza tumeanza maisha na anaona kipato changu ni cha kawaida. At the same time anakwambia ooh tujenge , tununue gari etc.
Bottom line is--- Lets learn to be Thankful for all things and appreciate the present moment, hoping for a better, bigger tomorrow!!

mwenye masiko na asikie... mwenye macho na aone...
 
sijui kwann binadamu tumeumbwa namna hii,
huwaga siku zote huwez kuona thaman ya itu hadi ukipoteze ndipo unapoona thaman yake. mathalani hata nguo yako uliyovaa waweza kuikalia popote pale pasi kujali usafi na usalama wa nguo yako lkn pindi itakapharibika na kushidwa kuvalika na ukopunuza idadi ya nguo basi ndipo majuto hutujia.

binadamu yyte yule huwa anathaman yake, iwe yuko na uwezo ama la, sasa anapoweka chachu ya ukarimu basi thamani yake uzidi kupanda maradufu.

kuna msemo mmoja niliwahi kuuona kwenye duka moja la muhindi pale moshi mjini zamani sana ulisome hivi ...............I WAS COMPLAINING I HAVE NO SHOES UNTILL ISAW A MAN WITH NO FOOT.

SO tujifunze kuwa watu wa shukuran hata kwa kidogo tunachopewa, ukishukuru kwa kipande cha nguru si haba basi hata papa utapewa.
 
noted............... lakini hata wale malecturer wanaogawa ''C'',supp na carry na wao tulidhike nao.
 
Hii nimeipenda...good message to these modern women we have! well done mzee,
 
Back
Top Bottom