Hana hisia kabisa na mke wake wa ndoa

scientificall

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
442
288
Habari za mda huu wana jamvi ameniomba nifikishe uzi huu yaezekana akapata suruhisho au ushauri kutoka kwetu kwani hili ni jukwaa muhimu sana katika hili.

Ni mtoto wa mjomba angu ambae ni wakiume.

Kutokana na ukaribu wangu nae haswa katika kumshaur mambo mbali mbali katika maisha toka bado anasoma mpaka amepata ajira na sasa yupo katika ndoa.

Kutokana na hili basi aliamua kunifikishia suala hili ambalo kwa haswa ni la kifamilia.

Mwanzoni mwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana alifunga ndoa na binti mdogo ambaye alifanyiwa connection na ndugu zake.

Baada ya ndoa ndugu yangu huyu amekuwa na upendo wa kawaida sana kwa mke wake kwani amejitahidi hata kutengeneza mazingira ya kudumisha upendo lakini hali bado ni ile ile.

Anadai imefikia kipindi mpaka hafurahii kuwa nyumbani na hata mke wake akihitaji sex yeye anaona kama ni usumbufu.

Imefikia kipindi hadi kwenye ndoto anaota amelala na mtu mwingine ambae sio mke wake na hata kufikia wakati mpaka moyoni anajisemea haswa huyu sio mke niliyemtaka mimi kwani.

Anasema mefikia kipindi mpaka nawaza kumuacha mke wangu na hata sifurahii tendo la ndoa bali nafanya kumlidhisha mke wangu.

Hivi juzi niliota ninamfanyia mpango mke wangu aolewe na mtu mwingine. Na hata ninashindwa kukaa na raha niwapo nyumbani na mke wangu kwani bado naona sio chaguo sahihi kwangu anasema.

Nimeshawazia mengi sana kuhusu hii ndoa yangu. Anasema pia upande wa mke wake yeye anampenda kwa dhati na kutimiza majukumu yote kama mama wa nyumbani na haswa kuhakikisha mme wake anakuwa na furaha mda wote.

Ndoa ndo bado changa hawana hata mtoto na sasa ndg angu anawaza kumuacha mke wake huyu ili atafute chaguo lake.

Naomba tumshauri kwa kina na sio matusi wala kejeli tulitendee haki jukwaa hili kwa ndg yetu huyu.

Nawasilisha......
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
4,258
7,492
Ni kheri kuishi na akupendae kama huyo ndugu yako, kuliko kuishi na mtu ambae yeye hakupendi na wewe unampenda.

Anajitaftia matatizo tu kumuacha huyo mwanamke, kama anampenda, ana tabia njema na anamjali ajifunze kumpenda taratibu kwa hayo mazuri yake machache.
 

Mr DIY

JF-Expert Member
Dec 24, 2016
735
1,099
Habari za mda huu wana jamvi ameniomba nifikishe uzi huu yaezekana akapata suruhisho au ushauri kutoka kwetu kwani hili ni jukwaa mila mtu hata ukinunua gari kwa mara ya kwanza, siku za mwanzo utajilaumu kwann umeleta kitu kinachokutesa ila ukishazoea hutampenda kwa asilimia 100% lakini utaona umuhimu wa kuwa na mke nyumbani.

Mambo ya mpito hayo cha msingi afanye majukumu yake kama kawaida kwa kipindi hiki, asiache kutoka nae out, kwenye sherehe au kitu kitakacho waunganisha kama mke na mme, asiwe mtu wa kukaa tu nyumbani na mkewe.
 

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
5,607
11,806
Mapema sana kuona umuhimu wake, inamtokea kila mtu hata ukinunua gari kwa mara ya kwanza, siku za mwanzo utajilaumu kwann umeleta kitu kinachokutesa ila ukishazoea hutampenda kwa asilimia 100% lakini utaona umuhimu wa kuwa na mke nyumbani, mambo ya mpito hayo cha msingi afanye majukumu yake kama kawaida kwa kipindi hiki, asiache kutoka nae out, kwenye sherehe au kitu kitakacho waunganisha kama mke na mme, asiwe mtu wa kukaa tu nyumbani na mkewe.
Ushawahi kuishi na mtu ambaye humpendi? Ndugu hakuna kitu kinachosha kama kuishi na mtu humpendi, akipita atakukera, akila atakukera, akipumua atakukera yaani kila kitu kitakukera.

Yaani wewe unazungumzia kutoka naye out, kuna watu hawaongozani out na wapenzi wao popote kisa hawawapendi. Na kama mtu unampenda hata akiwa mbaya utaongozana nae popote na utakuwa proud nae hutomficha utamtambulisha kwa kila mtu. Mtu akiwa hakupendi atakuficha kama ARV mkuu.

Mapenzi yanatakiwa tu yabalance hata kama sio 50/50 hata ikiwa 40/60 pia sio mbaya, yakiegamia upande mmoja sana, ujue mtu mmoja ataishi kwa mateso maisha yake yote.
 

Mr DIY

JF-Expert Member
Dec 24, 2016
735
1,099
Ushawahi kuishi na mtu ambaye humpendi? Ndugu hakuna kitu kinachosha kama kuishi na mtu humpendi, akipita atakukera, akila atakukera, akipumua atakukera yaani kila kitu kitakukera.

Yaani wewe unazungumzia kutoka naye out, kuna watu hawaongozani out na wapenzi wao popote kisa hawawapendi. Na kama mtu unampenda hata akiwa mbaya utaongozana nae popote na utakuwa proud nae hutomficha utamtambulisha kwa kila mtu. Mtu akiwa hakupendi atakuficha kama ARV mkuu.

Mapenzi yanatakiwa tu yabalance hata kama sio 50/50 hata ikiwa 40/60 pia sio mbaya, yakiegamia upande mmoja sana, ujue mtu mmoja ataishi kwa mateso maisha yake yote.
Sawa hampendi, lakini ameshamuoa ana nafasi ya kuokoa penzi lake kwa sasa, atoke nae kwa kujilazimisha hivyohivyo wakafurahie wanachokipenda huenda kikawaunganisha
 

LITA2019

JF-Expert Member
Dec 18, 2019
488
985
Kwa wengi waliooa hali hiyo ni ya kawaida na huisha. Atambue kwamba hata aoe mwanamke wa namna gani hali hiyo ipo paleaple. Haijalishi mrembo au chaguo lake kiasi gani lazima hali hiyo ijitokeze.

Ndio maana tunashauriwa tuoe tukiwa tumekomaa kiakili ili kuhandle hali kama hizi bila kuumizana kihisia mana ni temporary.

Ni hulka ya binadamu kukichoka kitu ambacho ameshakipata na kukizoea. Na hata wake zetu wanapitia hali kama hizo, ni kawaida.

Kitu pekee kinachosaidia katika hali hii ni ukomavu wa wahusika katika kupambana nayo na kuvuka.

Kama mkiwa matured huisha na maisha kuendelea kama kawaida, ni kipindi ambacho ndoa nyingi huyumba/kuvunjika kabisa kama inavyoelekea hiyo ya mdau

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,693
2,925
Kwa maelekezo yako labda ana chezewa na mtu au jini mahaba ni ngumu kuamini Ila mtu Hadi umemuowa ndyo hisia zikatee kuna kitu na kama anataka kuokoa ndoa yake akifanyie kazii kingine akili yake isitizame makosa ya mkewe au madhaifu ya mkewe aipe akili ya kufurahia kile alichonacho mkewe labda anajilaumu kwann kaowa Kwa kuangalia marafiki au watu wake WA karibu mwambie yupo sehemu sahihi
 

Semahengere

JF-Expert Member
Nov 29, 2020
949
1,524
Kama anaota ndoto kama hiyo maana yake ni hii;
Alichepuka alafu nafsi yake ikakamatwa
Sorry hili jibu ni la kiroho lakini jitahidi kunielewa.

Bible Inasema, Alalaye na kahaba amefanyika mwili mmoja nae.
Kwa hiyo sasa Jamaa ni mume wa zaidi ya Mke mmoja
Kumbuka huwezi kutumikia Mabwana wawili so lazima amchukie mmoja ampende mwingine
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom